Leo nimetimiza miaka 15 ndani ya JF

Bila kuwasahau Mzee mwanakijiji na Fild Marshall aka sauti ya umeme.
 
Hongera sana kwako. Mimi ningekuwa natimiza miaka 10 mwaka huu! Sasa kwa bahati nzuri nimebadili ID mara mbili.
Wewe ndugu huwa nakufananisha na yule ndugu alikuwa anaitwa MwanaDiwani. Kama sio basi ni 'Magonjwa Mtambuka'. Japo Mwanadiwani nyuzi zake zilikuwa ndefu ila miandiko yenu ni kama inafanana vile. Ha ha haa..
 
Changamoto imejitokeza baada ya kila mtu kumiliki Smartphone huku tukiwa hatujui matumizi yake sahihi.

Zamani JF watu wengi (sio wote) walikuwa wanaingia kwa kutumia Computer, tena siyo PC, yaani Desktop kabisa..Kwahiyo unaweza ona wakati huo JF ilikuwa Platform ya watu type ipi!
 
Umezeeka hivo.
 
Pongezi sana kwako mkuu, na wale waliotangulia mbele za haki, tuendelee kuenzi michango yao ya hapa jukwaani; ''life is a process; birth to death''​
 
Wewe ndugu huwa nakufananisha na yule ndugu alikuwa anaitwa MwanaDiwani. Kama sio basi ni 'Magonjwa Mtambuka'. Japo Mwanadiwani nyuzi zake zilikuwa ndefu ila miandiko yenu ni kama inafanana vile. Ha ha haa..
Dah! Hapana mkurugenzi. Tena huyo Magonjwa Mtambuka ndiyo kabisaa!! Enzi za utawala wa Magufuli, tulikuwa tunatofautiana sana kwa hoja.
 
Sasa hv kuna bando hadi la jero 😁
 
Mkuu hongera sana.

Nasikia nyie wa mwanzo mwanzo humu mlinufaika sana kiuchumi kutokana na connections mlizozipata humu, Je kuna ukweli kuhusu hili mkuu kwa experience yako binafsi?
 

Hongera sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…