Guys mayai mm napita nayo mbali sana. Maana kabla sijaoa nlikuwa nakula mayai tu. Nlikuwa ndo nimeanza tu kazi miaka ya 2008, mshahara nliuona mkubwa tu kama laki5.5 hivi and nlikuwa peke yangu, na room yangu moja tu ambayo ilikuwa ndani ya nyumba na nliishi na mwenye nyumba humo humo. Inshort alinichukulia kama mtoto wake. But target yake kumbe nioe mtoto wake. Nlivyooa tu nikapewa nitisi. Asubuhi. Nachemsha maji ya kuoga naweka mayai 2 owenye birika la kuchemshia maji. Nikiwa naoga yanabaki kwenye sahani yanapoa. Nikila naondoka zangu job. Saa nne na nusu vitumbua 3 yai moja na chai nzito ya maziwa, mchana wali ama ugali ,mboga ni mayai2 na youghurt maziwa, usiku wali ama ugali na mboga ni mayai ama nyama. Haya ndo yakawa maisha yangu for 3 yrs kabla sijaanza kuishi na mpenzi wangu, maana nlimpa mimba 2006 tukiwa chuo. Na baadae 2013 kufunga ndoa. Outcome nliota maziwa yakawa makubwa kama ya baunsa, uuuwi nikaambiwa sababu ya mayai, but nlikuwa nakula ya kienyeji, pia nikanenepa sana na mwili ukawa na cholestrol nyingi.nikachukia mayai totally huwa nayala marachache sana
Naona waku mme comment sana mafuta mafuta mafutaaaaaaaaaa,
Hapo nadhani Mimi inanihusu lakn sio kwa kukaangiza huko.
Iko ivi Mimi sijaoa, naishi pekeangu na kwenye kupika ni mvivu hatari, nishashindwa kuunga mboga maana kupika mda mrefu siwezagi, maximum time kwenye kupika kwangu ni dakika 15. eti nyanya, kitunguu,hoho,karoti,viungo niunge mboga nishashindwa na sijawahi. Ambacho hua nafanya hua nanunua samaki waliochomwa kwenye MAFUTA nawapasha kwa kuwachoma tena kidogo kwenye MAFUTA napika na ugali mchezo umeisha natafunia, kama ni nyama kuchemsha naona nachelewa, naichoma kwenye MAFUTA napika na ugali ivo nakula.
Chakula changu kikuu ni ugali kwa mboga samaki/nyama nmechoma kwenye MAFUTA.
Nikibadili menu ni viazi vitamu na vyenyewe nmechoma kwenye MAFUTA hapo napiga na tangawizi yenye sukari kwa mbali, Tufauti na hapo mkate plane na tangawizi yenye sukari kwa mbali.
Kula vyakula vingine labda mamaenu mdogo anitembelee atapika ndo ntaona mchuzi uloungwa na mboga za majani pembeni. au niende mgahawani.
Hua sili sana migahawani ila inatokea kama nikimiss vyakula vingine tofauti na hivyo juu nayo ni Mara mojamoja sana.
Wakuu mnisaidie maana hayo MAFUTA nayochomea nyama/samaki iyo ni almost kila siku YANAWEZA KUNILETEA MATATIZO?
note; Mafuta ni ya alizeti ndo natumia