Ndio mimi nimeomba ushauri, sote kwa pamoja tuwaze namna nzuri ya kucross check kama waomba misaada wanahitaji kweli msaada, either kupitia kwa wenye jamii forums au any verified figures wa humu (kama walivyo akina Malisa kule insta) kusudi wenye kuomba msaada basi wapate msaada, na watoa msaada watoe kwa kujua pesa yao inagusa hitaji la mtu.
Naelewa kuwa hata mtu awe na pesa nyingi kiasi gani hatapenda kumpa mtu muongo/tapeli. Binafsi kuna kakijana humu kalisema kama mke amejifungua na kazi imesimama, hawana hata hela ya chakula, nikafikiria njaa inavyouma wakati wa kunyonyesha ngoja nichangie mwanamke mwenzangu apone, looh! Hako kakijana kalikuja kuumbuliwa humu kuwa kana uraibu wa kubeti, hakana mke wala mtoto wa mchanga! What a waste..
Naelewa changamoto za utapeli, lakini humo humo kuna wenye shida kweli, hatuwezi kumaliza matatizo ya watu ila tunaweza kuelevate situations hata kwa masaa kadhaa.
Sijasema huyu achangiwe, namaanisha JF kama Community tunaweza kupata namna nzuri ya wenye uhitaji kusaidiwa.