Leo nakupa chimbo wewe kijana uliyechapwa na maisha. Nenda sehemu hii utakuja kufanikiwa

Leo nakupa chimbo wewe kijana uliyechapwa na maisha. Nenda sehemu hii utakuja kufanikiwa

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari ndugu zangu!
Lengo la Uzi huu si kujisifu, na wala hauna maudhui ya kukashifu harakati za vijana. Usiangalie lugha iliyotumika.
Umeomba kazi mara nyingi umekosa?
Umezunguka mahali pengi nchini kufanya ujasiriamali bila mafanikio?
Umekosa elimu ya kukuwezesha kuingia kwenye soko la ajira?
Umelima bila mafanikio?
Kama jibu ni ndio basi nakushauri nenda mkoa wa Njombe wilaya ya Makete maeneo ya jamii ya Uwanji.
Huko kuna ardhi ambayo inakubali mazao ya kibiashara kwa wingi kama ;
  • Viazi mviringo
  • Parachichi
•Vitunguu swaumu
  • Tangawizi
  • Mahindi
•Miti ya mbao
N.k, nk

Kule kuna watu wakarimu, ukifika kwa timing utafanikiwa sana. Nimetembea mikoa mingi Tanzania bara na vitongoji vingi ila kule ndipo sehemu ambayo nimeona ni simple kutoboa kimaisha kwa mtu ambaye anaamua kujihusisha na kilimo na biashara za msimu.

Haiwezekani Watanzania wote wakaishi sehemu moja ila si mbaya ukakimbilia fursa mahali fulani.
Si lazima uwe na mtaji. Jilipue tu hata ukiwa na nauli tu, mambo mengine utayakuta hukohuko.
Mimi niko Dar nalima Viazi mviringo huko wasimamizi ni ndugu wa mke wangu maana ndiko nilikoolea namimi naishi Dar. Uongo mbaya napiga pesa kiasi inaniboost.

Wale watu waaminifu sana. Kizazi hiki ambacho watu wanapigwa pesa na ndugu zao wa damu wanazotuma mikoani wafanyiwe shughuli fulani ila nimeona ajabu kwa wale watu jinsi walivyo waaminifu, wanakusimamia mwanzo mpaka mwisho wanakutumia pesa yako kamili, hawaombi hata Senti. Mimi ndio nawapa. Natamani ningeenda kununua Viazi kwa wakulima mashambani ili niviingize mjini sema muda tu sina.
 
Ila hali ya hewa baadhi ya mitaa nyumbani kwetu Makete iko hivi.
Screenshot_20220703-064156.jpg
Screenshot_20220703-064102.jpg
Screenshot_20220703-064132.jpg
Screenshot_20220703-064119.jpg
 
Ya'll gonna freeze your nuts.

Asante kwa taarifa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom