Leo nimefunga biashara yangu

Leo nimefunga biashara yangu

TRA inafanya kazi mwa sifa taasisi za serikali ni kama wanashindana kwenye kuminya watu ili waonekane wameingiza mapato makubwa.

TRA
TRAFFIC
TANESCO
DAWASCO

Hizi team zinashindana nani kinara wakuingiza pesa nyingi serikalini kwa njia yyte iwezekanayo.

TRA hata wakuandikie barua kukubali ufanye jambo Hata siku 1 usije itupa barua waliyokuandikia, utakuja kurukwa kweupe na hutoamini hata uweke mwanasheria gani.

TRA yale macomputer yao ni geresha tu hawahifadhi data za watu wao wanajua tu hifadhi ma faini,ma ongezeko ya kodi unayodaiwa,nk

Ila uende punguza deni, hawana muda wa kuhifadhi hiyo kumbukumbu.. so hakikisha unapojihusisha na TRA una ofisi yako binafsi kwako na secretary wako home wakukutunzia DATA zako or else anyday utalia.

FUNGA BIASHARA hiyo tumia TIN ya mtu fungua biashara hyo hyo kwa TIN ingine tena eneo hilo hilo.

Hawana wanachoweza kukufanya ila Usilipe kodi kama umefunga hyo biashara or else useme unataka kutoka nnje ya hii nchi.
Upigaji?

TANESCO TRA Tanzania @DAWASCO
 
Wakuu wiki iliyopita nilienda TRA kufunga biashara yangu baada ya kuona makadirio niliyoandikiwa ni makubwa mno na hayaendani na biashara.

Mwanzo Nilienda huko TRA kuomba kupunguziwa kodi tawi lao la chanika ilala. Kama kawaida wakamtuma afisa wao aje akague biashara yangu ili aone biashara hii inaendana na makadirio niliyoandikiwa au la!.

Basi afisa wao siku alivyokuja akakiri imekosewa nilivyokadiriwa. Na akaniambie niende chanika ofisini nitapunguziwa kodi

Siku nilivyorudi tena chanika nikakutana huyo Mama bonge Mkuu wao, huwezi ukaamini alikataa kunipunguzia. Na kwa nyodo akanaimbia kama vipi funga hiyo biashara. Maana hawezi kureverse alichokadiria

Baada ya kufikiria mno ikiwa sina namna nikaamua kufunga ile biashara. Kwa kufata utaratibu walionelekeza. Ikiwa ni pamoja na kulipa deni - nilifanya hivyo

Shida nikuwa kila mara natumiwa sms na hao TRA chanika kukumbushwa kulipa kodi ya awamu ya hii wakati nishafunga biashara . Nimeenda huko hawaoneshi ushirikiriano. Kila siku Njoo kesho.

Nifanyeje wadau
kukwepa ulishindwa mkuu?
 
Back
Top Bottom