Leo nimeondoka rasmi jijini Dar es Salaam baada ya kupata mchongo Jehanamu

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ushauri kwa vijana wote ambao hamna familia, ukipata kazi kama hizi sehemu ambazo ni changamoto, jitahidi sana kuishi kwa malengo.

Jipe mwenyewe time frame kwamba nitafanya kazi hapa kwa miaka mitatu lazima niwe nimepata ramani nyingine, cha muhimu tunza pesa, usifuate starehe za Mkumbo kijijini uzinzi na pombe kupitiliza.

Jaribu kuangalia mazao ya kibiashara sehemu husika yanayostawi vizuri basi kwa kutumia pesa hiyohiyo unayolipwa unaweza ukaanza kukodi mashamba na kulimisha kisasa kwa kufuata kanuni zote za kilimo, usishangae baada ya miaka miwili ukafikia maamuzi ya kuwa mkazi wa kudumu na kuanza kuplan kujenga nyumba ya kuishi na kupanuwa vitega uchumi.

Mimi natembea sana vijijini naandika na kutowa ushauri sahihi.

Kwa vijana bila kuwapa muongozo huwa hawaelewi, kuna vijana huwa napiga nao story chimbo fulani hivi vijijinini madreva wa truck kubwa, wanalipwa 20,000/= kwa tripu, kwa siku trip 3 jumla 60,000/= mwisho wa mwezi Boss wao anawalipa 300,000/= mshahara.

Sasa hapa vijana hii 60,000/= wanalaka guest 10,000/= per night badala ya kupanga chumba 30,000/= per month.

Atakula migahawani 10,000/= au zaidi, kuna pombe na umalaya hiyo posho ya 60 per day haionekani inakwenda wapi na anaendelea kulalamika maslahi madogo.

Kwahiyo kikubwa kwenye maisha ni hesabu tu ndio kila kitu, nidhamu ya matumizi.
 
ahsante sana kwa ushauri wako mkuu
 
hakika nimeupokea ushauri wako
 
Mishahara itakutana kama huna familia, kuna unayo familia bill za Mangi zinakufuata hukohuko kijijini.

Ni hatari sana kwa mtu mwenyewe familia Dar halafu kazi kijijini, Kipato inabidi ukigawe Mara mbili, hii inawalipa wenye mishahara mikubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…