Dunani huwezi kujua kila kitu, leo nimeshangaa kugundua kwamba mwanzilishi wa Kampuni ya Apple yaani Steve Jobs alikuwa Mwarabu wa Syria na baba yake alikuwa anaitwa Abdul Fattah Jandali ila alilelewa na wazazi ambao sio wake ambaye ni Paul jobs na mkewe.
Ila cha ajabu alikuwa akipenda sana kwenda kula restaurant ya Fattah bila ya kujua ndio biological father wake, hadi anakufa aliweza kuungana na mama yake mzazi na dada yake ila baba yake hakutaka kujishusha aliona akimfuata ataonekana kama kafuata hela.