Leo nimemfumania live bila chenga

Leo nimemfumania live bila chenga

Kuna siku nilimwambia mdogo wangu, kama hautaki karaha usijihusishe kabisa na mambo ya mahusiano iwe mapenzi au ndoa. Ukiamua tu kuingia kwenye hii tasnia, hayo yategemee japo sio kwa wote. Pole sana
Nilikuelewa..Na Sijaingia Kwenye Mambo...Maana hata sijawah sikia story nzur ya hayo mambo zaidi ya vilio.mm..Nashukuru Kwa Muongozo Wako!!! [emoji1] [emoji1] !!
 
Mbona na wewe huwa unachepuka, sema tu jamaa hajawahi kukufumania
 
Kuna siku nilimwambia mdogo wangu, kama hautaki karaha usijihusishe kabisa na mambo ya mahusiano iwe mapenzi au ndoa. Ukiamua tu kuingia kwenye hii tasnia, hayo yategemee japo sio kwa wote. Pole sana

Mapenzi ndio yanayoleta hadithi hapa duniani.
 
Habari wana MMU,

Nina mpenzi wangu ambaye tuna muda kidogo. Hapa kati niligundua anachepuka baada ya kuona msg kwenye simu yake,nilipomuuliza akakataa katakata na ugomvi juu nkajishusha yakaisha but moyoni mwangu nlikua namchunguza kimya kimya.

Kwa kawaida huwa tunapitiana asbh kwenda kazini kwan ofisi zetu zipo karibu, basi Leo nimeenda kama kawa nikagonga but hakufungua ila nilisikia movement ndani ameamka akawasha gesi na kubandika Maji ya kuoga basi nikajua atafungua mlango, nikaona kimya ila machale yakanicheza nikapanga kukaa nje mpaka nione mwisho, simu zangu nikaweka silent baada ya dk 40 hivi nikasikia sauti ya mwanamke ndani kumbe ndo alikua anamwandalia maji.

Ile kufungua mlango akakutana na macho yangu makavu nikamsalimia nikaingia chumbani nikamsalimia binti nikarudi kukaa sebuleni, bidada akanikaribisha kwa adabu zote nikamwambia apumzike tu asijali, kaka katoka kuoga anajishaua kuniuliza eti kwanini sijaenda kazini nimesimama tu nje m sikumjibu ktu akaingia rum kuvaa mi nimekaa tu sebuleni.

Sikutaka ugomvi kiukweli coz najijua hasira zangu ningechoma mtu kisu bure, basi bidada akavaa nguo huyo akaondoka na akaniaga eti Dada bye nikamwambia ok karibu tena! Alipoondoka nikamuuliza is it me or her akakosa jibu, nikaondoka zangu!

Now msg kibao za maelezo mimi sijajibu hata moja, hivi wanaume kwanini hamtosheki jamani? Bora nibaki single tu kuliko kuleteana magonjwa

Mapenzi yako hivyo kwa pande zote. Leo umemfuma live mme , kwa upande wa pili haya hutokea pia. Mapenzi si mchezo wa kuingia bila plan B.
 
''hivi wanaume kwanini hamtosheki jamani? ''

Dada zangu wa siku hizi hapa ndipo mnapofanya kosa kubwa sana kudhani mwanamume anapokosa kuwa mwaminifu kwako ni kwa sababu ya kutotosheka.

1. wengi mpo kwenye mahusiano ambayo hayakuanza rasmi, mlikutana na mkaanza ''kugegedana'' na ukaridhia kwa kudhani kwamba hiyo inatosha kumfanya jamaa aone kuwa wewe peke yako unatosha. Ukweli ni kwamba wengi huwa mnaingia kwenye mahusiano na wanaume wa wanawake wengine.

2. Kutokuwa wazi na uwezo wa kujieleza. Wengi mpo kwenye mahusiano na wala huulizi kama jamaa ana mpango wa muda mrefu au yupo na wewe kwa muda tu?

Hii dunia ya leo mkiendelea hivi mtaumia sana, jamaa anajua anachokifanya na bahati nzuri anajua utakubali msamaha wake halafu ataendelea na mambo yake kama kawaida.

Pole, chukua muda wako na ujichunguze kama unastahili kuwa na mahusiano na mtu wa namna hiyo....
 
Huyo si wako ndo maana hayo yame happen,tulia utapata wako ataekupenda kwa dhati.
 
Back
Top Bottom