Leo ndio nimejua kwanini TANESCO wamegoma kushusha bei ya umeme hata baada ya Bwawa kuanza kazi mwakani

Leo ndio nimejua kwanini TANESCO wamegoma kushusha bei ya umeme hata baada ya Bwawa kuanza kazi mwakani

Ujinga ni mzigo kwa hiyo kampuni za kitanzania kwenda kuuza umeme ili kutuletea kipato nayo ni nongwa?

Yaani tayari ni ajenda ya kisiasa sisi masikini kama tunaweza kupata vya kuuza ili tujiingizie kipato ni jambo zuri sio tu kuuza mahindi na maharage.

Kama tunauza na umeme jambo zuri sana hata awe mtoto wa nani binafsi nasupport kampuni za kitanzania kufanya hivyo.

Sio kila siku zinakuwa tu kampuni za kigeni kufanya hivyo napongeza sana kampuni ya tanzania inayofanya hivyo.
We we ndiyo jinga kabisa.unakimbilia kuuza nje wakati ndani kwako bei ya umeme ni juu na baadhi ya wananchi hawajaungwa
 
Acha ujinga wewe!

Kwa hiyo hakuna mitambo inayozalisha umeme pale kwenye bwawa?

Ile mitambo iliyokuwa inasafirishwa kupelekwa rufiji kufungwa kwenye bwawa ilikuwa inaenda kufingwa kama Toy eeeh??

Ile mitambo inapozalisha umeme haihitaji service kusema ikifungwa ndo imefungwa wala haiharibiki wala kuhutaji kubadilishwa vipuri?

Kama hamjui mambo kaeni kimya sio mnajionesha mlivyo wajinga humu
Wewe jamaa unakichwa kizito sana hivi megawatt 2100 ukiziachia zikafanye kazi sizitazalisha pesa nyingi sana zakuweza kufanyia hizo maintenance na kulipa deni kama ukiziuza Ili ulipe deni unakua unafanya Nini Sasa si Bora usinge kopa tu.
 
Wewe jamaa unakichwa kizito sana hivi megawatt 2100 ukiziachia zikafanye kazi sizitazalisha pesa nyingi sana zakuweza kufanyia hizo maintenance na kulipa deni kama ukiziuza Ili ulipe deni unakua unafanya Nini Sasa si Bora usinge kopa tu.
Pesa nyingi zinazozalishwa zinapaswa kuuchangia mradi ili uendelee na usije kufa mwishoni.
 
Kabisa, lengo la mradixlilikuwa kushusha bei ya umeme na kichagiza ukuaji wa viwanda ili vijana wapate ajira na kukuza uchumi. Leo hii hata kutumia heater kuchemshia maji ni anasa, umeme watu wanawashia taa tu, tena ya nje inawashwa moja tu.., vieanda viko hoi, umeme bei juu!! Sasa zinaingiaje Megawatt 2,100 mpya kabisa na bei isishuke?! How!???
Walisemaga ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni !! Huu utakuwa uonevu uliopitiliza kama itakuwa hivyo alivyosema Maharage !
 
Hisia ni kitu kibaya sana.

Umeandika mambo ya nadharia yasio na chembe ya ukweli. Hicho cha bei kutoshuka kinawezekana, ila umeme uuzwe halafu ela apokee mtu mwingine hilo sahau.
Inawezakana kupokea mtu mwingine. CCM haishindwi jambo
Inaonekana ulikuwa nje ya nchi na umerudi
 
Sasa unabishia Nini?
Nikuulize wewe? Unaetaka umeme uwe rahisi tu bila kuzingatia kuna gharama za uzalishaji pamoja na matengenezo ya mradi/ vifaa ambayo hayo yanaangalia thamani ya hela na hali ya uchumi sio unafuu wa mradi
 
Sema kama JamiiForums ndo wanaojiita great thinkers wana mawazo kama haya 🤔
Wanafikiri hivi, na kutoa point zao kwa style hii,
Wanajua kuzusha majungu hivi,

Bas ni halali bandari apewe mwarabu tu
 
We we ndiyo jinga kabisa.unakimbilia kuuza nje wakati ndani kwako bei ya umeme ni juu na baadhi ya wananchi hawajaungwa

Ko mkuu mimi sahizi nikipata deal la kuwekeza kenya umeme nianze kuuliza nawekezaje kenya wakati Nanjilinji hakuna umeme?
Kwani mimi serikali ?
Huyo dogo ni mtu binafsi, aweke mpunga wake asipangiwe pa kuwekeza akitaka kuwauzia hata Malawi na sawa tu, sisi tubanane na Tanesco kwanini Nanjilinji hakuna umeme
 
Ukisema uikosoe serikali wewe ndio unaonekana mbaya, kwa sababu ksingizio kikubwa kilichokuwa kinafanya wawekezaji wasije kuanzisha viwanda Tanzania ni kutokana na uhaba wa nishati. Sasa kama umeme unaajitosheleza kwa nini wasivutie hao wawekezaji waje kuanzisha viwanda hususani manufacturing na assembly plants hapa Tanzania? Au ndio kusema viongozi wetu wanafikiria maslahi yao binafsi? Maana hata sisi wawekezaji wazawa huwa tunaletewa urasimu mwingi tukitaka kuwekeza kutokana na uelewa finyu wa watendaji.
 
Hivi mbona unajisumbua kubishana na majitu mapumbafu Ina maana kwa umri alionao hajui hata Kodi inakusanywa vipi yaani Kuna wananchi wengine ni hasara
Yaani nimecheki comment zake zilizofuata ndio nikaona huyu yupo hapa kuvuruga majadiliano, nimemuweka kwenye ignore..., hata sioni tena comment zake
 
Tangu Maharage pale TANESCO alipotoa tamko lisilo na mantiki na linalo-defy all logical reasoning, kwamba eti hata baada ya Megawatt 2100 kuanza kuzalishwa kwenye bwawa la Nyerere na kuingizwa kwenye Gridi bado eti umeme hautashuka bei, nimekuwa nikiwaza sana nisielewe hii itawezekana vipi?!

Ni kwamba Law ya demand vs Supply inagoma kabisa!! Kwamba matumizi yetu hivi sasa ni Megawatt 1,600, na ndizo zinazalishwa kwa sasa, halafu ghafla uingize Megawatt 3,700 kwenye gridi, huo umeme wote atautumia nani kwa ghafla hivyo hadi uishe?

Tulitegemea kwa kuwa umeme hauwezi kutunzwa kwenye betri, kwamba Tanesco washishe bei ili hadi vijijini wapikie majiko ya umeme, kiasi umeme huo sasa utumike wote bila kupotea, vinginevyo itabidi tufungulie maji bwawani yamwagike bire bila kuzalisha umeme.

Sasa leo ndio nimejua mchezo wanaotaka kufanya, ni mwamba hizo Megawatt 2,100 za Bwawa la Nyerere tutazisikia kwenye bomba tu, maana zitaingizwa kwenye gridi ya taifa na kuwa offloaded kwenda Zambia, Malawi, Uganda, Kenya ,Zanzibar, Burundi, Rwanda, Msumbiji, na hata sentano mbuni hatutaiona ya mauzo ya umeme. How? Kwanini nasema hivi?

1.) Umeme huo hautaonekana kwamba umetoka Tanesco, bali kuna dogo mmoja inadaiwa ni mtoto wa mama yetu, yeye kaongozana eti na maafisa wa Wizara ya Nishati ili azalishe umeme wa Solar na kuiuzia Uganda , 😂😂😂, kwamba umeme utoke Rufiji, mseme ni umeme jua wa huyo dogo? Halafu malipo yote alipwe yeye?!! 😂😂😂 , ujamja wa kizani sana huu...

2.) Inadaiwa January Makamba anakazana sana kuunganisha gridi ya Tanzania na Gridi za Rwanda kupitia Rusumo, na anafanya mikutano na nchi nyingi zinazotuzunguza hasa malawi, Zambia na wengine eti tuunganishe gridi yetu kwa pamoja ili tuuziane umeme panapokuwa na upungufu. Shida hapa ni kwamba umeme utatoka Rufiji halafu watasema ni umeme wa gesi, hivyo malipo yataenda kwa wenye gesi yao.., sisi tutabaki kulipa mkopo wa Trillion 10 zilizotumika kujenga hiko bwawa, kwa tozo za miamala na kodi za majengo za kwenye umeme zilizopoandishwa.

Hivi mtu mwenye akili timamu unakubali vipi kuambiwa kwamba Megawatt 2,100 ziingizwe kwenye gridi na bado zote zitumike ziishe bila kushusha bei?!!!

We are finished!! Tumekwisha...

View attachment 2715874

I can’t imagine huyo mama abaki hapo hadi 2030, kweli?!! Tanganyika Tutakuwa na hali gani sisi, si tutakuwa tunatembea tunaongea wenyewe kama wehu?!

=========================
Haya Wai pengo akakupe posho yako
 
Atokeee
Mh. Samia simkubali hata kidogo jinsi anavyo endesha nchi lakini kuhusu biashara halali ya kijana anayedaiwa kuwa mtoto wake sioni tatizo lolote.
Kwani mtoto wa raisi siyo binadamu kama wengine? Hana uwezo, akili na haki ya kufanya biashara halali?

Hapa umeleta tuhuma nzito zilizo egemea kwenye hisia zaidi kuliko uhalisia na ukweli.
Acha kuchafua watu.

#MkatabaWaBandari-ni-uhuni-tupu_KataaDPWorld.
E
 
Ukisema uikosoe serikali wewe ndio unaonekana mbaya, kwa sababu ksingizio kikubwa kilichokuwa kinafanya wawekezaji wasije kuanzisha viwanda Tanzania ni kutokana na uhaba wa nishati. Sasa kama umeme unaajitosheleza kwa nini wasivutie hao wawekezaji waje kuanzisha viwanda hususani manufacturing na assembly plants hapa Tanzania? Au ndio kusema viongozi wetu wanafikiria maslahi yao binafsi? Maana hata sisi wawekezaji wazawa huwa tunaletewa urasimu mwingi tukitaka kuwekeza kutokana na uelewa finyu wa watendaji.
Na ndio lengo la mradi hilo, bei ya umeme ishuke ili wawekezaji wakimbile fursa ya nishati ya bei nafuu kuamzisha vinwanda. Sasa kama bei haishuki, huu mradi una faida gani?
 
Back
Top Bottom