Leo nakutana na mtu ananiuliza eti kati ya Juma Nature na Diamond nani zaidi?

Acheni kumlinganisha Sir kibra ,Juma nature na vitu vya kijinga
Msitu wa vina,Kiroboto,wali nazi,mwanaume halisi. Frankly huyu ndio msanii pekee niliyewahi kwenda kwenye tamasha lake. Nilienda kula Ugali akiwa na kina Soggy, Jay Mo pale Singida
 
Umetoa tafsiri ya magreat thinkers kwakweli ,nadhani hapa ndipo haswa kipimo cha kujua Nani mtabe, pressure yakwenda kumuangalia msanii akija yaani,au kubabaika ukikutana nae,
Yaa atakaebabaika akikutana nae jua uyo ndo star
 
Ungemjibu yeye ndiyo Bora zaidi.
 
Huwezi laumu maana Juma Nature landa sio generation yake. Ni sawa generation ya akina Marijani nayo ikusikie unawatajia akina Juma Nature watakushangaa pia.
 
sasa hii mada umeiweka jukwaa la mapenzi kwa lengo gani?
 
Mbona unafananisha vitu ambavyo havifanani?

Alaf ww ndo unayeleta utoto, unabishana na mtu kazaliwa 2002😄😄
 
Juma nature kiukweli alikuwa moto sana.....alikubalika na rika zote; watoto, vijana na hata wazee kutokana na aina yake ya maisha isiyokuwa na mambo meengi ya kimagharibi na kuyaishi maisha yetu ya hali ya chini. Ila kwa upande wa pesa hakuwa mjanja sana kuzimake km alivyo diamond sasa hv.
Ujanja wa mind wa kupiga mapesa (struggles) unamfanya, automatocally, akubalike kipindi hiki ila nature alikubalika mioyoni kiukweli kweli.....mpaka leo jamaa bado ana watu
 
hahahahhahahahaha khasante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…