LGE2024 Leo nimechukia sana nilipokuwa napiga kura kijijini kwangu Moshi, eti hakuna mpinzani hata mmoja anagombea na nimefanya kweli kwenye sanduku la kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Nimefika kupiga kura kituoni mida ya saa 5 asubuhi. Watu hawakuwa wengi na walikuwa wanakuja taratibu, wengine wapo shambani wanasubiri wapigiwe simu zamu yao ikikaribia.

Kilichoniudhi ni kukuta hakuna mpinzani hata mmoja anagombea, wote ni CCM tupu! Halafu nikakuta ule mtindo wa enzi za Mwalimu Nyerere wa NDIYO/HAPANA kwa mgombea asiye na mpinzani!

Nilichofanya ni kutembeza kura ya HAPANA kwa wagombea wote wa CCM kwenye karatasi bila hata kuangalia majina yao. Msimamizi wa uchaguzi akasema wapiga kura wote mkienda haraka haraka kama huyu tutamaliza mapema zoezi hili.

Moshi hakuna wapinzani, kweli!!!?
 
Kwani wewe sio mpinzani?Mkiambiwa hampo serious mnadhani utani.Uchaguzi unahitaji mikakati na pesa.Vyote hamna na viongozi wenu wanakula ruzuku mtashinda kwa miujiza?
 
Na unafurahia hilo?!
 
Kwani wewe sio mpinzani?Mkiambiwa hampo serious mnadhani utani.Uchaguzi unahitaji mikakati na pesa.Vyote hamna na viongozi wenu wanakula ruzuku mtashinda kwa miujiza?
HUJUI WAMEENGULIWA
 
Back
Top Bottom