Leo nimepotea Buguruni mjini "Dalisalama"

Leo nimepotea Buguruni mjini "Dalisalama"

b5e86e46c04b95a8dc5cef00a7eb9bfd.jpg

Hivi ile SEWA BAR bado ipo
 
Si mbaya umefanya utalii wa ndani na umejifunza njia mbadala...siku nyingine unaweza kupita njia hiyo ukiwa na gari kukwepa foleni.
 
Si mbaya umefanya utalii wa ndani na umejifunza njia mbadala...siku nyingine unaweza kupita njia hiyo ukiwa na gari kukwepa foleni.
Unaweza tokea kwenye ghetto la mtu na ukajikuta unakosa ata sehemu ya kugeuzia gari.......!
 
hahaha ukibuni unatokelezea tu ilabora ungesema kulikuwa na mchepuko mana hili jukwaasio la kupotea
 
Mkuu nilishituka mapema sana kwamba nimeshaingia cha kike, tatizo ni pale nilipoanza kutafuta ufumbuzi wa tatizo ndipo nilipopotea zaidi!!
Mkuu umenichekesha sana. Hii ndiyo Darisalama yetu GPS ni akili mukichwa. Pole sana Mkuu
 
Ungeuliza tu maana kuuliza sio ujinga na watanzania ni wakarimu sana wangekupeleka hadi sokoni
 
Au ulikuwa unatKA upate mambo yetu kwenye chocholo ndefu za wahaya ndio maana hukukata tamaa. Pole hiyo ndiyo dar salama
 
Au ulikuwa unatKA upate mambo yetu kwenye chocholo ndefu za wahaya ndio maana hukukata tamaa. Pole hiyo ndiyo dar salama
Hapana mkuu nilitaka kwenda kununua nyanya na vitunguu tu bana.
 
Sikuwahi kudhani kama naweza potea kizembezembe hivi kama leo.

Nilitokea mitaa ya Tazara na shida ilikua nifike Sokoni Buguruni ili kununua mazagazaga ya nyumbani, kwasababu ya foleni nikaamua kupiga teke tu.

Nilipofika pale kwa wauza mbao nikaamua kula 'chocho' upande wa kulia ili nitokee Sokoni.

Kiukweli nimejikuta nipo Malapa tena ni baada ya kuhangaika sana kuitafuta barabara ya Uhuru ili nisome ramani upya. Ilifikia wakati nikataka kuchukua pikpiki but nikasita maana pengine nipo sokoni tayari but ni kutafuta tu kaupenyo. Kwenye picha nimeweka mitaa ambayo nimeisaganya leo kwa masaa mawili!
Ubahili mwingine bana 😀
Siku nyingine tumia GOOGLE MAP
 
Back
Top Bottom