Nimeona mjadala mahali watu wakibishana kuwa leo ni Uhuru wa Tanzania au Tanganyika, nami nimeona kwa manufaa ya wengi nishiriki mjadala huu kwa kutoa mchango wangu wa mawazo.
Siku ya Uhuru Ina maana iliyo sawa na siku ya kuzaliwa kwa mtu. Kama mtu alizaliwa akawa anaitwa Juma atakaposheherekea siku yake ya kuzaliwa atasheherekea Kama Juma lakini Juma akibadili jina akaitwa Hassan, tutasheherekea siku ya kuzaliwa Hassan na sio Juma.
Kutokana na mfano huo wa kubadili jina kwa Juma kuwa Hassan kutafanya kumbukumbu pekee inayobaki kukumbukwa ni ya Hassan na sio Juma. Mifano ipo mingi ya watu kubadili jina ili kupata jina lenye nguvu na maana kubwa zaidi lakini kwa ufupi nigusie mifano michache ya kwenye biblia. Abram alibadili jina na kuwa Abraham , Simon alibadili jina kuwa Petro.
Kubadili jina kunaweza kuwa na maana nyingi lakini kubwa kuliko zote ni kufuta kumbukumbu za mateso na maumivu za jina la zamani na kuvuta baraka na mafanikio kwa jina jipya.
Kama inavyokuwa kwa mtu kubadili jina, ndivyo iliyokuwa inaitwa Tanganyika imebadilishwa kuwa Tanzania. Ile kumbukumbu mbaya ya mateso na maumivu ya Tanganyika imebadilishwa kwa kuwa Tanzania.
Kwa sababu Tanganyika haipo na imebadilishwa ,toka siku ya Kwanza baada ya kubadilishwa kumbukumbu zilikuwa zinaishi na zisizofutika Tanganyika zikawa za Tanzania. Kama vile mtu ambavyo hawezi kufuta siku yake ya kuzaliwa ndivyo nchi haiwezi kufuta siku yake ya Uhuru Ila inaweza kubadili jina.
Nihitimishe kwa kusema Leo ni siku ya Uhuru wa Tanzania, hakuna tena inayoitwa Tanganyika Kama vile ambavyo hakuna Juma baada ya kubadili jina kuwa Hassan.