Leo msela mimi nimepika Wali Nazi na Mboga Nazi

monotheist

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
830
Reaction score
1,449
Leo nimepika chakula kitamu mno hasa mboga maana ilikua na viungo vingi nyenye kuleta ladha

MAHITAJI NILIYOTUMIA

Mchele nusu kilo, mafuta ya kula, viazi mviringo viwili, nusu kuku, njegere, tui la nazi, paprika, black pepper, curry powder, soya source, pilipili ya kuwasha ya unga, majani ya coriander nyanya 3, hoho ya kijani na karot

Hoho na karot nimekata vipande vikubwa kidogo na kuku niliwaweka kwenye mafuta kwa dakika 2


Majani ya coriander nilisaha pamoja na nyanya kwenye blender

Viungo nilivyotumia ili kuleta radha nzuri kwenye chakula

Mchele niliuosha kisha nikakausha maji

Wali wa nazi upo tayari kuliwa umekauka vizuri kabisa

Mboga yangu tamu ipo tayari kuliwa ni tamu mno, yenye radha na inanukia

Nacheki movie ya atlas 2024 huku napiga msosi mtamu na wenye radha nzuri
 
Mkuu hiyo mboga unakula siku ngapi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…