Leo nimeshuhudia Umahiri, unyenyekevu, na uchapakazi wa Waziri Dr. Dorothy Gwajima Mubashara yaani ana kwa ana

Leo nimeshuhudia Umahiri, unyenyekevu, na uchapakazi wa Waziri Dr. Dorothy Gwajima Mubashara yaani ana kwa ana

Samahani mtoa mada, kuitikia salamu yako kama mama wa uswahilini ndio uchapa kazi? I mean ndio kigezo hicho

Sikatai mama Gwajima kuwa mchapa kazi ila mkuu ungeishia kusema ni humble
Sawa aliitika in just humble ways yaani hakuwa Ktk standard yoyote. That was my meaning.
 
Sijawahi kupost Uzi wa maua Kwa yeyote ninaomba kutokana na kokosa kifaa Cha kupiga Picha au video jongefu isiwe sababu ya kuona nimetunga. Wala sitafuti chochote Kwa mtu. Ila Kwa vile sifa zake nimewah zisoma hapa wakati Fulani wakuu wakiwa wanawajibu Taasisi Fulani kufuatia mfano wa Waziri Gwajima.
Tuchukue na ushahidi wa waliosema aliwakuta wamekaa akawatania na kuwatani. Asanteni
 
Kama alikuwa anatembea bila guard umetupiga
Utajuaje kama walikuwa kule kando ya barabara? Ile barabara ilikuwa na watu wengi na Mimi nilikutana nae ghafla na nilipomsalimia akajibu nilipita Wala sikugeuka nyuma kuangalia yuko na nani. Labda huyo aliyesema alikuwa na mumewe akawatania alikuwa na nani?
 
Kuna sehemu alitukuta tumekaa na mshikaji wangu, alikuwa na mumewe akaja mpaka pale akatutania,mbona mnaangalia sana hiyo iPad,vijana msije kuwa mnaangalia Pilau,tukacheka pale na story mbili tatu, kusema kweli yule mama na kazi yake ya ustawi wa jamii inamfaa sana.

Hata ukiangalia namna anavyojibu comments mitandaoni,hajali ni nani ameibua jambo,hata wale wakosoaji wakubwa wa serikali kama kina Boni Yai,anajibu na anafanyia kazi na mrejesho analeta.
Mtampoza na hizo sifa. Top in town apendi kufunikwa. Yasije kua kama ya Jerry alipokua ardhi
 
Samahani mtoa mada, kuitikia salamu yako kama mama wa uswahilini ndio uchapa kazi? I mean ndio kigezo hicho

Sikatai mama Gwajima kuwa mchapa kazi ila mkuu ungeishia kusema ni humble
Huko kuitikia ka mama wa uswahili ikoje sijui!?
 
Ni mtu ambae kila anayekutana nae kwenye jukwaa lolote haachi kumzunguzia kwa jema na wema , la kama sio kila sifa njema anapewa rais basi huyu waziri angesifiwa sana
 
Sidhani kama kuna jipya hapo. Ni siku za hivi karibuni tu viongozi wamegeuka miunguwatu. kuna mzee mmoja kiongozi zamani sana alikuwa anakatiza mitaa ya Posta hapo anatafuna zake vipande vya mihogo. Ukimuuliza anakwambia hivyo vyakula vya asili ndivyo vilivyomkuza.
 
Sijawahi kuwa shabiki ya wanasiasa na kipindi cha Magu na kupiga nyungu nilimnanga sana Waziri Gwajima.

Ila ukimlinganisha na mawaziri wengine kwa sasa, Dr. Gwajima ndie waziri interactive kuliko yeyote yule.
Ni approachable na ana hands on approach.
 
Back
Top Bottom