Leo naweka 'Utani' wangu pembeni kabisa na naomba wana Simba SC Wenzangu 'Mnisamehe' ila kwa huyu Michael Sarpong Kazi ipo Kwetu na Tuisila abadilike

Leo naweka 'Utani' wangu pembeni kabisa na naomba wana Simba SC Wenzangu 'Mnisamehe' ila kwa huyu Michael Sarpong Kazi ipo Kwetu na Tuisila abadilike

Yanga wako vizuri sana msimu huu, na huenda wakachukua taji la TPL.

Mugalu
Kwa nilimwanagalia mech ya kwanza Mugalu hawezi kuwa bora pale Msimbazi.
Hajiamini uwanjani, hakabi, anasubiri kutafuniwa ili afunge, ni afadhari hata Kagere ana fight.
Yanga ilifanya scauting nzuri Wakati wa usajiri.
 
Kuna muda tuache tu ubishi usio na maana yeyote tuongee tu sport...Sapong Jana hakufunga? hukuona movement zake mkuu? Hao Prisons unaowaona msimu uliopita achana na kushinda Simba hatukupata hata goli...kweli ni kipimo sahihi cha kuipima Yanga Leo kama ni mbovu?
Fanya hivi...Yanga ulioiona Jana inafanana na Yanga ya misimu mitatu iliyopita?
Na si kila mchezaji akicheza Yanga basi akija Simba atakua average...mkuu kuna watu wana Universal quality...unamtaja Ajib na Gadiel kama mifano na humtaji Morison huoni kama unakua biased?
Sometimes tujadili football tu...si kila kilichopo Jirani ni kibaya au kitaendelea kuwa kibaya milele...
Sijawahi kushuhudia shabiki wa Simba mwenye uelewa mkubwa hivi hongera sana mkuu wangu [emoji120]
 
Michael Sarpong

Leo niseme tu ukweli wangu nimewahi Kuwashuhudia Washambuliaji mahiri sana hapa nchini Tanzania kutokea Timu mbalimbali za Ligi Kuu yetu hii ila kwa Kumtizama Kwangu katika Mechi zake Mbili huku nami nikiwa 'namtathmini' kwa Jicho langu la Kiuchezaji Mpira hasa miaka yangu ya nyuma kama Beki wa Kulia, Namba Nne na Kiungo wa Chini ( Namba Sita ) leo nitayasema machache ila yenye Umuhimu juu ya huyu Mchezaji.

Huyu Mchezaji ana yafuatayo mazuri tupu....

Ni Mpambanaji muda wote awapo Uwanjani
Ni Mwenye Uroho na Goli ( Goal Poacher )
Ni mwenye Kujiamini muda wote
Ni mwenye Uwezo mkubwa sana wa Kumiliki mpira
Ni mwenye Kupiga Pasi zenye Tija kwa Timu
Ni mwenye Nguvu za Kutosha
Ni mwenye kutumia vizuri uwezo wake wa Kichwa na Miguu katika Kufunga

Pongezi zangu nyingi sana kwa Uongozi wa Watani zangu wakubwa Yanga SC kwa 'Kumsajili' huyu Mshambuliaji kwani pamoja na kwamba GENTAMYCINE ni Simba SC 'lia lia' kabisa Kwangu Mimi nadhani huyu Mchezaji kwa Kushiriki Kwetu Mashindano makubwa basi huenda ndiyo angetufaa kwa 100% kuliko huyu Mshambuliaji wetu Chris Mugalu tuliyemtoa nchini Zambia.

Na nawaonya mapema sana 'Mabeki' wa Timu zote za Ligi Kuu kuwa kama hawatamuundia 'Kamati' ya 'Roho Mbaya' ya 'Kumdhibiti' asilete 'Madhara' Kwao GENTAMYCINE natabiri mapema leo hii kuwa huenda Mshambuliaji huyu wa Yanga SC Michae Sarpong akaja Kufunga Goli / Bao hata 50 ( Hamsini ) kwa Msimu huu na Kuvunja hadi Rekodi inayoshikiliwa na aliyewahi kuwa Mshambuliaji wa Yanga SC Mohammed Hussein 'Mmachinga' na niseme tu kuwa hapa Yanga SC imelamba 'Dume' hasa.

Tuisila Kisinda

Kama kuna Mchezaji ambaye nina uhakika anaenda 'Kuwakera' na 'atawakera' mapema tu wana Yanga SC endapo tu 'hatobadilika' upesi ni huyu. Nikiri tu hapa kuwa huyu Tuisila Kisinda ni Bernard Morrison ndani ya Yanga SC na naweza Kudiriki kusema hapa kuwa amemzidi vitu kadhaa muhimu Mchezaji wangu wa Simba SC Bernard Morrison na hili wala halihitaji Mjadala.

Kitu pekee tu ambacho kinaenda 'Kummaliza' huyu Kijana wa Kikongo Tuisila Kisinda ni Makosa yake ya Kitoto ( Schoolboy Mistakes) pia ameshalewa 'Sifa' tayari, anataka Kuutafuta kwa haraka sana 'Ufalme' ndani ya Kikosi cha Yanga SC, ni Mchoyo ( Mbinafsi ) na kibaya zaidi anapenda mno Kucheza na Jukwaa na hata Nidhamu yake pia sidhani kama iko vyema ukianza tu Kuangalia jinsi ambavyo hupenda Kuvalia Jezi kwa Kuzikunja na huku Bukta yake nayo akiikunja ikiashiria kuwa huenda ama ana 'Ushamba' au amekulia katika 'Mazingira' ya 'Kiuswahili' sana huko Kwao Congo DR.

Kama si ule 'Upuuzi' wake alioufanya Jana pale Uwanjani nina uhakika ile Mechi Yanga SC ingeibuka 'Mshindi' tena kwa Goli / Bao nyingi sana kwani Tuisila Kisinda alikuwa anaingia kabisa katika eneo la Hatari la Wapinzani na kutakiwa kutoa tu Pasi ya mwisho kwa Wenzake ili wafunge Yeye hakuwa akifanya hivyo na badala yale alitaka asifiwe tu Yeye kama Yeye na siyo Yanga kama Timu.

Angalau sasa kwa Msimu huu Simba SC tutapata 'Upinzani' wa kweli kutoka kwa Yanga SC na tuwe nao 'Makini' kwani sasa nao ni Wazuri sana tu.
For the first time leo Gentamycine umeongea positive kuhusu YANGA Safi sana kiongozi wangu [emoji120]
 
Na wala sikufichi GENTAMYCINE nimeshawahi pia kuwa katika Kamati 'Maalum' ya 'Kuiroga' Yanga SC tena ile 'mliyopigwa' zile Goli / Bao 5 Taifa.
Hahahaha nimecheka sana [emoji23][emoji23]
 
Unajua hata yanga ya mwaka jana haikuwa mbaya, sema njaa ndio ilikuwa tatizo, naamini kwa tanzania, yanga ndio club yenye madeni mengi sana, sasa anapokuwa na timu ya aina hii moral ya wachezajj lazima itashuka mida baada us muda, hata hii inaonekana ina uhai fulani hivi, ila situation ya fedha ikiwa kama mwaka jana yanga wategemee vipigo tu.
 
Mikia kwa kuiba wachezaji,mkachukua Ajib,Gadiel,Morrison sasa mnawamezea mate kina sarpong jitu la miraba minne shingo ya kiboko hatari kichwa jiwe

Mchezaji wa Yanga akija Simba tunamuweka bench tu kama Man City[emoji16]
 
Kwani huyo sarponho jana hakuwepo? Hata ajib aliyokuwa yanga alikuwa mkali sana il@ huku simba amekuwa average,
Gadiel alikuwa hatari kule uto ila huku simba amekuwa average,mifano ni mingi sadney, lamine nk

Kama hujui hata ukimchukua ndemla umpeleke pale uto lazma atakuwa mfalme pale, yaani sawasawa udondoshe silva katika mkaa, pale simba sc kuna rundo la wachezaji bora.
Ubora upi kwa mpira huo mbovu wa Mikia fc.
 
Back
Top Bottom