Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 34,020
- 79,098
Hivi ni nani aliyewaloga ninyi wanawake?Nifah hili suala lilikuwa gumu na bado ni gumu tena sana... Hiii vita inapiganwa kwa mbinu na kila aina ya SILAHA tusubiri part 2
Mnavuana nguo hadharani sababu ya mwanaume?
Tena mbaya zaidi ni wapenzi tu,angekuwa mume ndio kila mtu angewaelewa (hasa X)
Mwanamke wewe unamtukana na kumdhalilisha mwanamke mwenzio ambaye atakusitiri siku isiyo na jina.
Hivi ukipata ajali au kudhalilika ukabaki uchi atakayevua khanga yake kukusitiri maungo yako ni nani?
Kwanini mnajitoa fahamu namna hii?
Hivi hamna watoto?Mnadhani Karma itawaacha?
Halafu ni kujidhalilisha watu wazima kwa huu upuuzi mnaoufanya wa kugombea mwanaume.
Mwanaume hagombewi,anamjua anayemtaka,na atamtafuta kwa wakati wake.
Hakuna kitu sipendi kama kumgombea mwanaume.
Hivi nini hasa tatizo?Ni kutokujiamini au?
Ukigundua mwanaume wako ana mwanamke mwingine,mwanamke mwenye kujitambua fanya haya..
1.Achana nae
2.Play part yako
Hakuna haja ya kumgombea mwanaume na kumdhalilisha mwanamke mwenzio ambaye nae alitongozwa kama wewe.
Kama kajitongozesha hiyo ni case nyingine,huyo mwanaume ndio JIPU.
Period