Man Utd walidhaminiwa na Sharp (Tv) halafu baadae Vodafone ilikuwa hatari sana huku Liverpool wakidhaminiwa na Calsberg (bia) wakiwa wadhamini wa muda mrefu sana wa Liver.
Hiyo jezi yenye nembo ya Calsberg nawakumbuka Spice Boys akina Michael Owen ( The Golden Boy ), Robbie Fowler ( God ) mashabiki wa Liverpool walimuita jina la utani Mungu. Alikuwa na kipaji kikubwa sana cha kufunga.
Halafu kuna mtu wa kuitwa Stan Collymore... we acha utani kabisaa bila kumsahau Mc Manaman. Hapo nazungumzia miaka ile ya 97 mpk 2000!
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 wakaja watu kama akina Aboubacar Titi Camara, huyo alikuwa Mguinea, mtukutu El Hadji Diouf, Salif Diao japo hakutamba sana, pia alikuwepo mwamba wa Finland, Sammy Happya! Bila kumsahau Mkongwe Danny Murphy.
Cc
Guasa Amboni