Amani kwenu wanajamvi, natumai mu wazima na mnasonga vyema kwa uwezo wake Labana. Ni asubuhi tulivu siku ya jumamosi ya tarehe 06/07/2013 watu tumenyuka vyuti (ndio uwingi wa suti) vyetu na tai tukiwa na nyuso za furaha huku wale wenye chuki wakigumia kwa vilio vya kwikwi na macho ya kutokuamini kinachotokea..... Naam ni siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu ambapo kijana
Arushaone na binti
Lady doctor watapanda altareni na kwa kauli moja watasema REST IN PEACE UKAPERA......
Nikiwa kama mwenyekiti wa mahusiano na ndoa ningependa kutoa wito (kama sio ONYO) kwa wale wote waliokuwa wanajiita sijui wake, mara wachumba,mara hawara wa
Arushaone wakiongozwa na vibibi
Madame B na
Mamndenyi washike adabu zao japo kwa siku ya leo ambapo MKE HALALI anachukua nafasi yake katika Himaya ya
Arushaone... , Na vile vidume vilivyokuwa kwenye foleni ya kukaguliwa na
Lady doctor wakae kando kwanza wakati mkaguzi mwingine
Evelyn Salt anamalizia mazoezi ya ukaguzi kule gym ya jukwaa la chini....
Peoples...!!! baba kapata mama na mama kapata baba..... tuwaombee wanandoa hawa kila la heri....
Wapi
ladyfurahia atuanzishie pambio, ODM babu
Asprin na kati ya maternity ward tunakutegemea kwa ajili ya picha mjongeo na picha mnato.... Nasaha zitatolewa na nyani mzee aliyekwepa mishale mingi babu DC
Dark City.... sina uhakika kama
Mtambuzi amesharudi toka kwa wagogo(duru zinaripoti kuwa amepata kajikuku ka kienyeji) naamini
watu8 atasimamia vyema masuala ya protokali....
copy:
Bishanga Slave,
Erickb52, -@measkron,
King'asti,
snowhite (wewe nakudai ujue)
Mentor marejesho ,
Filipo ,
Mamzalendo , .................!!!!!!!!!!!!!
Tupo pamoja....