Scientifically speaking huwez ku-prove kuwa mungu yupo, but also Scientifically speaking, the complexity and proximity of this universe suggests there must be a Grand creator, a designer and an intellectual being.
Huwez ondoa contradictions, kweny maisha ya binadamu contradictions ni muhimu, ndizo zinatufanya tufikirie and become better everyday, hata kwa sisi tunamwamini Yesu bado tume tofautiana, tuna contradictions kibao tuu, hata wanaomwamini Muhammad nao wana contradictions kibao tuu, hata sisi watanzania ni watu wa taifa moja lakini tuna contradictions huyu ccm huyu chadema, huyu mchaga anaamini hivi huyu mwingine mmasai anaamini vingine.
Acha contradictions ziwepo, kumuamini mungu haimaanishi kusiwepo na contradictions, na hio ndio maana ya imani, kusingekuwa na contradictions isingeitwa imani, ingeitwa "fact", sasa kama wewe unataka kumwamini mungu bila contradictions ni uamuzi wako na mm nimeamua kumuamini mungu hivohivo na sintofahamu zilizopo.
Kwa nini unaona the universe suggests there must be a grand creator, a designer?
Ikiwa complexity ni lazima iwe na designer, huoni kwamba huyo designer naye itabidi awe complex zaidi ya hicho kilichokuwa designed, kiasi kwamba na yeye atahitaji kuwa na designer complex zaidi, na huyo naye awe na wake complex zaidi, ad infinitum, ad nauseam ?
Umeandika vizuri "the universe suggests...".
Inabidi tuwe waangalifu sana kwenye habari za "the universe suggests...".
Unajuaje kipi ni kweli "the universe suggests..." na kipi ni bias yako ya kiutu tu?
Nitakupa mfano. Tuongelee rangi. Unaweza kusema rangi zipo, nyekundu, bluu etc. Hizi tunaziona. Ni jambo ambalo halina mjadala. The universe suggests rangi zipo, hivyo zipo.
Lakini, rangi hazipo. Rangi ni matokeo ya ubongo tu unavyofanya kazi na mwanga. Vitu havina rangi. Vitu vinatoa mwanga tu, jinsi ubongo unavyotafsiri huo mwanga ndiyo tunapata rangi. Na kuna watu wako color blind, kuna wanyama hawaoni rangi fulani.
Sasa hapo, ukitaka kwenda na uzoefu wako tu kusema "the universe suggests there is color" utapotea.
Sasa huoni argument ya "the universe suggest..." iko so prone to anthropic bias, the bias of looking at things from a human point of view, to the extent of assigning a designer God to the universe?
Pia, umesema tu contradiction haikwepeki. Ni sehemu ya maisha. Lakini hujajibu kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, aumbe ulimwengu sio tu wenye contradictions, bali mpaka unao conntradict uwepo wake yeye mwenyewe (problem of evil).
Hujajibu swali hili.
Nakuuliza kwa nini Mungu kaumba ulimwengu unao contradict uwepo wake?
Unaniambia contradiction ni sehemu ya maisha tu.
Hujajibu swali hapo. Unaonesha hujui jibu tu, kama hata swali umelielewa.