Leo ndio tutajua baba mwenye gari ana umuhimu gani..!

Hivi mwenye mshahara wa laki tatu na anapanga nyumba vyumba viwili na ana watoto wanasoma anaweza kumudu gari? Nisaidie mchanganuo ili kesho nilitafute mvua zikikatika.
Mjini mipango....sio gari tu hata nyumba anajenga wakati mwenye mshahara 2m analia haumtoshi.
 
Hii mvua imeleta balaa, usafiri hamna watu wamezagaa barabarani na miamvuli kwa kweli hata kutoa lift ni ngumu maana utamchukua yupi utamuacha yupi?

Leo ndio baba mwenye gari anatembea kifua mbele
Bwahahahah!
😀😀😀😀😀
 
Umeongea cha maana sana.
 
Tujue na kutofautisha kati ya gari na usafiri. Siyo kila mwenye gari ana usafiri and vice versa
 
Baba mwenye gari au baba mwenye gari wote wanaelekea kwa baba mwenye vyote ila hapa katikati ya safari ndio kuna hizi changamoto
Muhimu ni kuwa baba mwenye gari na baba mwenye nyumba, hii mvua unapaki gari ccm unatembea hadi home ni heri tu kuwa both.
 
Mjini mipango....sio gari tu hata nyumba anajenga wakati mwenye mshahara 2m analia haumtoshi.
Huo ni wizi siyo mipango. Huwezi kuwa credible na mshahara huu ukamiliki gari au ukajenga. Hongera mwenzetu.
 
Huo ni wizi siyo mipango. Huwezi kuwa credible na mshahara huu ukamiliki gari au ukajenga. Hongera mwenzetu.
Sio wizi ni mipango tu..mshahara haujawahi kumtosha mtu. This aint about me.
 
Kodi haiji ghafla....
Haiji ghafla lakini ikija stress haziishi nakuambia, 250-500kpm kwa mwaka mzima kama tu kuna sehemu ulikosea kudunduliza, utaomba poo, tena ukutane na landlord mkali.

Kipindi hiki bajaj zinaokoa "baba wenye nyumba".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…