Leo ni siku ya tatu jogoo wangu hawiki

Leo ni siku ya tatu jogoo wangu hawiki

amatolo

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2017
Posts
690
Reaction score
712
Habari za asubuhi wakuu, kisa hiki ni cha kweli na kimenitokea mimi mwenyewe.

Nimekuwa na tatizo la kupata maumivu ya kawaida na ya kipindi kifupi, maumivu haya huwa nayasikia kwenye korodani zangu, tatizo hili lilianza miaka mitatu iliyopita. Tatizo lilipoanza nilihisi ni mshipa wa ngiri nilienda kwa watalaam nikapewa dawa nikatumia lakini tatizo halikuisha, pia nilipohojiwa na mtalaam dalili zake zilikuwa tofauti kabsa na zile za mshipa wa ngiri,.
1. Sijawahi pata tatizo lolote wakati wa baridi, au ngurumo
2. Sijawahi pata maswahibu yoyote yale wanayopata wenye tatizo la ngiri.
3. Maumivu yamekuwa yakitokea muda wowote ule (nimekuwa nayasika kwa muda na badae kupotea), maumivu haya huanzia kwenye korodani na kupanda taratibu kupitia mirija ya korodani na badae hupotea, maumivu haya yakianza huwa napata maumivu kidogo tumboni.

Siku tano zilizopita maumivu haya yalianza mfululizo, korodani zilikuwa zinauma muda wote totauti na kipindi cha nyuma ambapo nilikuwa nayapata kwa dadika moja au mbili na badae kupotea kwa muda mrefu (mwezi mmoja mpaka minne), tofauti na kipindi hiki. Hali hii imeendelea kwa muda wa siku tatu/nne mfululizo cha ajaabu ambacho nimeshindwa kukielewa toka juzi maumivu haya siyasikii tena lakini ukweli ni kwamba bwana mkubwa kalala fofofo, hata nikienda kukojoa jamaa kasinzia tu, nimejaribu kujichunguza toka jana pindi niamkapo lakini jogoo bado kasinzia tu, nmejaribu kuvuta hisia kama nataka kuingia ulingoni lakin jamaa bado kazinda. Najua humu ndani tuna vipaji vyote naomba kama kuna mwenye kuelewa tatizo hili anisaidie. Utani ufuate baada ya suluhisho, Ahsante
 
Hahahaaaa nacheka Kama mazuri, eti bwna mkubwa kalala fofofo

Kwahiyo kunjiginjigi ndiy basi tenaaaa mayooooo weeeeee![emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Hemu taja umri wako,
Alafu sema kama umewahi kupata ajali ya hapo eneo la korodan na kukupa maumivu?

Pia kuna sehemu yoyote ukiigusa pemben na korodan unahis kama shimo shimo?
 
Hahahaaaa nacheka Kama mazuri, eti bwna mkubwa kalala fofofo

Kwahiyo kunjiginjigi ndiy basi tenaaaa mayooooo weeeeee![emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Mkuu hujafa hujaumbika. Skatai jokes ila bora ingefuata baada ya kupata suluhisho
 
Hemu taja umri wako,
Alafu sema kama umewahi kupata ajali ya hapo eneo la korodan na kukupa maumivu?

Pia kuna sehemu yoyote ukiigusa pemben na korodan unahis kama shimo shimo?
Umri 27 yrs
Sijajoa ila nina mzazi mwenzangu ambae tumejaliwa watoto wawili, wakanza nilimpata wakati niko field mwaka wa tatu chuo
Niliwahi kupata jipu utotoni chini ya kitovu karibu kabisa na mavuzi
Hakuna sehem yenye shimo
 
We ni mseng******
Hahahaaaa nacheka Kama mazuri, eti bwna mkubwa kalala fofofo

Kwahiyo kunjiginjigi ndiy basi tenaaaa mayooooo weeeeee![emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Nenda hospitali kwa masSpecialist wa magonjwa ya mkojo..wanaitwa UROLOGIST...kumbuka kwenda hospitali kubwa..usiende kwenye vizahanati maana utapoteza pesa zako bure.
 
Pole sana Mzee Baba
tapatalk_1474308410133.jpeg
 
Ukishishika korodan kwa wakat ambao maumivu yametulia, unahis hali ya maumivu?
Umri 27 yrs
Sijajoa ila nina mzazi mwenzangu ambae tumejaliwa watoto wawili, wakanza nilimpata wakati niko field mwaka wa tatu chuo
Niliwahi kupata jipu utotoni chini ya kitovu karibu kabisa na mavuzi
Hakuna sehem yenye shimo
 
Sijasoma uzi wote, kutokana na kichwa cha uzi... tafuta hela ya kutosha kupata mahitaji muhimu, jifunze kuwa jasiri na ondoa hofu, hata ukila mananasi asubuhi mchana na jioni jogoo atasimama pale unapotaka tena atalala lava ikishsmwagika au ukitaka.
 
Linatibika hospital kwan kisababishi ni bacteria, hasa wanao kuingia wakat wakufanya mapenz kupelekea inflammation ya testicle au epididymis
Ndio huwa nasikia maumivu
 
Back
Top Bottom