Leo ilipaswa kuwa mwaka 2031, Error katika upangaji wa Calender imetufanya tuwe 2024

calendar ni man made thing, civilization nyingi zina calendar tofauti, sisi tunafuata ya wakoloni wetu(Gregorian calendar ), sio kila nchi leo ni 2024, mfano Ethiopia leo ni 2014
kwahyo mkuu nikitoka Hapa tz nikaingia Ethiopia simu yangu itaniambia ni 2/7/2014?
 
Zamani kalenda iliyokua ikitumika ilikua haiendani na mzunguko wa dunia kuizunguka jua, kwa hiyo majira yakawa yanabadilika mfano mwaka huu mvua zinanyesha mwezi wa 7, mwaka ujao zinanyesha mwezi wa 12, na kadhalika. Hii ni kwa sababu kalenda ilikua inapishana na jinsi dunia inavyozunguka jua.

Mwaka 45 KK (kama tunavyoujua kwa sasa), Julius Caesar alipanga kalenda upya ili iendane na mzunguko wa dunia. Akaweka mfumo wa kuwa na mwaka mrefu wenye siku 366 kila baada ya miaka mitatu yenye siku 365. Akaweza kupata wastani wa mwaka wenye siku 365.25 ambao ukawa unaendana na mzunguko wa dunia kwa kiasi kikubwa. Hii kalenda inaitwa Kalenda ya Julian.

Karne ya 6, takriban mwaka 525 BK, kulikuwa na mwanafunzi wa dini anayeitwa Dionysius Exiguus ambaye alianzisha mfumo wa kuhesabu miaka kutokana na mwaka aliozaliwa Yesu. Baada ya uchambuzi na mahesabu alizofanya, mwaka aliozaliwa Yesu aliuita 1 BK (Anno Domini), 2 BK, 3 BK, na kadhalika. Mwaka mmoja kabla ya kuzaliwa Yesu aliuita 1 KK (Before Christ), 2 KK, 3 KK, na kadhalika.

Kabla ya hapo, miaka ilihesabiwa kutokana na matukio, utawala, na kadhalika. Kwa Dola ya Kirumi, miaka ilihesabiwa kutokana na kuzaliwa kwa Dola ya Roma. Mfano mwaka 45 KK ambapo Julius Caesar alirekebisha kalenda ulikua ukijulikana kama mwaka 709. Kwa hiyo iliendelea kuhesabiwa hivyo hadi takriban mwaka 525 BK ambapo mfumo wa huyo mwanafunzi wa dini ukaanza kusambaa wa kuhesabu kuanzia mwaka aliozaliwa Yesu.

Kalenda ya Julian bado ilikua na makosa kwa kiasi fulani. Mwaka 1582 ikazaliwa kalenda mpya iliyorekebisha makosa kwenye Kalenda ya Julian, inaitwa Kalenda ya Gregorian. Hii kalenda tunayotumia sasa inaitwa Kalenda ya Gregorian ilianzishwa na Papa Gregory XIII mwaka 1582 ili kurekebisha mpangilio uliokuwepo kwenye Kalenda ya Julian. Kalenda ya Julian ilikuwa na wastani wa siku 365.25, ila kiuhalisia dunia inatumia siku 365.2424 kumaliza mzunguko wake kuzunguka jua. Kwa hiyo kutokana na Kalenda ya Julian, baada ya muda mrefu mzunguko wa dunia unapishana na kalenda.

(kafatilie mabadiliko yaliyofanywa ila siku 10 zikapunguzwa)

Kwanini Sasa Sio 2024?​

  1. Mwanafunzi wa dini aliyeanzisha mfumo wa kuhesabu miaka kwa kuzingatia mwaka aliozaliwa Yesu aliupanga mwaka aliozaliwa Kristo kuwa 1 BK. Mwaka kabla ya 1 BK aliuita 1 KK, kwa hiyo hakuna mwaka sifuri, maana yake ni lazima kuna mwaka umerukwa hapo kati.
  2. Kutokana na teknolojia ya sasa, wanasayansi wa anga (astronomers) wanaweza kuunda tena nafasi ya vitu vya anga: sayari, nyota, na kadhalika kama vilivyoonekana miaka mingi iliyopita. Kutokana na vitabu vya Injili vinavyoelezea kuzaliwa kwa Kristo, Injili ya Mathayo inaongelea kuonekana kwa nyota juu ya anga la Bethlehem ambayo iliwaongoza wanajimu. Kutokana na astronomia, mwaka 1 BK hakukuwa na nyota wala kitu chochote kilichoonekana angani. Ila mwaka 7 KK sayari Saturn na Jupiter zilikingiliana mara tatu ndani ya miezi tisa juu ya anga la Bethlehem (planetary conjunction), kitu kinachofanya ikiangaliwa kutoka duniani inaonekana kama nyota inayong'aa sana.

Kwanini 7 KK ni Muhimu Zaidi Licha ya Kuwa Conjunction ni Kawaida Kutokea?​

Conjunction ya 2 KK ya Jupiter na Venus iliyoonekana kama nyota inayong'aa sana Bethlehem, haina umuhimu sana kwa sababu ilitokea mara moja mwaka 2 KK na imewahi kujirudia sehemu mbalimbali baada ya miaka fulani. Mfano 66 BK, hata mwaka 2021 pia kulikuwa na conjunction ya Jupiter na Saturn.

Umuhimu wa Triple Conjunction ya 7 KK​

  1. Conjunction ya 7 KK imejirudia mara tatu ndani ya mwaka mmoja, Triple Conjunction, na haijawahi kujirudia kutokea hivyo tena (mara tatu ndani ya mwaka mmoja).
  2. Kutokana na Injili ya Mathayo, nyota iliwaongoza wanajimu watatu kutoka sehemu mbali mbali kwenda Bethlehem (ambazo pia zilikuwa ni mbali sana na Bethlehem). Conjunction ya 2 KK ilionekana mara moja tu hivyo isingeweza kuwaongoza. Conjunction ya 7 KK ya Saturn na Jupiter imeonekana mara 3 ndani ya miezi tisa, kwa hiyo ni likely kuwaongoza wanajimu kutoka sehemu ya mbali.
(ukitaka kujua zaidi fuatilia triple conjunction of Saturn and Jupiter of 7 KK)

Kwa hiyo, kulingana na astronomia ya kisasa, upangaji wa miaka kwa kadiri ya mwanafunzi wa dini Dionysius Exiguus ulikuwa na makosa ya miaka 7 ambayo inaweka huu mwaka kuwa 2024 badala ya 2031.

Ambacho Huenda Hukukijua Kabla​

Tarehe inayofuata baada ya tarehe 4/10/1582 ni tarehe 15/10/1582. Yaani baada ya tarehe 4 ilifuata tarehe 15 (kutokana na kuhama kutoka kutumia Kalenda ya Julian kwenda kwenye Kalenda ya Gregorian). Pia kwa mtazamo mwingine utaona ni jinsi gani Roma na Kanisa Katoliki limekuwa na nguvu na ushawishi kwenye mifumo tunayotumia hadi sasa.
Inawezekana ikawa Kweli maana waislamu wapo mwaka wa 1400 ndio maana wanatuambia haramu na kafiri sababu wajafikia
 
calendar ni man made thing, civilization nyingi zina calendar tofauti, sisi tunafuata ya wakoloni wetu(Gregorian calendar ), sio kila nchi leo ni 2024, mfano Ethiopia leo ni 2014
Sahihi
Kalenda haihusiani na Mungu wala nini

Ziko calenda nyingi sana duniani

Mfano kuna Ethiopian calendar kwao mwaka huu wa 2024 kwao ni 2014

Ukija kwa waislamu wana kalenda yao mwaka huu wa 2024 kwao ni mwaka 1400

Kuna kalenda ingine ya Korea kaskazini wao huanza kalenda yao huanzia mwaka aliozaliwa Mwanzilishi wa nchi Kim ili Sung kwao mwaka 2024 ni mwaka wa 103 Kalebda yao inaitwa Juche Calendar

Ziko nyingine nyingi .tu
 
swali langu bado halijajibiwa mkuu
Screenshot_20240702-071331.png
 
Duuuh watu as if mnalipwa kuchimba haya madude ya astronomy
Yaani yye anafanya effortlessly Tena anaenjoi Kama ambavyo huwa naona wanaongelea Mpira ama siasa utadhani wanalipwa.
Kuna watu Wana hobby tu ya ku explore history, knowledge,kusoma Mambo mbalimbali kuhusiana na binadamu na dunia anayoishimo.
Sasa Kuna mwingine anachambua namna ya kuitafuna k Ila hakuna anayemshangaa kabisa anaona kawaida.
Yaani mtu anaweza akasoma Uzi wa kimasihara ama romantic novel page 5000 Ila ishu ya maarifa hata namna ya kutunza ubongo ama vital organs like liver, kidney and heart ya page 50 akawa mvivu.
So pia na huyu anayependa kusoma kuhusiana na maarifa ya dunia anamshangaa huyo anayesoma page 6000 za romantic novel.
Ni ishu ya priority, interests na desire ama moyo aka feelings.
Ni sawa na mtu aliye train mwili wake kufanya zoezi ama aka train moyo wake ama akili kusali mara kumi kwa siku. Yaani wewe ambaye hujafunza mwili na akili yako kufanya hayo Mambo unashangaa anawezaje kufanya zoezi Kila siku wakati yeye ameshajizoesha anafanya bila hata ya mental resistance,yaani hakuna ugumu wowote katika moyo,hisia,kiakili na kiroho ni sawa unavyonawa uso.
Naye anakushangaa anasema mbona ni vyepesi mno kufanya tizi Kila siku asubuhi ama kusali mara kumi kwa siku.
Ukienda kuangalia hakuna unamchozidi kuwa labda wewe hupotezi muda kusali ama kufanya tizi.
Mfano unapata uvivu unalala unashindwa kuamka uende kulima since labda saa 10 asubuhi saa mbili ama saa tatu uwe umerudi home.
Mtu ataenda atalima atarudi atakukuta hapo hapo umekaa unakuta jua.

Ishu kubwa ni discipline.
Pia nb we build the behavior then behavior build us
 
mkuu, kigezo cha kua na Callender nyingi utakitumia kusema Mungu hayupo ?

mbona hata miungu ni mingi ila Mungu mkuu ni mmjoja

Callender pia ni ningi ila reference kuu ya kidunia ni Callender hii ya Gregorian

Fungua akili kwa falsafa pana.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kimantiki na kidhana ni mnyoofu kiasi kwamba angekuwepo, ingejulikana kalenda yake moja ya msingi, ingejulikana wazi, na ingejulikana kwa viumbe wote, bila utata wowote wala shida ya kujifunza chochote. Yani tungeijua kama tunavyojua kupumua, tungeijua bila kufundishwa, tungeijua tangu tunazaliwa.

Matatizo ya kujua kalenda iliyonyooka na kujua Mungu wa kweli ni yupi kiujumla yameua watu wengi sana, Mungu huyo angekuwepo asingeachia matatizo haya yaendelee, kuachia hivyo kuna contradict characters zake za ujuzi wa yote, uwezo wote na upendo wote.

Hakuna Mungu mkuu mmoja. Hiyo ni imani yako tu. Hakuna Mungu, hadithi za Mungu zimetungwa na watu tu.

Ukweli kwamba watu hatuelewani kuhusu Mungu yupo au hayupo, na hata wanaokubali Mungu yupo hawakubaliani Mungu wa kweli ni yupi unaonesha Mungu hayupo.

Umeelewa?

Au unahitaji mifano ya kimantiki na ithibati?

Mungu angekuwepo, hata ubishani wa akuwepo Mungu usingewezekana.

Kila kiumbe kingejua Mungu yupo, kingejua bila utata, kingejuabkwa ukamilifu, kingejua muda wote.
 
Yaani yye anafanya effortlessly Tena anaenjoi Kama ambavyo huwa naona wanaongelea Mpira ama siasa utadhani wanalipwa.
Kuna watu Wana hobby tu ya ku explore history, knowledge,kusoma Mambo mbalimbali kuhusiana na binadamu na dunia anayoishimo.
Sasa Kuna mwingine anachambua namna ya kuitafuna k Ila hakuna anayemshangaa kabisa anaona kawaida.
Yaani mtu anaweza akasoma Uzi wa kimasihara ama romantic novel page 5000 Ila ishu ya maarifa hata namna ya kutunza ubongo ama vital organs like liver, kidney and heart ya page 50 akawa mvivu.
So pia na huyu anayependa kusoma kuhusiana na maarifa ya dunia anamshangaa huyo anayesoma page 6000 za romantic novel.
Ni ishu ya priority, interests na desire ama moyo aka feelings.
Ni sawa na mtu aliye train mwili wake kufanya zoezi ama aka train moyo wake ama akili kusali mara kumi kwa siku. Yaani wewe ambaye hujafunza mwili na akili yako kufanya hayo Mambo unashangaa anawezaje kufanya zoezi Kila siku wakati yeye ameshajizoesha anafanya bila hata ya mental resistance,yaani hakuna ugumu wowote katika moyo,hisia,kiakili na kiroho ni sawa unavyonawa uso.
Naye anakushangaa anasema mbona ni vyepesi mno kufanya tizi Kila siku asubuhi ama kusali mara kumi kwa siku.
Ukienda kuangalia hakuna unamchozidi kuwa labda wewe hupotezi muda kusali ama kufanya tizi.
Mfano unapata uvivu unalala unashindwa kuamka uende kulima since labda saa 10 asubuhi saa mbili ama saa tatu uwe umerudi home.
Mtu ataenda atalima atarudi atakukuta hapo hapo umekaa unakuta jua.

Ishu kubwa ni discipline.
Pia nb we build the behavior then behavior build us
hii ni kweli aisee mkuu

mimi nadhani hata vigezo vya kutetea kua hayupo vinakosa mantiki

na vinatokana na kua na maarifa madogo kumhusu
 
Hata kama kalenda imerudi nyuma, Wewe inakuathiri vipi?

By the way, Kumbuka Waislam wao wako mwaka 1400 hivi Sasa!
Mwaka wa kislam unatumika msikitini na shughuli za kidini,huku duniani hatuutambui
 
Yaani yye anafanya effortlessly Tena anaenjoi Kama ambavyo huwa naona wanaongelea Mpira ama siasa utadhani wanalipwa.
Kuna watu Wana hobby tu ya ku explore history, knowledge,kusoma Mambo mbalimbali kuhusiana na binadamu na dunia anayoishimo.
Sasa Kuna mwingine anachambua namna ya kuitafuna k Ila hakuna anayemshangaa kabisa anaona kawaida.
Yaani mtu anaweza akasoma Uzi wa kimasihara ama romantic novel page 5000 Ila ishu ya maarifa hata namna ya kutunza ubongo ama vital organs like liver, kidney and heart ya page 50 akawa mvivu.
So pia na huyu anayependa kusoma kuhusiana na maarifa ya dunia anamshangaa huyo anayesoma page 6000 za romantic novel.
Ni ishu ya priority, interests na desire ama moyo aka feelings.
Ni sawa na mtu aliye train mwili wake kufanya zoezi ama aka train moyo wake ama akili kusali mara kumi kwa siku. Yaani wewe ambaye hujafunza mwili na akili yako kufanya hayo Mambo unashangaa anawezaje kufanya zoezi Kila siku wakati yeye ameshajizoesha anafanya bila hata ya mental resistance,yaani hakuna ugumu wowote katika moyo,hisia,kiakili na kiroho ni sawa unavyonawa uso.
Naye anakushangaa anasema mbona ni vyepesi mno kufanya tizi Kila siku asubuhi ama kusali mara kumi kwa siku.
Ukienda kuangalia hakuna unamchozidi kuwa labda wewe hupotezi muda kusali ama kufanya tizi.
Mfano unapata uvivu unalala unashindwa kuamka uende kulima since labda saa 10 asubuhi saa mbili ama saa tatu uwe umerudi home.
Mtu ataenda atalima atarudi atakukuta hapo hapo umekaa unakuta jua.

Ishu kubwa ni discipline.
Pia nb we build the behavior then behavior build us
Mkuu haya madude tatizo ni magumu ndo mana nashangaa hii astronomy nina vitabu vyake kama vitatu hivi lakini nashindwa kuelewa kabisa...

Sasa assume jamaaa anasoma then anaelewa kile kitu anakuja ana explain kwetu aiseee unazani hiyo ni kitu simple...

Kuna watu wanaletaga vitu hapa kwa msaada wa Google translate ila huyu jamaa yeye ka deep down kaelewa concepts nzima..

Daaah mi mtu wa namna hii huwa na m term as genius.. mkuu astronomy ni ngumu wewe...

Naona madogo wanaosoma Bsc in physics inavyo wakalisha hii kitu acha kabisa..

Jamaa apewe maua yake..
Yaani kama kuchambua hayo mambo ni burudani yake assume tuu kama anakuaga na muda wa watoto huyu jamaa ahahahahha.
Ila salout kwako NadeOj aiseeee
 
Back
Top Bottom