Leo nimeondoka rasmi jijini Dar es Salaam baada ya kupata mchongo Jehanamu

Leo nimeondoka rasmi jijini Dar es Salaam baada ya kupata mchongo Jehanamu

Maisha Popote Ila Sio Kwa Ubaya Mungu Naomba Unibakishe Maisha Yangu Yote Na Familia Yangu Ibaki Dar Es Salaam Bandari Salama,AMEEN
 
Ukitaka kuishi unapopataka wewe achana na habari za kuajiriwa.
 
Mkuu kwanza hongera kwa kupata kazi yenye uhakika,ambayo inaambatana na kupewa bima ya afya,uhakika wa pesa kila mwezi itakayoambatana na annual increment,na finally uko subjected kwenye mikopo endapo utahitaji kwa siku zijazo,pili fanya kazi kwa bidii uwatumikie watanzania kwa moyo wako wote,kwani ulisoma na kuandaliwa ili utoe huduma kwa mwananchi yeyote ambaye yupo popote pale Tanzania bara au visiwani.Nakupa hongera tena mkuu.Mwanzo mgumu.
Unajifanya mzalendo we ukipelekwa kakonko utaandika barua uache kazi
 
Pole sana nichangamoto tuu za maisha. Kaa kwa muda hata miezi mitatu uombe uhamisho
 
Hakika dar es salaam ni Mji ulionipa marafiki wengi, network kubwa na hata pesa ya kuishi japo kuna siku mji huu ulinilaza njaa.

Asubuhi ya leo wakati natoka mbezi kuja huku mkoani chozi limeni tililika sana(fear of new changes)

Doh! nimefika mkoani , nikaenda kuripoti kituo changu cha kazi nilichopangiwa na shirika moja binafsi hapa nchini! ni aibu sana kwakweli!.

Wafanyakazi wenye certificate,diploma wanavimba ofisini na kipupwe mimi wamenipeleka kijijini wastani wa kilomita 120 kutoka mjini,hakuna makazi bora,maji ya tabu,usafiri wa shida na network inashika haloteli tu.

Nimeikuta jamii ni walevi mno, sura zao zimekosa nuru, najiona kabisa napotea kwenye ulevi wa kupindukia huku kijijini, wanatumia punda kwenda kuchota maji ya kunywa kweli!
Nipe mchongo kaKa,Mungu akutangulie
 
Back
Top Bottom