Leo ilipaswa kuwa mwaka 2031, Error katika upangaji wa Calender imetufanya tuwe 2024

Calendar ni man made thing na zipo nyingi sana, mungu hahusiki hapo
Mungu hahusiki, kwa sababu hayupo.

Angekuwapo, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hata calendar zisingekuwa nyingi.

Ingekuwa moja tu ya Mungu.

Kuwepo kwa kalenda nyingi nako ni ushahidi Mungu hayupo.
 
Hiyo common era haianzii na mwaka wa Yesu kuzaliwa. Hii ndiyo habari nzima iliyosababisha huu uzi.

Kama Yesu ni Mungu kweli kaashindwaje kuwafanya hao walioweka kalenda kuweka mwaka halisi aliozaliwa Yesu?

Yani Mungu kashindwa kupanga hesabu za kalenda tuanze kuhesabu miaka alipozaliwa yeye?
Leo hii ni AD 2024 au 2024 CE utasemaje sio kitu hicho hicho?
 
Gregorian calendar
Julian calendar
Lunar calendar
Islamic calendar

Hizi zote zipo tofauti. Hata wewe unaweza kuwa na calender yako na ukaifuata maisha yataendela vile vile.

Au tatizo katiba 😅
 
Una matumizi mabaya ya akili,unapoteza usingizi wako bure tu sasa hivi saa 7 usiku kwa ajili ya kubishana na facts
 
Zamani kalenda iliyokua ikitumika ilikua haiendani na mzunguko wa dunia kuizunguka jua, kwa hiyo majira yakawa yanabadilika mfano mwaka huu mvua zinanyesha mwezi wa 7, mwaka ujao zinanyesha mwezi wa 12, na kadhalika. Hii ni kwa sababu kalenda ilikua inapishana na jinsi dunia inavyozunguka jua.

Mwaka 45 KK (kama tunavyoujua kwa sasa), Julius Caesar alipanga kalenda upya ili iendane na mzunguko wa dunia. Akaweka mfumo wa kuwa na mwaka mrefu wenye siku 366 kila baada ya miaka mitatu yenye siku 365. Akaweza kupata wastani wa mwaka wenye siku 365.25 ambao ukawa unaendana na mzunguko wa dunia kwa kiasi kikubwa. Hii kalenda inaitwa Kalenda ya Julian.

Karne ya 6, takriban mwaka 525 BK, kulikuwa na mwanafunzi wa dini anayeitwa Dionysius Exiguus ambaye alianzisha mfumo wa kuhesabu miaka kutokana na mwaka aliozaliwa Yesu. Baada ya uchambuzi na mahesabu alizofanya, mwaka aliozaliwa Yesu aliuita 1 BK (Anno Domini), 2 BK, 3 BK, na kadhalika. Mwaka mmoja kabla ya kuzaliwa Yesu aliuita 1 KK (Before Christ), 2 KK, 3 KK, na kadhalika.

Kabla ya hapo, miaka ilihesabiwa kutokana na matukio, utawala, na kadhalika. Kwa Dola ya Kirumi, miaka ilihesabiwa kutokana na kuzaliwa kwa Dola ya Roma. Mfano mwaka 45 KK ambapo Julius Caesar alirekebisha kalenda ulikua ukijulikana kama mwaka 709. Kwa hiyo iliendelea kuhesabiwa hivyo hadi takriban mwaka 525 BK ambapo mfumo wa huyo mwanafunzi wa dini ukaanza kusambaa wa kuhesabu kuanzia mwaka aliozaliwa Yesu.

Kalenda ya Julian bado ilikua na makosa kwa kiasi fulani. Mwaka 1582 ikazaliwa kalenda mpya iliyorekebisha makosa kwenye Kalenda ya Julian, inaitwa Kalenda ya Gregorian. Hii kalenda tunayotumia sasa inaitwa Kalenda ya Gregorian ilianzishwa na Papa Gregory XIII mwaka 1582 ili kurekebisha mpangilio uliokuwepo kwenye Kalenda ya Julian. Kalenda ya Julian ilikuwa na wastani wa siku 365.25, ila kiuhalisia dunia inatumia siku 365.2424 kumaliza mzunguko wake kuzunguka jua. Kwa hiyo kutokana na Kalenda ya Julian, baada ya muda mrefu mzunguko wa dunia unapishana na kalenda.

(kafatilie mabadiliko yaliyofanywa ila siku 10 zikapunguzwa)

Kwanini Sasa Sio 2024?​

  1. Mwanafunzi wa dini aliyeanzisha mfumo wa kuhesabu miaka kwa kuzingatia mwaka aliozaliwa Yesu aliupanga mwaka aliozaliwa Kristo kuwa 1 BK. Mwaka kabla ya 1 BK aliuita 1 KK, kwa hiyo hakuna mwaka sifuri, maana yake ni lazima kuna mwaka umerukwa hapo kati.
  2. Kutokana na teknolojia ya sasa, wanasayansi wa anga (astronomers) wanaweza kuunda tena nafasi ya vitu vya anga: sayari, nyota, na kadhalika kama vilivyoonekana miaka mingi iliyopita. Kutokana na vitabu vya Injili vinavyoelezea kuzaliwa kwa Kristo, Injili ya Mathayo inaongelea kuonekana kwa nyota juu ya anga la Bethlehem ambayo iliwaongoza wanajimu. Kutokana na astronomia, mwaka 1 BK hakukuwa na nyota wala kitu chochote kilichoonekana angani. Ila mwaka 7 KK sayari Saturn na Jupiter zilikingiliana mara tatu ndani ya miezi tisa juu ya anga la Bethlehem (planetary conjunction), kitu kinachofanya ikiangaliwa kutoka duniani inaonekana kama nyota inayong'aa sana.

Kwanini 7 KK ni Muhimu Zaidi Licha ya Kuwa Conjunction ni Kawaida Kutokea?​

Conjunction ya 2 KK ya Jupiter na Venus iliyoonekana kama nyota inayong'aa sana Bethlehem, haina umuhimu sana kwa sababu ilitokea mara moja mwaka 2 KK na imewahi kujirudia sehemu mbalimbali baada ya miaka fulani. Mfano 66 BK, hata mwaka 2021 pia kulikuwa na conjunction ya Jupiter na Saturn.

Umuhimu wa Triple Conjunction ya 7 KK​

  1. Conjunction ya 7 KK imejirudia mara tatu ndani ya mwaka mmoja, Triple Conjunction, na haijawahi kujirudia kutokea hivyo tena (mara tatu ndani ya mwaka mmoja).
  2. Kutokana na Injili ya Mathayo, nyota iliwaongoza wanajimu watatu kutoka sehemu mbali mbali kwenda Bethlehem (ambazo pia zilikuwa ni mbali sana na Bethlehem). Conjunction ya 2 KK ilionekana mara moja tu hivyo isingeweza kuwaongoza. Conjunction ya 7 KK ya Saturn na Jupiter imeonekana mara 3 ndani ya miezi tisa, kwa hiyo ni likely kuwaongoza wanajimu kutoka sehemu ya mbali.
(ukitaka kujua zaidi fuatilia triple conjunction of Saturn and Jupiter of 7 KK)

Kwa hiyo, kulingana na astronomia ya kisasa, upangaji wa miaka kwa kadiri ya mwanafunzi wa dini Dionysius Exiguus ulikuwa na makosa ya miaka 7 ambayo inaweka huu mwaka kuwa 2024 badala ya 2031.

Ambacho Huenda Hukukijua Kabla​

Tarehe inayofuata baada ya tarehe 4/10/1582 ni tarehe 15/10/1582. Yaani baada ya tarehe 4 ilifuata tarehe 15 (kutokana na kuhama kutoka kutumia Kalenda ya Julian kwenda kwenye Kalenda ya Gregorian). Pia kwa mtazamo mwingine utaona ni jinsi gani Roma na Kanisa Katoliki limekuwa na nguvu na ushawishi kwenye mifumo tunayotumia hadi sasa.
Ujinga tu na kunichosha na story za kufikirika kama hizi 😀😀😀 sasa kama sio 2024 mbona ni 2024 mkuu izo ni story za kufikirika tu sema unataka kujionyesha kwamba na wewe unajua historia kumbe nonsense
 
sawa
 
Dakika, sekunde, saa, siku, wiki, mwezi mwaka ni illusion tuu hakuna kitu chochote kinachothibitisha hayo mambo.
ndio, ila zimewekwa ili kupima muda na kuupanga, ndo maana kila mwaka miezi ina sifa zinazifanana

mfano kipindi cha baridi, joto, mvua etc
 
calendar ni man made thing, civilization nyingi zina calendar tofauti, sisi tunafuata ya wakoloni wetu(Gregorian calendar ), sio kila nchi leo ni 2024, mfano Ethiopia leo ni 2014
ila ambayo inatambulika official kidunia kama reference ni Gregorian

kwasababu ndo yenye mpangilio unaokubalika zaidi upo accurate zaidi
 
Leo hii ni AD 2024 au 2024 CE utasemaje sio kitu hicho hicho?
kitu ndo hicho hicho labda u replace to neno BC na BCE au AD na CE

ila namba zinabaki zile kwasababu ndo reference iliyotumika kwa zaidi ya miaka 2000
 
Mungu hahusiki, kwa sababu hayupo.

Angekuwapo, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hata calendar zisingekuwa nyingi.

Ingekuwa moja tu ya Mungu.

Kuwepo kwa kalenda nyingi nako ni ushahidi Mungu hayupo.
mkuu, kigezo cha kua na Callender nyingi utakitumia kusema Mungu hayupo ?

mbona hata miungu ni mingi ila Mungu mkuu ni mmjoja

Callender pia ni ningi ila reference kuu ya kidunia ni Callender hii ya Gregorian
 
Gregorian calendar
Julian calendar
Lunar calendar
Islamic calendar

Hizi zote zipo tofauti. Hata wewe unaweza kuwa na calender yako na ukaifuata maisha yataendela vile vile.

Au tatizo katiba 😅
sio tu katiba, kwamba iwe ndo reference ya kidunia
 
ndio, ila zimewekwa ili kupima muda na kuupanga, ndo maana kila mwaka miezi ina sifa zinazifanana

mfano kipindi cha baridi, joto, mvua etc
Hiyo n nature tuu Ipo hvy kuwa ikitoka majira fulani ifate majira fulani
 
Zamani kalenda iliyokua ikitumika ilikua haiendani na mzunguko wa dunia kuizunguka jua, kwa hiyo majira yakawa yanabadilika mfano mwaka huu mvua zinanyesha mwezi wa 7, mwaka ujao zinanyesha mwezi wa 12, na kadhalika. Hii ni kwa sababu kalenda ilikua inapishana na jinsi dunia inavyozunguka jua.

Mwaka 45 KK (kama tunavyoujua kwa sasa), Julius Caesar alipanga kalenda upya ili iendane na mzunguko wa dunia. Akaweka mfumo wa kuwa na mwaka mrefu wenye siku 366 kila baada ya miaka mitatu yenye siku 365. Akaweza kupata wastani wa mwaka wenye siku 365.25 ambao ukawa unaendana na mzunguko wa dunia kwa kiasi kikubwa. Hii kalenda inaitwa Kalenda ya Julian.

Karne ya 6, takriban mwaka 525 BK, kulikuwa na mwanafunzi wa dini anayeitwa Dionysius Exiguus ambaye alianzisha mfumo wa kuhesabu miaka kutokana na mwaka aliozaliwa Yesu. Baada ya uchambuzi na mahesabu alizofanya, mwaka aliozaliwa Yesu aliuita 1 BK (Anno Domini), 2 BK, 3 BK, na kadhalika. Mwaka mmoja kabla ya kuzaliwa Yesu aliuita 1 KK (Before Christ), 2 KK, 3 KK, na kadhalika.

Kabla ya hapo, miaka ilihesabiwa kutokana na matukio, utawala, na kadhalika. Kwa Dola ya Kirumi, miaka ilihesabiwa kutokana na kuzaliwa kwa Dola ya Roma. Mfano mwaka 45 KK ambapo Julius Caesar alirekebisha kalenda ulikua ukijulikana kama mwaka 709. Kwa hiyo iliendelea kuhesabiwa hivyo hadi takriban mwaka 525 BK ambapo mfumo wa huyo mwanafunzi wa dini ukaanza kusambaa wa kuhesabu kuanzia mwaka aliozaliwa Yesu.

Kalenda ya Julian bado ilikua na makosa kwa kiasi fulani. Mwaka 1582 ikazaliwa kalenda mpya iliyorekebisha makosa kwenye Kalenda ya Julian, inaitwa Kalenda ya Gregorian. Hii kalenda tunayotumia sasa inaitwa Kalenda ya Gregorian ilianzishwa na Papa Gregory XIII mwaka 1582 ili kurekebisha mpangilio uliokuwepo kwenye Kalenda ya Julian. Kalenda ya Julian ilikuwa na wastani wa siku 365.25, ila kiuhalisia dunia inatumia siku 365.2424 kumaliza mzunguko wake kuzunguka jua. Kwa hiyo kutokana na Kalenda ya Julian, baada ya muda mrefu mzunguko wa dunia unapishana na kalenda.

(kafatilie mabadiliko yaliyofanywa ila siku 10 zikapunguzwa)

Kwanini Sasa Sio 2024?​

  1. Mwanafunzi wa dini aliyeanzisha mfumo wa kuhesabu miaka kwa kuzingatia mwaka aliozaliwa Yesu aliupanga mwaka aliozaliwa Kristo kuwa 1 BK. Mwaka kabla ya 1 BK aliuita 1 KK, kwa hiyo hakuna mwaka sifuri, maana yake ni lazima kuna mwaka umerukwa hapo kati.
  2. Kutokana na teknolojia ya sasa, wanasayansi wa anga (astronomers) wanaweza kuunda tena nafasi ya vitu vya anga: sayari, nyota, na kadhalika kama vilivyoonekana miaka mingi iliyopita. Kutokana na vitabu vya Injili vinavyoelezea kuzaliwa kwa Kristo, Injili ya Mathayo inaongelea kuonekana kwa nyota juu ya anga la Bethlehem ambayo iliwaongoza wanajimu. Kutokana na astronomia, mwaka 1 BK hakukuwa na nyota wala kitu chochote kilichoonekana angani. Ila mwaka 7 KK sayari Saturn na Jupiter zilikingiliana mara tatu ndani ya miezi tisa juu ya anga la Bethlehem (planetary conjunction), kitu kinachofanya ikiangaliwa kutoka duniani inaonekana kama nyota inayong'aa sana.

Kwanini 7 KK ni Muhimu Zaidi Licha ya Kuwa Conjunction ni Kawaida Kutokea?​

Conjunction ya 2 KK ya Jupiter na Venus iliyoonekana kama nyota inayong'aa sana Bethlehem, haina umuhimu sana kwa sababu ilitokea mara moja mwaka 2 KK na imewahi kujirudia sehemu mbalimbali baada ya miaka fulani. Mfano 66 BK, hata mwaka 2021 pia kulikuwa na conjunction ya Jupiter na Saturn.

Umuhimu wa Triple Conjunction ya 7 KK​

  1. Conjunction ya 7 KK imejirudia mara tatu ndani ya mwaka mmoja, Triple Conjunction, na haijawahi kujirudia kutokea hivyo tena (mara tatu ndani ya mwaka mmoja).
  2. Kutokana na Injili ya Mathayo, nyota iliwaongoza wanajimu watatu kutoka sehemu mbali mbali kwenda Bethlehem (ambazo pia zilikuwa ni mbali sana na Bethlehem). Conjunction ya 2 KK ilionekana mara moja tu hivyo isingeweza kuwaongoza. Conjunction ya 7 KK ya Saturn na Jupiter imeonekana mara 3 ndani ya miezi tisa, kwa hiyo ni likely kuwaongoza wanajimu kutoka sehemu ya mbali.
(ukitaka kujua zaidi fuatilia triple conjunction of Saturn and Jupiter of 7 KK)

Kwa hiyo, kulingana na astronomia ya kisasa, upangaji wa miaka kwa kadiri ya mwanafunzi wa dini Dionysius Exiguus ulikuwa na makosa ya miaka 7 ambayo inaweka huu mwaka kuwa 2024 badala ya 2031.

Ambacho Huenda Hukukijua Kabla​

Tarehe inayofuata baada ya tarehe 4/10/1582 ni tarehe 15/10/1582. Yaani baada ya tarehe 4 ilifuata tarehe 15 (kutokana na kuhama kutoka kutumia Kalenda ya Julian kwenda kwenye Kalenda ya Gregorian). Pia kwa mtazamo mwingine utaona ni jinsi gani Roma na Kanisa Katoliki limekuwa na nguvu na ushawishi kwenye mifumo tunayotumia hadi sasa.
...MUMEMUELEWA ??...[emoji848]
 
Back
Top Bottom