Leo nayatoa ya moyoni

Leo nayatoa ya moyoni

Nifah hili suala lilikuwa gumu na bado ni gumu tena sana... Hiii vita inapiganwa kwa mbinu na kila aina ya SILAHA tusubiri part 2
Hivi ni nani aliyewaloga ninyi wanawake?
Mnavuana nguo hadharani sababu ya mwanaume?
Tena mbaya zaidi ni wapenzi tu,angekuwa mume ndio kila mtu angewaelewa (hasa X)

Mwanamke wewe unamtukana na kumdhalilisha mwanamke mwenzio ambaye atakusitiri siku isiyo na jina.
Hivi ukipata ajali au kudhalilika ukabaki uchi atakayevua khanga yake kukusitiri maungo yako ni nani?
Kwanini mnajitoa fahamu namna hii?
Hivi hamna watoto?Mnadhani Karma itawaacha?

Halafu ni kujidhalilisha watu wazima kwa huu upuuzi mnaoufanya wa kugombea mwanaume.
Mwanaume hagombewi,anamjua anayemtaka,na atamtafuta kwa wakati wake.

Hakuna kitu sipendi kama kumgombea mwanaume.
Hivi nini hasa tatizo?Ni kutokujiamini au?
Ukigundua mwanaume wako ana mwanamke mwingine,mwanamke mwenye kujitambua fanya haya..
1.Achana nae
2.Play part yako
Hakuna haja ya kumgombea mwanaume na kumdhalilisha mwanamke mwenzio ambaye nae alitongozwa kama wewe.
Kama kajitongozesha hiyo ni case nyingine,huyo mwanaume ndio JIPU.
Period
 
naomba tuliache hili jambo ili kufikiwa maridhiano kwa wahusika.. naona tunapoelekea tutafika kwingine kubaya zaidi. Napigania heshima ya dada angu
 
Hivi ni nani aliyewaloga ninyi wanawake?
Mnavuana nguo hadharani sababu ya mwanaume?
Tena mbaya zaidi ni wapenzi tu,angekuwa mume ndio kila mtu angewaelewa (hasa X)

Mwanamke wewe unamtukana na kumdhalilisha mwanamke mwenzio ambaye atakusitiri siku isiyo na jina.
Hivi ukipata ajali au kudhalilika ukabaki uchi atakayevua khanga yake kukusitiri maungo yako ni nani?
Kwanini mnajitoa fahamu namna hii?
Hivi hamna watoto?Mnadhani Karma itawaacha?

Halafu ni kujidhalilisha watu wazima kwa huu upuuzi mnaoufanya wa kugombea mwanaume.
Mwanaume hagombewi,anamjua anayemtaka,na atamtafuta kwa wakati wake.

Hakuna kitu sipendi kama kumgombea mwanaume.
Hivi nini hasa tatizo?Ni kutokujiamini au?
Ukigundua mwanaume wako ana mwanamke mwingine,mwanamke mwenye kujitambua fanya haya..
1.Achana nae
2.Play part yako
Hakuna haja ya kumgombea mwanaume na kumdhalilisha mwanamke mwenzio ambaye nae alitongozwa kama wewe.
Kama kajitongozesha hiyo ni case nyingine,huyo mwanaume ndio JIPU.
Period
bora uwaambie ukweli huku tunapokwenda watafikia mbali sana.. Napigania usawa katika hili... wao ni watu wazima
 
Wakuu habarini za jumapili.
Leo napenda kuzungumzia suala la mtu ku pretend na kutaka kuonekana katika jamii kwamba ni mtu fulani smart lakini anachokionyesha yeye hayuko hivo hata kidogo .
Suala hili lipo sana hapa jf na mtaani yamkini. Na huu ufake unapelekwa hadi kwenye mahusiano. Kwanini usiwe wewe halisi? Wapungukiwa nini? Ya nini kujitia mzigo kwa sababu mwisho wa siku hutoweza ku maintain hizo dramas kwa muda mrefu wenye upeo watakuumbua tu.
Kisa kamili. .....
Niliwahi kutafuta rafiki hapa jf na kwa bahati nzuri niliwapata wengi kisha nikafanya uchambuzi yakinifu nikaibuka na mchumba hapa [emoji28].
Ukaribu wangu na jf ingawa sichangii sana mada nimekuwa msomaji zaidi kutokana na ukulima wangu unaniweka busy sana lakini nimeweza kufahamiana na wadau wengi humu nje ya jukwaa lkn ni members wa jf.
Katika kuwafahamu na kuwasoma nimegundua ufake mwingi sana kwa wanajamii humu ndani. Anyway ni fantasy zao no objection.
Ila kinachonipelekea leo nilete mada ni juu ya wale ma fake kiasi cha kumshirikisha hata Mungu ku justify ubazazi wao. Hapo nawachoka kabisa yaani.
Yaani unamkuta mtu anajipambanua humu ndani kuwa ni bonge la mcha Mungu na anaandika vitu full contents unamwamini kumbe [emoji15]. ...ni chui katika ngozi ya kondoo.
Jamani badilikeni na mbebe uhalisia mnalinajisi jina la Mungu tafadhali. Bora ijulikane kuwa wewe si mlokole kuliko kujifanya mwema mbele za watu ilhali matendo yako hata shetani anakushangaa.
Hii imetokana na kisa halisi kilichonitokea. Kama nilivoanza mwanzo kuwa nilipata rafiki humu ndani ambaye tulianza mahusiano tukiwa na malengo ya kufika hatua ya ndoa. Kimsingi huyu kaka ni anajipambanua humu ndani kuwa mcha Mungu sana na maandiko yake yanajidhihirisha ivo na hata alipokuwa nami amekuwa akijionyesha mwema sana. Ajabu akawa ananambia yeye kukutana na mimi ni Kaonyeshwa na mungu ili nitende nae huduma [emoji16] [emoji16] hapo ndipo nilipoanza kumuundia tume though mwanzo nilimuamini kiaina. Akawa ni mtu mwenye kunishauri sana juu ya uchaji Mungu. Mie nikaanza kuona kweli huyu katumwa kuja kuniokoa coz kiukweli mimi nimekuwa sio msafi kiroho yaani ni mdhambi tu.
Nikaendelea nae ktk hali ya uchumba hivo but alipohitaji nimpeleke home kidogo nikawa mzito sijui sababu. Akanitambulisha kwa rafiki na baadhi ya ndugu zake. Baada ya kama 3months jamaa huyu akarudi US coz anaishi huko na huku alikuja likizo ingawa ana mpango wa kurudi bongo akimaliza masomo yake . Huku akaniachia rasilimali zake kadhaa nizimiliki nami kiroho safi nikachukua maana alizibadilisha hata majina akaweka yangu.
Alipofika Marekani akawa anafanya mchakato niende kule nimfuate nami nikataaa kwakuwa alisema anamalizia masomo atarudi bongo so hakuna haja mie niende badala yake niboreshe hapa home. Akaniambia baba yake ambae ni anafanyia kazi huko na maisha yake kiasi kikubwa amefanya huko amemshauri asiondoke upesi that's why anataka niende. Nikamwambia anipe muda nijipange.
Wakati huo mimi mbali na kumwamini nikawa namfutilia kimya kimya kuanzia kanisani anakoabudu nikawa nimepata contacts za baadhi ya waumini pale, ndugu zake wengine pia nikawa nimepata contacts zao ili niwafukunyue details kadhaa za Bwana kaka. Mimi nina tabia ya ufukunyuku sana [emoji6]
Basi kupitia hizo contacts si ndio nikagundua mkaka kaoa na anaishi na mkewe na ana watoto ingawa kuhusu watoto alishanitonya alidai mama yao alimkimbia. Kumbe mkewe wanaishi pamoja. Nilipogundua nikatafuta muda nikamweleza akakiri ni kweli lkn mke ana matatizo hataki kujirekebisha ivo ameamua kumwacha na ana process divorce. Nikaishiwa nguvu why aniongopee. Nikaanza kumshauri ili asimwache. Akawa haelewi anakomaa tu bwana kamwonyesha mimi. Nikaona huyu analeta drama kwangu. Nikapata namba ya mkewe nikampigia nikijifanya nimekosea namba basi hapo hapo urafiki ukaanza nikaanza kumdodosa uhusiano wake akawa ananieleza yuko poa na mumewe na anampenda sana. Tukaendelea kuwasiliana na mkewe sana hata akanieleza weakness kadhaa za mumewe nami nikawa namshauri sana.
Huku upande wa huyu bwana humu jf na Facebook haonyeshi kama ameoa na humu jf anajifanya anatafuta mke mwema kutoka kwa Bwana daily na anatoa ushauri humu utajua boongeeee la mlokole na mume mwema ukijaaliwa kumpata. Mwenyezi Mungu atuponye nafsi kwakeli tumekuwa wanafiki mbele za watu.
Yaani naandika natetemeka natamani kama nimtaje mumjue na wapo wengi tu humu wameharibu ndoa zao halafu wanajifanya washauri nasaha wakati wanayoongea hawayaishi.
Basi mawasiliano yangu na mkewe yakanifanya nimuonee imani mwanamke mwenzangu kwani hata zile properties alizonipa huyu kaka huku bongo ni efforts za mkewe. Nikajisikia vibaya sana jinsi huyu kaka anavyomlazimisha mkewe amuache kwa visingizio vya kijinga ili tu atimize adhma yake awe na mimi wakti mimi nimeshamjua. Nikawa natafuta namna ya kumpa ukweli. Baadae nikamweleza lakini hakujali ndio akazidisha dharau kwa mkewe. Ikabidi nimpe mkewe ukweli kuhusu mimi na uhusiano wangu na mumewe na niko tayari kutoa ushahidi amweleze tu na mimi siwezi kuwa nae kwakuwa hakunieleza ukweli na kimsingi yuko na mkewe na kwanini awe analitumia jina la Mungu kuniaminisha kuwa yeye ndie mtu sahihi kwangu maana naamini Mungu hawezi fanya double standard.
Basi nikaibua ugomvi mkubwa kwenye ile familia lkn niliahidi full support kwa mke. Mke akahama pale home kwa muda .huyu mume ndio kama karogwa akazidi kujileta kwangu. Nikamblock kwa simu akawa ananitumia pm tu humu jf simjibu niko karibu na mkewe tu.akaenda mahakamani kufungua kesi ya talaka ili amuache mkewe akisisitiza mungu wake kamwonyesha mimi ndie mkewe. Hali ikawa si shwari habari ikawafikia ndugu zao nami nikawa tayari kuwaeleza ukweli.
Talaka haikutolewa hadi sasa ingawa wawili hawa wanaishi nyumba tofauti lakini wewe jamaa naomba uniache na ukizidi kunifuatailia nakutaja humu humu jf na mengine mengi sijayasema unajua.
Halafu fanya toba ya kweli Acha kujionyesha kwa watu humu kuwa wewe unamjua sana Mungu na unawadanganya watu kuwa una mchumba utamuoa wakati huko unaishi na mkeo na hamjaachana sio vizuri unadhalilisha Ukristo aisee.
Jitafakari upya na ujitathmini.
Mkeo anakupenda sana kamuombe msamaha mlee watoto. Hakuna alie mkuu kuliko Mungu utambue. Jiulize tu mwanadamu ni nani hata ajikweze. Umeaibisha ingawa sio issue bali issue kuwa mkweli na mhalisia. Unawezaje kujiita mlokole halafu unafanya ubazazi mkeo yumo ndani eti unanipenda [emoji15] [emoji15]
Najua mihemko tu inakusukuma na ninakuombea pia utambue ulichofanya ili utubu.
Poleni wanajamii mimi si mwandishi mzuri so hata mpangilio sio mzuri ila ujumbe wangu mkuu ni kwa wale pretenders wabadilike jamani halafu tabia zenu za kudhania kwakuwa mko nje ya nchi basi tunawahusudu na viingereza vyenu muache. Sisi tupo hapa bongo na tunawapiga gap sana kimaendeleo. Kuwa nje kuwafanye mtumie fursa vizuri kukwamua familia na taifa sio kujionyesha.
Muwe na vision lol.
Jumapili njema.


Hii ina uhusiano na hii
 
Mbona sielewi au ni Mimi tuu... Nilisoma Uzi mwingine kule nimeona watu wawili wanajibishana mmoja kammchokoza mwenzie na hapa naona mengine.. Kulikoni?
 
Ukitenda kichwan unakuwa na mambo kibao huku ukiwaza maneno haya it's Time to Love Yourself,..It's better to be single mana uwezo wa kuwa na album huna Ila ukipendwa ndo utamu ulipo kuna maneno haya Love Is Sweet...Feel the power of love, You drive me crazy...upande wa pili unacheka tuuu...Mwisho wa siku Kuachwa au Kuacha si dhambi ila dhambi kumsema vibaya mbaya wako huku ukiwapa faida hadhira..
 
Ukitenda kichwan unakuwa na mambo kibao huku ukiwaza maneno haya it's Time to Love Yourself,..It's better to be single mana uwezo wa kuwa na album huna Ila ukipendwa ndo utamu ulipo kuna maneno haya Love Is Sweet...Feel the power of love, You drive me crazy...upande wa pili unacheka tuuu...Mwisho wa siku Kuachwa au Kuacha si dhambi ila dhambi kumsema vibaya mbaya wako huku ukiwapa faida hadhira..
naona umeweka hadharani kila kitu.. Andishi la kiuchokozi hili
 
Mkuu ongea nao waambie kugombea liborooo fc tena kwenye mitandao ni aibu....umri wao na matendo yao hayaendani kabisa istoshe jamaa amewashinda kwa KO kma mayweather
kuu mmoja ameshanitii na yupo kimya anatafuta pesa tu na namuomba aendelee kuwa kimya kuepusha maneno.. Popote ulipo dada angu tambua ahadi yangu kwako
ni kukupenda
 
Back
Top Bottom