Supapawa
JF-Expert Member
- Aug 29, 2026
- 1,076
- 2,690
Wakuu habari ya Jumapili,
Leo asubuhi nilikuwa kanisani kwenye ibada. Mchungaji alikuwa anahubiri, alikuwa anahubiri kwa kuchanganya maneno ya kiswahili na kiingereza. Si mnawajua wachungaji wetu walivyo wajuaji!
Mimi kama kawaida yangu popote ninakokuwa huwa nakuja kuchungulia humu JF Ili kujua kinachojiri. Wakati naperuzi humu kisirisiri kanisani, nikikutana na comment ya jamaa mmoja hivi iliyonifanya nicheke kwa sauti kubwa sana bila kujizuia.
Salaaaalee! Watu wote kanisani nao walicheka kwa nguvu baada ya kusikia kicheko changu. Dah! Wao walidhani mimi nilicheka kwa sababu mchungaji kaongea broken English, kube mimi nimechekeshwa na comment ya mja mmoja wa humu JF.
Cha kushangaza, pale kanisani kulikuwa na masomi wengi, walikuwepo walimu wa secondary, mwenyekiti wa vijana wa CCM wilaya, na wasomi wengine wengi ambao nao walicheka pasina breki.
Kilichonikitisha ni kuona mchungaji wa watu akiishiwa na komfidensi kwani hakujua kilichofanya watu wacheke.
Aisee! Leo ndiyo nimegundua kuwa watanzania wengi ni bendera fuata upepo, ukifanya kitu fulani nao lazima wakifuate.
Mwisho, natambua kuwa kuperuzi katika ya ibada ni kosa na naomba mnisamehe bure!
Seran,
Harmful,
Nelly.