Leo nimetimiza miaka 15 ndani ya JF

Nimebadili ID mara sita sasa ila ningekuwa mkongwe sana ikiwa ningebaki na ID ya mwanzo .

Nimezikumbuka zile nyakati ambazo kukomenti hapa jamvini ilikuwa ni lazima utafakari ni nini unataka kuandika ,je una uhakika?

Kipindi ambacho usingeweza kumbeza yeyote kwa mchango wake ,kipindi ambacho kujibizana kwa hoja na wale walioko kwenye mfumo wa serikali ilikuwa ni kawaida sana.

Kipindi ambacho haka kamtandao kaliitwa Jamboforum hakika hapa palifana sana

All in all ya kale ni dhahabu , but hongera sana ndugu Elli
 
Zilikua nyakati nzuri sana sana! Shukrani Kaka
 
Swali langu ni je, kwa hiyo miaka 15 uliyokuwemo humu JF, umeifanyia nini JF kuifanya iwe bora zaidi?
 
Swali langu ni je, kwa hiyo miaka 15 uliyokuwemo humu JF, umeifanyia nini JF kuifanya iwe bora zaidi?
Swali zuri sana. Naomba nitaje mambo mawili tu ninayokumbuka.
1. Uanzishwaji wa Jukwaa la JF photo,
2. Ku-organize na kusimamia Safari ya Wana JF kutembelea Wagonjwa pale Ocean Road Hospital.

Hili la pili ndio kubwa saaana kwangu!
 
Swali zuri sana. Naomba nitaje mambo mawili tu ninayokumbuka.
1. Uanzishwaji wa Jukwaa la JF photo,
2. Ku-organize na kusimamia Safari ya Wana JF kutembelea Wagonjwa pale Ocean Road Hospital.

Hili la pili ndio kubwa saaana kwangu!
Hongera mkuu, unastahili kusherehekea.

Ila nina swali lingine la kizushi, hapo kwenye kuratibu safari ya wana JF kutembelea wagonjwa pale Ocean road, je mlikutana? Na mkatambulishana? Manake najaribu tu kuwaza siku nakutana na mtu kama Mpwayungu village sijui itakuwaje..[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Those days hahahahaha ilikua Bomba sana saàna, baadhi tulifahamiana kama dada Asnam na wengine, tulipiga picha kabisa, tulianza kukutana pale ufukweni tukapanga mizigo yetu na tukapiga picha.

Baadae tukaenda kupata kinywaji kwa pamoja kwa hisani ya Maxence Melo . Ule Uzi siukumbuki jina
 
Unaweza kukuta Mpwayungu ni bonge la Mchungaji hahahahhah
 
Hongereni sana wakuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…