Leo, nimethibitisha kwamba Zanzibar ni nchi inayojitegemea

Kaka,

Kuna Id ya NIDA Kama kitambulisho hard copy na Kuna namba za Nida,zote zinasolve matatizo,

Dar walikataa Namba ya NIDA, Ila zanzbar waliikubali, zanzbar walikataa Barua ya Kisutu,bara wakakubali Barua ya kisutu
Kuna tatizo hapo, labda tuseme la kiufundi zaidi ila nahisi ni la watendaji (mmoja kakataa kata kata namba ya NIDA, mwengine kaikubali, naona hapa changamoto wafanyakazi na si mfumo).


Wasalimie huko Mchambawima
 
Kuna tatizo hapo, labda tuseme la kiufundi zaidi ila nahisi ni la watendaji (mmoja kakataa kata kata namba ya NIDA, mwengine kaikubali, naona hapa changamoto wafanyakazi na si mfumo).
Wasalimie huko Mchambawima
Nipo hapa kwa Bibi ake zuchu Paje,nakula upepo mwanana kabisa
 
Sheikh / muadhham / ulaamaa
Skupingi juu ya kuongea ...juu ya maono na hisia zako hongera sana mwinyi.

Ila lait tungalijua neema ilyoko huku bara wallahi thumma wallahi ..tusinge nena hayo
Mimi nimetoka huko 2008 baada ya kumaliza skuli

Ila neema niliyoipata huku na pesa ninazo tengeneza tusiwaseme vbaya ..hawa jamaa, tusiishie dar es salaam ..tu tuje huku mbali kabisa ..ambapo ..wazanzibar tunahesabika..
Ah tunanyenyekewa na kujaliwa ...kwa kila hali na mali ..niko tarime .huku...lakin kama niko home
Maisha murua ..

Karibu sana sheikh karibu bara


Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Aha ha haaa...! Mkuu umenichekesha sana ila mwanao ana akili sana unapaswa utembee kifua mbele kujivunia huyo mtoto
 
Niliwahi kushuhudia the same scenario hapo bandarini Dar.

Mama mmoja wa Kizenj alizuiliwa na Polisi kuingia bandarini kwa kuwa hana hard copy ya NIDA, alimuonyesha NIDA aliyopiga kwenye simu yake afande amekomaa hataki, lazima atoe kitambulisho halisi au akachukua barua Mahakamani.
 
Wengine hawajahi kufika upande wa pili wa Muungano, ukichukulia wafanyakazi wa mahoteli ya Zanzíbar ,90% wanatoka Bara, ila alokuwa hajafika ataleta kelele, vijijini Bara kuna wavisiwani kibao, wanalima n.k ila wengime ndo kama hao.

Je tunashindwa na huu wa nchi mbili, tutaweza wa Afrika nzima ? Wanamajumui was kiafrika watanifahamu hapa.
 
Shukrani kwa kunihabarisha, nitajongea huko Tarime panapo majaaliwa.

Wape salam pande hizo.
 

Haina jeshi, ndiyo maana akina Maalim walishinda kesi ya uhaini miaka ya 00's mwanzoni.
 
Hizo ni sababu za kitoto tumia kuwadanganya wenzako

Hayo majitu ya visiwani ni mabaguzi hayana tofauti na shwetan

Mbona wao wakiwa wanakuja tanganyika hawapewi usumbufu km watanganyika wakiwa wanaenda uko kwenu
@Kikwajuni One kasema sahihi, kote kote unaulizwa hata ukienda tiketi ya meliupande wa zenji lazima uulizwe kitambulisho, unless uwe unapanda haya majahazi hayo ndio hamna hizo mambo.
 
Kaka,

Kuna Id ya NIDA Kama kitambulisho hard copy na Kuna namba za Nida,zote zinasolve matatizo,

Dar walikataa Namba ya NIDA, Ila zanzbar waliikubali, zanzbar walikataa Barua ya Kisutu,bara wakakubali Barua ya kisutu

Habari Kiongozi.

Bandari Dar kwa wauza ticket hawakatai namba ya Nida.

Tatizo mamlaka ya Bandari haijaweka machine ya kutambua vitambulisho hivyo basi wahudumu wanataka vitambulisho phisically ili kuthibitisha.

Ndiyo maana mara nyingi kama ikitokea situation kama hiyo watakushauri ufuate barua ya utambulisho au ukatoe maelezo mwenyewe kwa Askari wa Uhamiaji au Mamlaka ya Bandari.

Ahsante..
 
Ungewaambia huyu Rais wenu hapa ni home boy, mwiteni athibitishe kama hanijui
 
Ukimaliza hapo, nenda kajifunze muungano wa Chechnya ndani ya Urusi, Toka Tena ukajifunze Nafasi ya Buryat ndani ya Urusi.

Halafu huje hapa ukiwa na akili timamu.
 
Na sasa Ndugu yao ndiyo kaishika nchi tutegemee makubwa zaidi ya Kustaajabisha na hata Kutukwaza nayo pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…