Leo ndo Leo...., Arushaone na Lady doctor mbele ya baba paroko... Ndoa hiyooo...!!!!!

Leo ndo Leo...., Arushaone na Lady doctor mbele ya baba paroko... Ndoa hiyooo...!!!!!

Last edited by a moderator:
Protokali...
Intelijensia imeleta taarifa kuwa huko ulipo si salama kuleta helikopta...hivyo bi mkubwa tafuta bajaj ikulete ukumbini

thijawahi! Ila naona ulivyoshadadia, umepewa kamati gani vileee?
 
Protokali...
Intelijensia imeleta taarifa kuwa huko ulipo si salama kuleta helikopta...hivyo bi mkubwa tafuta bajaj ikulete ukumbini

Nakuaminia mkuu wa protokali, hakikisha ulinzi wa bwana harusi... Madame B hachelewi kumteka...
 
Last edited by a moderator:
Ngoja nimhimize dobi wangu awahi kumalizia suti yangu, hizi pasi za mkaa noma sana. Ibada saa ngapi?
 
Last edited by a moderator:
1. Naanza na pambio hii kwanza:
Jamani leo ni shangwe jamani leo
vifijo na nderemo na kizaizai vimetanda
kotekote si MMU, CC, SIASA, JOKES wala
jamii intellegence kwani wale walio nuna,
sasa wanacheka kwa shingo upande na
huku wakikodoa mimacho utadhani ,
wamebanwa na mlango kama mjusi,
hawaamini yale wayaonayo mbele ya kioo
cha jamii cc. angalia my cousin huyo ni mliberia,
asijekuumiza home ukakimbilia na usijue lakufanya,
huyo kashashindikana km alivyoshindikana Mentor,
onyo ninakupa nduguyo usijesema sikusema mie.


2. Na wengine twafurahi kuona wawili wakipatana,
wakila kiapo cha ndoa yao dumu daima
maneno wakiyatoa utadhani hawatagombana,
wakinena kwa uzuri kusema wamependana,
wamesahau ya kwamba watakuja kulana,
hawajui yakuwa kwenye ndoa ni conflits tu
kumbe kwenye ndoa kuna ups and downs,
Ni vyema wajipange upya na kuona wako sweets,
Acha sie tufurahi na kurukakuruka kama ndege x2

sasa kiongozi nimeshaimba wimbo ulisema nianzishe kuimba ila sijawaona waitikiaji inakuwaje tena na songi hilo hapo juu halafu kiongozi Baba V mbona hujaniambia niandae cheti cha ndoa? hiki hapa nenda kawapadirishe hao wanandoa sasa mcert.jpg

Amani kwenu wanajamvi, natumai mu wazima na mnasonga vyema kwa uwezo wake Labana. Ni asubuhi tulivu siku ya jumamosi ya tarehe 06/07/2013 watu tumenyuka vyuti (ndio uwingi wa suti) vyetu na tai tukiwa na nyuso za furaha huku wale wenye chuki wakigumia kwa vilio vya kwikwi na macho ya kutokuamini kinachotokea..... Naam ni siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu ambapo kijana Arushaone na binti Lady doctor watapanda altareni na kwa kauli moja watasema REST IN PEACE UKAPERA......
Nikiwa kama mwenyekiti wa mahusiano na ndoa ningependa kutoa wito (kama sio ONYO) kwa wale wote waliokuwa wanajiita sijui wake, mara wachumba,mara hawara wa Arushaone wakiongozwa na vibibi Madame B na Mamndenyi washike adabu zao japo kwa siku ya leo ambapo MKE HALALI anachukua nafasi yake katika Himaya ya Arushaone... , Na vile vidume vilivyokuwa kwenye foleni ya kukaguliwa na Lady doctor wakae kando kwanza wakati mkaguzi mwingine Evelyn Salt anamalizia mazoezi ya ukaguzi kule gym ya jukwaa la chini....

Peoples...!!! baba kapata mama na mama kapata baba..... tuwaombee wanandoa hawa kila la heri....
Wapi ladyfurahia atuanzishie pambio, ODM babu Asprin na kati ya maternity ward tunakutegemea kwa ajili ya picha mjongeo na picha mnato.... Nasaha zitatolewa na nyani mzee aliyekwepa mishale mingi babu DC Dark City.... sina uhakika kama Mtambuzi amesharudi toka kwa wagogo(duru zinaripoti kuwa amepata kajikuku ka kienyeji) naamini watu8 atasimamia vyema masuala ya protokali....
copy: Bishanga Slave, Erickb52, -@measkron, King'asti, snowhite (wewe nakudai ujue) Mentor marejesho , Filipo , Mamzalendo , .................!!!!!!!!!!!!!

Tupo pamoja....
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom