#COVID19 Leo ndo nimeamini COVID-19 ni hatari

Sisemi kuwa tatizo letu halitibiki. Utamaduni ni mafundisho, wakati wowote kwa kupenda ama kutopenda tunaweza kubadilika. Moja ya kazi za serikali ni kutoa elimu sahihi ili jamii iondokane na tabia zinazodumaza maendeleo.
Hatuelewani mkuu, tatizo si utamaduni tofauti yetu sisi ni kutojengewa hofu kwa kutishwa na huu ugonjwa kama ambavyo hao wengine walivyofanyiwa,kwahiyo issue hapa ni kutishwa tu na ndio maana hata huko kwengine wapo waliyogundua hilo na wanasema corona inakuzwa sana.
 
Ni corona?
 
Kenge huwa anaelewa baada yakupigwa na kitu kizito kichwani na mpaka atoe damu masikioni wakati huo keshafariki, watanzania wengi tupo kama huyo jamaa.
 
Corona ipo. Best yangu ameteseka sana hii wiki na iliyopita tunamshukuru Mungu sasa anaendelea vizuri. Maumivu yake anasimulia si mchezo mwili kama umevunjwa vunjwa halafu unachomwa na misumari. Kifua ndio usiseme.
Watu wengine dalili inakuja kny kutapika tu
 
Nyie kila siku mnasema mmefiwa na anko zenu, mbona nyie hamfi?

Au inakuwaje jamani?
 

Nshapigwa na hii kitu
Wanaosema haipo nawaombea kwa nguvu iwalambe wajifunze kuwa na utu
 
Alikuwa hospitali au
Alikuwa anatumia dawa gani
 
Nshapigwa na hii kitu
Wanaosema haipo nawaombea kwa nguvu iwalambe wajifunze kuwa na utu
Kama haijakupiga au kumpiga mtu wako wa karibu utaona watu wakiongea ni blablah tu.
Pole sana kwa kupitia hii changamoto
 
Tulienda msiban huko mwanza-ukerewe na barakoa zetu na sanitizer za kutosha Ila tulipofika Tu msiban walitunyanyapaa na barakoa zetu mpaka tulivua...Kwa maeneo ya vijijini ni vigumu Sana kuwaelimisha juu covid-19
[emoji23][emoji23] Ni kweli..ukivaa barakoa unaonekana mjuaji flani
 
Mimi nipo nchi moja hivi kimasomo asikuambie mtu nimeona watu wa karibu sana wakidondoka. Maprofesa wangu watatu wamepukutika mmoja wawili waliopona wamekaa ICU siku 40 wametoka ukiwaangalia machozi yanatoka maana wakitembea wanapepesuka tu mpaka unasema ni bora wangefariki. COVID 19 haina formula unaweza kuwa kijana na confidence yako ila ukipata hata usiku huvuki na pia unaweza ukawa nayo ukadunda bila kujijua. Muhimu kama wewe huogopi jali wazazi wako na watu wengine ambao ni dhaifu. Naangalia watanzania tulivyo na dharau na maneno ya kashfa mitandaoni ila kumbukeni tu machozi humtoka mwenye msiba.
 
Mkuu maisha siku zote yapo hivyo labda uwe hukuwahi kushuhudia watu wako wa karibu wakiuguwa au wewe mwenyewe kuuguza, sie wengine tumeshawahi kuuguza na kufiwa na watu wa karibu ndani ya wiki moja tu hiyo kabla ya corona, kwahiyo hisia hizo mnazozisema humu watu tunazijua ila wengine kwa sababu zimewakuta hisia hizo kipindi hiki cha corona ndio maana mnaona ni vitu vya ajabu havijawahi kuwepo.
 

Mkuu inaonyesha bado ugonjwa wa corona hauujui vizuri ,sasa hali ya hewa/mazingira/immunity ya watu wa moshi ni sawa nchi nzima? Kama watu hawajasambaza kwenye mikoa mingine si itaishia huko huko Moshi?
 
Mkuu inaonyesha bado ugonjwa wa corona hauujui vizuri ,sasa hali ya hewa/mazingira/immunity ya watu wa moshi ni sawa nchi nzima? Kama watu hawajasambaza kwenye mikoa mingine si itaishia huko huko Moshi?
Kwahiyo hapo unataka nikuelewe vp maana mara Moshi watu wanapukutika mara wanaokufa ni asilimia tano tu mara hali ya hewa na mazingira ya moshi, hebu niambie nikuelewe vp kuhusu hiyo corona huko moshi?
 
Kwahiyo hapo unataka nikuelewe vp maana mara Moshi watu wanapukutika mara wanaokufa ni asilimia tano tu mara hali ya hewa na mazingira ya moshi, hebu niambie nikuelewe vp kuhusu hiyo corona huko moshi?

Wataalam kila siku wanatoa maelezo kuhusu huo ugonjwa mkuu ,google it utapata factors zinazo favor corona virus ku spread ,wameeleza kwa kina immunity,environment(weather condition) etc impact zake kwenye uviko.
 
Kwa hiyo unaamini kila ukibanwa na kifua ni C-19.Dah!Kweli ujinga hauna mwisho.Hivi hujui kwamba vitu vingi vinaweza kuleta kubanwa na kifua,hata air pollution!Na hivi hujui kwamba hicho kinachoitwa Corona ukinywa Hydroxychloroquine au Ivermectin au hata Pine Oil au hata Pine Juice kinapotea?Tumeingizwa mkenge kweli kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…