Leo nimekumbuka kesi ya Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, ilipelekea mahabusu kugoma kwenda mahakamani siku tano Dar wakidai dhamana yake ifutwe

Nakumbuka kuna siku nilikuwa na kaka yangu kwenye Harrier yake ndio ina wiki tu tangu ainunue kwahiyo alikuwa na kimuhemuhe nayo sana tulipofika kwenye mataa pale Masasi mjini sisi tulisimama kama inavyotakiwa, chakushangaza bodaboda akaja akagonga taa ya pembeni ikapiga ufa brother akashuka akamfuata kwa wema tu ila yule bodaboda akaanza kutukana matusi ya nguoni wakati kosa ni lake na ukifìkiria yule bodaboda kiumri ni mdogo sana brother yule ni kama mwanae tu nikasema haya ndio ya Ditopile.
 
Ditopile alishafariki mkuu
Mariam Ditopile mbunge wa viti maalum Dodoma. Kafungua mdomo wake karibuni kuwashambulia wanaopinga mkataba wa uwekezaji bandari wa DP World. Anataka wadhibitiwe, hii imetukumbusha uovu wa Mzee Ditopile.

Tunahisi ukatili wa kushughulikia watu unaopishana nao kimtazamo au jambo lolote upo kwenye damu yake ni urithi.
 
Nakumbuka kuna siku nilikuwa na kaka yangu kwenye Harrier yake ndio ina wiki tu tangu ainunue kwahiyo alikuwa na kimuhemuhe nayo sana tulipofika kwenye mataa pale masasi mjini sisi tulisimama kama inavyotakiwa chakushangaza bodaboda akaja akagonga taa ya pembeni ikapiga ufa brother akashuka akamfuata kwa wema tu ila yule bodaboda akaanza kutukana matusi ya nguoni wakati kosa ni lake na ukifìkiria yule bodaboda kiumri ni mdogo sana brother yule ni kama mwanae tu nikasema haya ndio ya ditopile
Lakini yeye hakumshughulikia dereva wa boda boda kama alivyofanya Dito kwa dereva wa daladala?
Wakati mwingine kudhibiti hasira au mihemko ni jambo la busara unaepuka mengi sana.
 
Sikia nikuambie kitu brother tulimshikashika tu na wakati huo ni alhaj ana miezi miwili tangu arudi kuhiji....fikiria mtoto wa miaka 23 anatukana matusi ya nguoni kwa mtu mwenye miaka zaidi ya 50 tena anamtusi mpaka mama yako aliefariki halafu unaongea kizembe tu eti udhibiti hasira
 
Rejea zinasema dereva aliomba radhi, baadae akafunga vioo na kufunga mlango(hakufanya majibizano), hakushuka kwenye gari kama alivyoamriwa na Ditopile labda aliogopa kutokana na maneno ya Ditopile na dereva wake..
 
Kwanini aligoma kushuka unadai aliomba radhi ila akafunga vioo na milango... Ditopile hakuwa mjinga huyo dereva tax alijibu majibu ya kunya
 
Kwa hiyo Ditopile alikuwa askari usalama barabarani hadi huyo dereva atii kushuka ndani ya gari?
Hata askari akikupa amri ya kushuka kwenye gari kwa makosa ya traffic au matusi hana mamlaka ya kukuhukumu kifo.
 
Kiburi ndicho kilimponza huyo fala dereva ambae alikuwa na akili za kipumbavu kama bodaboda wa leo walivyo
 
Kwanini aligoma kushuka unadai aliomba radhi ila akafunga vioo na milango... Ditopile hakuwa mjinga huyo dereva tax alijibu majibu ya kunya
Hata Kama dereva alijibu majibu ya kunya,Ditopile bado alaikua na uwezo wa kumwambia DTO au RTO wamuweke ndani dereva hadi akili yake itakapo kaa sawa kuliko kumpiga dereva Chuma mbele ya abiria kwenye daladala!! Dito alikosea sana, ndiyo maana baada lile tukio na mbwembwe zote za Ditopile zikaishaa, mwisho wa siku watu wanakuja sikia Jamaa kafia Nyumba ya wageni huko kwao Tabora!!
 
Unajuaje kuwa mbwembwe ziliisha? Huyo dereva alistahili chuma ni kama bodaboda tu akili zao ni watu wa matusi mno bila kuangalia wanayemtusi ni nani
 
Katika suala lililoitikisa fani ya sheria na utoaji haki ni tukio la miaka 17 iliyopita kutokana na mlolongo wa matukio yaliyojiri baada ya kufunguliwa mashitaka ya mauaji kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora wa wakati huo, Ukiwaona Ditople Mzuzuri baada kumpiga risasi dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33) mwaka 2006.

Pia, soma=> Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Kesi ya mshitakiwa huyo ilisababisha mahabusu katika magereza ya Dar es Salaam na kwingineko, kugoma kuingia kwenye magari kwenda mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa kesi zao. Mgomo huo wa siku tano haukuwahi kutokea nchini.

Upelelezi wa kesi dhidi ya Ditopile ulichukua miezi minne tu hadi mashitaka kubadilishwa kutoka mauaji ya kukusudia na kuwa mauaji ya kutokusudia, na hivyo kupewa dhamana.

Hilo liliwakasirisha sana mahabusu wengine waliokuwa wakingojea kesi zao (pamoja na zile kesi za mauaji), ambazo baadhi yao walikuwa mahabusu kwa miaka kadha. Walitaka nao wafanyiwe uharaka wa namna hiyo katika kuchunguza kesi zao, la sivyo dhamana ya Ditopile ifutwe.

View attachment 2685405
Askari kanzu wakimpeleka Athumani Ukiwaona Ditopile Mzuzuri lupango mara baada ya kusomewa shtaka la mauaji mbele ya hakimu mkazi, Michael Lugulu mahakama ya Kisutu November 06, 2006.​

Kesi ya Ditopile ili-trend kwa matukio mengi ikiwemo ndugu wa Ditopile kuwarushia maneno na kuwafanyia vurugu ikiwemo kuwamwagia maji waandishi wa habari waliokuwa wanafatilia kesi hiyo kwa madai ya 'kuishikia bango'. Baada ya tukio hilo kesi ya Ditopile ilitawala 'Front Page' zote za magazeti makubwa na prime ya TV stations 'waandishi wakilipa kisasi'

Pia kapteni Ditopile akiwa mahabusu, alipata bahati ya kutembelewa na Rais aliye madarakani wakati huo, Jakaya Kikwete akisema ni rafiki yake wa siku nyingi.

Ndani ya miezi minne uchunguzi ulikamilika na kesi yake ikabadilishwa kutoka mauaji ya kukusudia kwenda mauaji bila kukusudia.

Baada ya kesi kubadilishwa, Ditopile alitoka nje kwa dhamana.

View attachment 2685448
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimfariji mjane wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Marehemu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri huko nyumbani kwake Upanga. Kulia ni Mariam Ditopile mtoto wa marehemu na nyuma ya Rais ni mtoto wa Rais, Rashid Chodo Kikwete.(April 21, 2008)

Hata hivyo, mwaka 2008 ikiwa bado kesi yake haijapata hukumu, kapteni Ditopile aliaga dunia katika hoteli ya Hilux mkoani Morogoro akiwa na mke Mdogo. Sababu ilitajwa kuwa mshtuko wa moyo.

Pia, Soma=> Ukiwaona Ditopile afariki dunia
Umenikumbusha mbali sana. Huyu mwamba alifanya mbaya sana. Nilitazama viongozi wanavyolitolea maelezo ya Siyo kipindi kile, nilibaki kupigwa butwaa sana. Haikuwa kawaida kabisa katika mahakama kufunguliwa mashtaka ya kuua bila kukusudia. Kwa mara ya kwanza ilikuwa Kwa huyu Ditopile.
 
Ile kesi ilikuwa na mafunzo mengi sana kwa viongozi wa Serikali. Kwamba cheo ni dhamana. Kiburi si Uungwana. Pamoja na madaraka yote uliyonayo, hauna haki ya kutoa uhai wa mtu, kwa sababu tu gari yako imegongwa, na gari yenyewe imenunuliwa kwa pesa za walipa kodi.

Halafu gari yenyewe Ina insurance fully covered. Asubuhi yake angepewa gari nyingine. Lakini kwa kulewa madaraka akajisahau. Ubongo wa yule dogo ukamwagwa.

Raisi mstahafu, pamoja na shutuma nyingi anazopewa, hapa ndipo alipoonyesha ukomavu wa akili; kwamba umeua mtu asiye na hatia, basi tuache sheria ichukue mkondo wake. Ushkaji tuweke pembeni.

Ile ilikuwa bab kubwa. Na jela akaenda kumtembelea. Kwamba, yeye Rais Kikwete na mtuhumiwa wametoka mbali sana (damudamu) lakini suala la kumua yule kijana litaamuluwa na mahakama. That was really cool [emoji41].
Alafu alipogongewa na alikoenda kumwaga ubongo Kuna mwendo kitambo Fulani. Haikuwa papo Kwa papo.
 
unamaanisha nini unaposema alienda jela? Kila mtu atakufa ila nikuulize swali umewahi kuletewa dharau au kuchokozwa?
Ditopile alikwenda jela akatoka kwa dhamana kwa kosa hilo tunalozungumzia.
Nimewahi kuchokozwa na kuletewa dharau na boda boda tena mbele ya mwanamke ambaye watoto wangu wanamuita mama.
Nimewahi kuletewa dharau, uchokozi na mwanamke ndani ya usafiri wa umma tena na matusi ya kutisha kisa kidogo tu. Nimedondosha kitu nikashuka kuokota, niliacha begi lenye laptop juu ya siti ile narudi nakuta kalikalia begi anasema hakuna kuzuia siti kama yako kisha kaanza kuporomosha matusi.
 
Unajuaje kuwa mbwembwe ziliisha? Huyo dereva alistahili chuma ni kama bodaboda tu akili zao ni watu wa matusi mno bila kuangalia wanayemtusi ni nani
Achaa utoto,matusi hayaamuliwi kwa kupigwa Chuma kumbuka tunaishi really life na siyo Maisha ya Movie, isije kua zile movie za kimarekani za kupigana risasi hovyo hovyo zimekuharibu,wwe unaamini Chuma ndiyo kila kitu!!
 
Katika suala lililoitikisa fani ya sheria na utoaji haki ni tukio la miaka 17 iliyopita kutokana na mlolongo wa matukio yaliyojiri baada ya kufunguliwa mashitaka ya mauaji kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora wa wakati huo, Ukiwaona Ditople Mzuzuri baada kumpiga risasi dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33) mwaka 2006.

Pia, soma=> Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Kesi ya mshitakiwa huyo ilisababisha mahabusu katika magereza ya Dar es Salaam na kwingineko, kugoma kuingia kwenye magari kwenda mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa kesi zao. Mgomo huo wa siku tano haukuwahi kutokea nchini.

Upelelezi wa kesi dhidi ya Ditopile ulichukua miezi minne tu hadi mashitaka kubadilishwa kutoka mauaji ya kukusudia na kuwa mauaji ya kutokusudia, na hivyo kupewa dhamana.

Hilo liliwakasirisha sana mahabusu wengine waliokuwa wakingojea kesi zao (pamoja na zile kesi za mauaji), ambazo baadhi yao walikuwa mahabusu kwa miaka kadha. Walitaka nao wafanyiwe uharaka wa namna hiyo katika kuchunguza kesi zao, la sivyo dhamana ya Ditopile ifutwe.

View attachment 2685405
Askari kanzu wakimpeleka Athumani Ukiwaona Ditopile Mzuzuri lupango mara baada ya kusomewa shtaka la mauaji mbele ya hakimu mkazi, Michael Lugulu mahakama ya Kisutu November 06, 2006.​

Kesi ya Ditopile ili-trend kwa matukio mengi ikiwemo ndugu wa Ditopile kuwarushia maneno na kuwafanyia vurugu ikiwemo kuwamwagia maji waandishi wa habari waliokuwa wanafatilia kesi hiyo kwa madai ya 'kuishikia bango'. Baada ya tukio hilo kesi ya Ditopile ilitawala 'Front Page' zote za magazeti makubwa na prime ya TV stations 'waandishi wakilipa kisasi'

Pia kapteni Ditopile akiwa mahabusu, alipata bahati ya kutembelewa na Rais aliye madarakani wakati huo, Jakaya Kikwete akisema ni rafiki yake wa siku nyingi.

Ndani ya miezi minne uchunguzi ulikamilika na kesi yake ikabadilishwa kutoka mauaji ya kukusudia kwenda mauaji bila kukusudia.

Baada ya kesi kubadilishwa, Ditopile alitoka nje kwa dhamana.

View attachment 2685448
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimfariji mjane wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Marehemu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri huko nyumbani kwake Upanga. Kulia ni Mariam Ditopile mtoto wa marehemu na nyuma ya Rais ni mtoto wa Rais, Rashid Chodo Kikwete.(April 21, 2008)

Hata hivyo, mwaka 2008 ikiwa bado kesi yake haijapata hukumu, kapteni Ditopile aliaga dunia katika hoteli ya Hilux mkoani Morogoro akiwa na mke Mdogo. Sababu ilitajwa kuwa mshtuko wa moyo.

Pia, Soma=> Ukiwaona Ditopile afariki dunia
Hivi huyo msichana mdogo ndiyo huyu domokaya wa sisieim anayekazia kuunga mkono upumbaf wa mikataba ya hovyo?
 
Hata Kama dereva alijibu majibu ya kunya,Ditopile bado alaikua na uwezo wa kumwambia DTO au RTO wamuweke ndani dereva hadi akili yake itakapo kaa sawa kuliko kumpiga dereva Chuma mbele ya abiria kwenye daladala!! Dito alikosea sana, ndiyo maana baada lile tukio na mbwembwe zote za Ditopile zikaishaa, mwisho wa siku watu wanakuja sikia Jamaa kafia Nyumba ya wageni huko kwao Tabora!!
Lack of wisdom.Viongozi wengi sana wapo hivyo
 
Ditopile alikwenda jela akatoka kwa dhamana kwa kosa hilo tunalozungumzia.
Nimewahi kuchokozwa na kuletewa dharau na boda boda tena mbele ya mwanamke ambaye watoto wangu wanamuita mama.
Nimewahi kuletewa dharau, uchokozi na mwanamke ndani ya usafiri wa umma tena na matusi ya kutisha kisa kidogo tu. Nimedondosha kitu nikashuka kuokota, niliacha begi lenye laptop juu ya siti ile narudi nakuta kalikalia begi anasema hakuna kuzuia siti kama yako kisha kaanza kuporomosha matusi.
Wewe ukafanyaje?
 
Back
Top Bottom