Leo naolewa


Kwanini umeamua kufunga ndoa mamaa?
 
Hongera sana mtoto mzuri! kwa hiyo baafae mtakwenda kwenye "mwezi wa asali"! karibu sana.
 
Hongera. Karibu kwenye hiki chama kizuri. "Naye mwanamke atamtii mumewe Na Mume ampende mkewe". Zingatia "U" tatu utaenjoy kwny ndoa yako nazo ni.
1."U"- Utii
2."U"- Uaminifu
3."U"- Uvumilivu.
 
Bila Picha kamwe sintaamini habari hii. AHSANTE.
 
hakikisha unabadili ID baada ya hapo maana nakuja kukujua.......yote kwa yote kila la heri
 
Ndani ya ndoa assume mmeo atembei nje ya ndoa, nae hivyo hivyo ndoa itakuwa na raha sana, pili epuka kuchokono chokonoa Simu yake, Simu yake iwe yake na yako iwe yako, hapo utaufurahia ndoa,

Nakutakia ndoa njema na yenye furaha moniccca

Note: Nitaamini hasa ukiweka picha ya ndoa usije ukawa unatuuzia mbuzi kwenye gunia
 
Hahahaha!! miss chagga si bora hata kudinda! Kitu kimelala doroooo! Hata umwagie petrol hakiwaki! Hahahah! Bibie plz ukampende mumeooo!!! Hahah!
 
A successful marriage requires falling in love many times, always with the same person..
 
Hongera sana, ila ujue ndo mwisho wa kulala na chupi!
 
Lete kadi ya mwariko tuje hahaaaaa, hongera saana
 
Kama masihara lilitolewa tangazo watu wakaponda akatokea mjanja mmoja serious akapewa nafasi mara posa hiyo mahali ikalipwa na ndoa Leo inafungwa. Sasa nyie mliokuwa hamuamini kwamba watu wanapata wenza humu jf na kuoana ndo muamini tangu sasa na kama hamjapata tafuteni wanawake na wanaume wamo humu. Huwezi kuwa unashinda jf halafu unaenda kutafuta mchumba barabarani tafuta humuhumu. Kila la kheri moniccca ushuhuda wako unaiongezea thamani love connect.
 
Humu naamini kuna wifes/husbands material
 
"NDOA, NDOANO"
TUNAKUTAKIA BARAKA NA FURAHA TELE KATIKA MAISHA YAKO MAPYA. MPENDE MUMEO, NAE ATAKUPENDA. CHEERS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…