Leo nayatoa ya moyoni

Leo nayatoa ya moyoni

Mhhhhhh......
Hili jambo lilikua zito sana kwangu na hakika nilishindwa kuliba.
Hapo niliamua kumtafuta tena X wangu na kuanza kufanya nae mazungumzo kwa kutaka kujua kulikoni hata wakafikia hatua ilie.
Yeye alinijibu kwamba anaumia kwakua ananipenda sana, hivyo ana amini kwamba bila NG nisinge mtosa kwani ningeweza msamehe.
Anyway.....
Kuna mengi sana yalitokea na kufupisha nikwamba.....
Naomba niwaweke wazi wadau wote ambao wanaijua hii maneno kuhusu kilicho jiri kwa NG kuchafuliwa na X, yote alio yafanya X sio ya kweli na hata hayo anayo yasema kwamba mimi ni mchumba wake pia sio kweli, zaidi anacho kifanya X ni kutumia kunijua kindakindaki kama ndio njia ya kuwashawishi watu kwamba mimi ni mumewe, nakumbuka kuna mdau mmoja aliniukiza hili swali na nilicho kifanya ni kumtumia cheti cha ndoa cha X nilicho tumiwa na mumewe wa pili ili kunihakikishia kwamba yule ni mkewe kwasababu hata mimi nilikua nakataa kwamba kwajinsi X alivyo mpole vile lazima atakua auasingiziwa au ni wivu wa mapenzi wa jamaa.
Pia X amekwenda mbali zaidi kwa kuingilia hata Uhuru wa kuabudu wa NG ili tu kuhakikisha kwamba anamchafua.
Mwisho nisema kwa wadau kwamba Lengo la mimi kuleta uzi huu si kuntetea NG, kwani nayeye tuliamua kuweka mahusiano pembeni kutokana na hii sinema ambayo imetengenezwa na X kwa akili kubwa.

Naomba niseme radhi iwapo kuna yeyote nitakua nimemkwaza kutokana na uzi huu, isipokua nilichokua najaribu kufanya ni kuweka mambo sawa huku nikimsisitiza X aache kumuumiza mdada wa watu na akumbuke kwamba hata yeye ana watoto wakike na haito tokea akafurahi iwapo binti yake atafanyiwa kama hivyo anavyo mfanyia mwenzie.
 
Ok....
Baada ya X kufanya yake wakati mimi sijui, ghafla nilianza kupata PM kadhaa kutoka kwa wadau humu jf wakiniuliza kulikoni.
Wakati huo pia nilipata msukosuko mkubwa na huyu mdada mpya huku akinitumia shutuma nyingi sana.
Hapo nilibaki kati na nikaamua kunyamaza na kukata mawasiliano kwa new girl na X.
Kwambaali nikaanza kushuhudia minyukano ya wawili hawa humu jf, new girl akiwa mzuri kwa hoja na X akiwa mtu wa kupopoa maneno ya hovyo.
Hapo nilijiweka pembeni zaidi ya sana huku nikiwa tazama kwambaaaali... na nikiendelea kuwapuuza kwasababu wote walikua wakishutumiana kupitia kwangu.
New girl aliamua kukata mawasiliano na mimi kabisa, huku X akizidi kupigana kufa na kupona kwamba mahusiano yake yamevunjwa na NG, hata nilipokua nikimueleza wazi kwamba simpendi tena jibulake lilikua ni kwamba kwakua nipo na NG.
Mwisho nae niliamua kupuuza.
Baada ya muda flani kupita huku nikishudia X akim quote NG humu jf kwa crushed comments... Ghafla nilipata msg kutoka kwa NG... huku akinishutumu kwa mambo mengi mabaya ambayo kwa hakika siku yafanya na sikuhusika.
Kumbe X alitengeneza picha chafu za NG kwa kushirikiana na X boy wa huyu NG. Na sijui waliweza pata mawasiliano wapi hata wakaanza kuwasiliana, kwakweli yule jamaa x boy wa NG wangu alimueleza X wangu mambo mengi sana ambayo ni past za NG.
Amahakika kweli kua uyaone.
Lengo lilikua ni kumchafua na hapo X Boy wa NG wangu pia akapata kushawishika kwamba mimi ndie nilie sababisha waka achana
Aiseee kaka pole.sio yule ze ticha kwel?? Hahaa
 
Cha msingi ascan copy ya talaka na akutumie maana hakuna namna nyingine
 
Hivi wasichana wakoje...why ufike hatua ya kumkomoa msichana mwenzako had kumuunganishia picha za X.....Kwel dunia kijiji..just kwa pm tu mtu ana nyaka hadi namba za x's wako wote!!! Mhhh kweli bado niko chini yaa technologia....hivi pale buguruni bado wanafundisha IT??
 
Pole sana ushimen. Hayo yanatendwa na wadada wengi tena ambao huwezi amini kwa staha zao. Simama upya songa mbele na maisha achana na kicheche hicho
 
Kuna mengi humu ndani, Ila Ujumbe umefika kwa wahusika na niwakati wa kufungua page mpya sasa.
 
Duh,hawa wachumba hawa ukiwa mwepesi unaweza kunywa dawa ya kahawa.Pole sana Ushimen
Mkuu wewe kubali tu Ulikuwa BUZI
Kwanza uko nje ya Bongo.
Pili kazi yako ilikuwa kwenda Westen Union.
Halafu huyo Demu alikuwa babyyyyy nyingiii Na of course zisizo isha.
Mimi nakaribia kupona Na hayo maumivu ya moyo ingawa niko hapa Dom kijijini.
Vumilia tu.
 
Mmh umbea utaniua sasa khaaa. Me nilivyomuelewa ni kwamba anataka kuweka mambo clear, especially kwa baby wake mpya. Coz ni kama figisu figisu za huyo ex zinaweka huu uhusiano wake mpya matatani + baby wake mpya kuchafuliwa humu ndani( khaa bye mpendwa, ntakuja kusutwa mama mtu mzima hivi haipendezi, utadhani Nilikuwepo sasa mmh)
Asante kwa kunielewa mkuu.
Ila bahati mbaya niliamua kukaa pembeni kwanza huku nikitafaka maisha na kuongeza bidii kwenye utafutaji wa pesa
 
Napata pata kapicha, nadhani matusi yamefika mpk blog moja machachari kwa michambo na umbea
 
Back
Top Bottom