Leo ni Birthday yangu, miaka 25 sina mtoto wala uelekeo wa maisha

Leo ni Birthday yangu, miaka 25 sina mtoto wala uelekeo wa maisha

Nilikuwa sina hili wala lile, ghafla sms kutoka Voda ikaingia kwa simu na kunikumbusha kuwa leo ni Bday yangu

Kwa furaha nikatoka ndani ya chumba changu na kusimama nje ya nyumba ya Mzee Matula, nikapiga kelele kwa sauti kuu "Happy Birthdaaaaay to meeeee". Ile kugeuka nyuma nashangaa majirani wameduwaa

Sikujali, nikaingia zangu magetoni, nikaweka nyimbo za father christmas, muda wa kama dakika 2 hivi nikahisi watu wanafanya kikao hapo nje, ile kusogeza skio kwa umakini, kumbe wananiteta!

Ma Masudi: Huyu kijana amepanga hapa tokea 2021, hata na mimi nimemkuta, kile alichokuwa nacho ndani ndo hicho hicho alichonacho mpaka sasa. Analalia ulimi kama nyoka

Ma Shaban: 😂Uwiii, tokea aachane na kale kabinti kanakojiita Ashura Mabomu, hajawahi kuingiza demu humo ndani, sijui uwaga anajimaliza mwenyewe

Ma Masudi: Usiniambie, ndo maana anakaukiana ngozi jamani, si aseme tu hata mimi nitampa kwa kumsaidia jamani😯

Ma Shabani: Jamaa anaishi maisha ya kitawa sana, hadi leo hii 2025 hana habari ya mke wala mtoto wa kusingizia, atakufa kibudu huyu mbw*

...na mengineyo mengi ya kusikitisha

Ila suala la familia na mtoto limetachi sana.
# Ndoa ni utapeli

Na hili nalo mkalitazame kwa kina
Ulijaribu japo kuutaafuta?
 
Back
Top Bottom