Leo nimekumbuka kesi ya Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, ilipelekea mahabusu kugoma kwenda mahakamani siku tano Dar wakidai dhamana yake ifutwe

Leo nimekumbuka kesi ya Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, ilipelekea mahabusu kugoma kwenda mahakamani siku tano Dar wakidai dhamana yake ifutwe

Hii nchi bhana! Eti hako kabinti kake tayari ni kabunge ka viti maalum kakila posho na mshahara mnono. Mimi Tate Mkuu bado napambama tu na hali yangu huku Usambaani.

Yaani hiyo 2006 wakati kakiwa kabinti kadogo tu, mimi tayari nilikuwa mtu mzima kabisa. ccm Mungu anawaona kudadek zenu. Yaani keki ya Taifa mnatafuna nyinyi wenyewe tu na familia zenu.
Sasa hivi ni fundi pia wa kukoboa. Anahonga Sana, akimkamata demu wako au mkeo basi jua imekula kwako
 
Hata Kama dereva alijibu majibu ya kunya,Ditopile bado alaikua na uwezo wa kumwambia DTO au RTO wamuweke ndani dereva hadi akili yake itakapo kaa sawa kuliko kumpiga dereva Chuma mbele ya abiria kwenye daladala!! Dito alikosea sana, ndiyo maana baada lile tukio na mbwembwe zote za Ditopile zikaishaa, mwisho wa siku watu wanakuja sikia Jamaa kafia Nyumba ya wageni huko kwao Tabora!!
Alifia Moro mkuu kama sikosei.
 
Ni kweli kabisa. Yule bwana aliua kwa kukusudia kabisa. (Mtuhumiwa, marehemu Ditopile) alimwambia swahiba yangu, ambae pia alikuwa mtu wake wa karibu kwamba anauhakika nguvu za giza zilitumika kumfanya amuue yule kijana. Kwamba, ni kama vile akili zilimruka. Haktambua alilokuwa anafanya.

Mhhh....Mzee wa Saigon nani alimroga?
 
Ile kesi ilikuwa na mafunzo mengi sana kwa viongozi wa Serikali. Kwamba cheo ni dhamana. Kiburi si Uungwana. Pamoja na madaraka yote uliyonayo, hauna haki ya kutoa uhai wa mtu, kwa sababu tu gari yako imegongwa, na gari yenyewe imenunuliwa kwa pesa za walipa kodi.

Halafu gari yenyewe Ina insurance fully covered. Asubuhi yake angepewa gari nyingine. Lakini kwa kulewa madaraka akajisahau. Ubongo wa yule dogo ukamwagwa.

Raisi mstahafu, pamoja na shutuma nyingi anazopewa, hapa ndipo alipoonyesha ukomavu wa akili; kwamba umeua mtu asiye na hatia, basi tuache sheria ichukue mkondo wake. Ushkaji tuweke pembeni.

Ile ilikuwa bab kubwa. Na jela akaenda kumtembelea. Kwamba, yeye Rais Kikwete na mtuhumiwa wametoka mbali sana (damudamu) lakini suala la kumua yule kijana litaamuluwa na mahakama. That was really cool [emoji41].
Familia ya Marehemu ikanunuliwa makochi mapya na msiba ukageuka kuwa wa Serikali.
 
Back
Top Bottom