#COVID19 Leo ndo nimeamini COVID-19 ni hatari

#COVID19 Leo ndo nimeamini COVID-19 ni hatari

Dada yangu na wewe umekubali kuwa corona ni hatariii ?
Usidanganyike na corona ya kutunga.watu wanakufa kwa magonjwa mengine sio corona. Mtaani mbona hakuna hizo habari? Yaani imefika wanatangaza eti corona sijuhi mjikinge kwa nini wanatumia nguvu kubwa? Virona ni ugonjwa wa kutengeneza unakuja kama nvua na kuondoka.
 
Si hofu ya malezi bali kutishwa ndiyo maana wengine wanasema corona inakuzwa.
.

Hofu imejengwa ulimwengu mzima lakini mwitikio, kwa kulinganisha, unatofautiana kati ya jamii na jamii. Aidha, sisi si kwa korona pekee, kutochukua tahadhari kwa mambo kama magonjwa ama hatari zozote ni utamaduni. Sababu zingine zinaweza kuwepo lakini utamaduni huchukua nafasi kubwa. Hata leo hii, mtu ana uwezo, atajenga nyumba, hamna tahadhari zozote za kujihami na hatari kama za moto. Hata bima hamna.

Ninakumbuka baada ya visa vya moto kama Shauritanga kutokea ndiyo baadhi ya mashule yakahimizwa kufundisha watoto kujihadhari. Kisha kimyaaaa. Sasa hivi unaona mabalaa ya moto tena, kwakuwa hajafa mtu, hamna kinachofanyika. Kesho watu wakigeuka mishikaki utaona tunavyoanza kulipuka na kujipanga upya.
 
Hata hapa Tanzania sasa hivi serikali ikitaka kuwatisha wananchi wake inaweza na ilishakuwa hivyo ile mwaka jana mwanzoni watu waliitikia huo muito wa hofu.
 
Jamaa yangu alienda Moshi last week , alivyofika huko maeneo ya kwao akaona daily watu wanakufa ikabidi arudi DAR fasta.
 
Jamaa yangu alienda Moshi last week , alivyofika huko maeneo ya kwao akaona daily watu wanakufa ikabidi arudi DAR fasta.
Kwa hii hali yetu ya kutochukua tahadhari ambayo tuko nayo mwaka jana, unadhani itachukua muda gani hadi hivyo au maambukizi kama hayo ya Moshi kuweza kuwepo nchi nzima?
 
Hata hapa Tanzania sasa hivi serikali ikitaka kuwatisha wananchi wake inaweza na ilishakuwa hivyo ile mwaka jana mwanzoni watu waliitikia huo muito wa hofu.
Sisemi kuwa tatizo letu halitibiki. Utamaduni ni mafundisho, wakati wowote kwa kupenda ama kutopenda tunaweza kubadilika. Moja ya kazi za serikali ni kutoa elimu sahihi ili jamii iondokane na tabia zinazodumaza maendeleo.
 
Kwa hii hali yetu ya kutochukua tahadhari ambayo tuko nayo mwaka jana, unadhani itachukua muda gani hadi hivyo au maambukizi kama hayo ya Moshi kuweza kuwepo nchi nzima?

Mkuu unachoshindwa kuelewa ni kwamba kati ya watu 100 watakaopata corona , 85 wanaweza wakapona bila kuonyesha dalili , 10 wanaweza kuonyesha dalili , 5 wanaweza kufariki na hao huwa na magonjwa mengine).

Kwahiyo corona ni risk sana kwa watu wenye magonjwa mengine eg kisukari ,magonjwa ya moyo ,sicklecell ,Pumu etc

Darwin Theory inasema :- Survival of the fittest means Only the strong will survive.
 
Nilikuwa nachukulia poa hii kitu. Yaani kuvaa barakoa na kunawa sijui mikono ilikuwa ni mpaka nione kuna ulazima au kulazimishwa.

Mfano nikienda hospital ni mpaka nione watu hawaruhusiwi kuingia bila barakoa ndo na mimi nitanunua na kuvaa. Ila sasa yaliyotokea leo ndugu zangu nimenyoosha mikono juu. Yaani nimepigiwa simu jana saa nne usiku naambiwa mama yako mkubwa anaumwa kifua kimembana na vichomi tunampeleka hospitali, nikachukulia kawaida tu. Kufika saa saba na nusu usiku watu wanapiga simu wanalia amefariki.

Nimefika msibani tena naambiwa watoto wake wawili wamelazwa hospitali wapo hoi kwa tatizo hilo hilo la vifua kubana na vichomi. Aise ikabidi nitoke kimya kimya kwanza kwenda kununua barakoa za kutosha na groves kabisa maana ni hatari.

Covid ipo ndugu zangu ni hatari na inaua ghafla ghafla kabla hata hujatubu dhambi zako.

Take care chukua tahadhari.

Tangu Samia awalegezee kidogo mmeshapata mwanya.

Lengo lenu halitafanikiwa.
 
My condolence ..

Miafrika ni mijinga mno ndio maana ilitia aibu dunia nzima kwenye Ukimwi , ugonjwa ambao unadhibitika na kuafuta masharti rahisi mno.
mijitu ilikuwa haisikii ikiambiwa ipo kwenye uzinzi, Tanzania ilifikia kuwa nchi ya tano duniani kwa maambukizi ya ukimwi.

Na sasa lile pumbavu poripori tulilipa nchi ndio liliwajaza matope vichwani na kuirudisha nchi nyuma sana na ushabiki wa kijingajinga....
 
Mi wiki iliyopita ndo nimeamini kaugonjwa kapo bhana, kwenye familia kulikuwa na wagonjwa 5 na wote wakaugua kwa pamoja, 3 wako nyumba moja, mmojawapo ni mzee zaidi ya 85 na ndie nilishika usukani kumuuguza jinsi alivyokuwa akihangaika hadi huruma Yani, nashukuru Mungu mpk Sasa wametoboa ila siku ile za hatari hali haikuwa nzuri niliharisha Kila dakika niliiona yenye thamani, uhai mtamu jamani
 
Nami leo ndiyo naamini nimesikia Sana Kwa watu.
Nasikitika nimempoteza uncle wangu asubuhi ya leo mbaya zaidi nilikuwa naye kwenye mazishi ya uncle wangu mwingine siku Sita nyuma yeye karudi mkoani hajachukua round.
Kwa kifupi nimefiwa na uncle zangu wawili ndani ya wiki mbili acheni tu...
 
Mkuu unachoshindwa kuelewa ni kwamba kati ya watu 100 watakaopata corona , 85 wanaweza wakapona bila kuonyesha dalili , 10 wanaweza kuonyesha dalili , 5 wanaweza kufariki na hao huwa na magonjwa mengine).

Kwahiyo corona ni risk sana kwa watu wenye magonjwa mengine eg kisukari ,magonjwa ya moyo ,sicklecell ,Pumu etc

Darwin Theory inasema :- Survival of the fittest means Only the strong will survive.
Mkuu Moshi watu wanakufa sana kama ulivyoelezea maana yake huko maambukizi ni mengi ndio kuna ongezeko la vifo, ndio maana nikauliza itachukua muda gani hadi maambukizi yasambae nchi nzima iwe kama huko Moshi? hao hao watano 5 ambao jamaa kawaona wakifa sana huko moshi ndio nauliza itachukua kuwa hivyo kwa mikoa mengine pia?
 
Nami leo ndiyo naamini nimesikia Sana Kwa watu.
Nasikitika nimempoteza uncle wangu asubuhi ya leo mbaya zaidi nilikuwa naye kwenye mazishi ya uncle wangu mwingine siku Sita nyuma yeye karudi mkoani hajachukua round.
Kwa kifupi nimefiwa na uncle zangu wawili ndani ya wiki mbili acheni tu...
Pole mkuu
 
Back
Top Bottom