Leo nimetimiza miaka 30, sijawahi miliki hata Godoro

Leo nimetimiza miaka 30, sijawahi miliki hata Godoro

Wala haujachelewa. Kinachoogopesha wengi ni uwoga wa maisha.
Mimi baada ya kumaliza elimu yangu, sina kazi, nashinda nalala tu nyumbani.
Nilipata mpaka msongo wa mawazo. Nilichoamua, nilitoka nikaenda mkoa wa mbali na nyumbani. Na lengo langu lilikuwa ni kuishi kwenye mkoa ambao sina ndugu wala rafiki ili nisipate msaada wowote ili nipambane zaidi kutafuta pesa.

Mwanzo huwa ni mgumu, utalala njaa, utadharaulika hata mate utatemewa ila ndiyo mwanzo wa kutoboa. Baada ya kulipa nauli 20,000. Nikalala guest ya 5,000, nikalipa chumba miezi 3 (45,000). Nikabakiwa na 2, 000 (elfu mbili). Imenijenga sana kutafuta pesa. Toka hapo ulipo, nenda mkoa mbali na kwenu, hakika kichwa chako kitakuwa chepesi kutafuta pesa.
Baada ya kutimiza huu umri nimejikuta natamka maneno magumu sana education is a lottery ticket not a safe investment.
nimetafuta kazi nimekosa, nimefanya biashara nimefilisika.
so nilichobakiza ni kuwalamba wana mizinga ya ten tu ili niishi.
 
Miaka 30 ni umri mdogo sana wala hutakiwi kuteseka kwa mawazo kisa godoro tu sijui na kitanda.

Kuwa na elimu tu uliyonayo ni achievement tosha kabisa to brag about.

Cha kukusaidia tu kwa sasa hutakiwi kuwaza kwa nini huna hata godoro tu, kwanza godoro la nini wakati hata hela ya kumiliki huna, Utaliweka chini ya mti ?

Sasa hivi tumia muda mwingi namna gani utazalisha pesa au utapata chanzo cha mapato, kuwa na godoro sijui piki au whatever ni jambo la dakika tu ukiwa na pesa.

Usitafute godoro tafuta hela kwanza
 
Baada ya kutimiza huu umri nimejikuta natamka maneno magumu sana education is a lottery ticket not a safe investment.
nimetafuta kazi nimekosa, nimefanya biashara nimefilisika.
so nilichobakiza ni kuwalamba wana mizinga ya ten tu ili niishi.
Mkuu pole sana najua situation unayopitia ni ngumu sana, maisha sio straight way, kuna waliofanikiwa na miaka 20, 25, etc hadi miaka 50.......kikubwa usikate tamaa, elimu bado ni muhimu mno, muombe Mungu akufungulie ridhiki zaidi
 
Mleta mada kila mtu anakupa comment ya kukupa faraja na kukutia moyo ila kama ungeleta thd kua maisha umeyapatia na unamiliki magari ya kifahari na maisha ni mazuri basi wangekuponda na kukuona wewe ni muongo umepigika tu,

Hii ndio JF.
😀😀
 
Cha muhimu afya na chakula godoro unaweza ukatengeneza mwenyewe acha uvivu.
 
Mleta mada kila mtu anakupa comment ya kukupa faraja na kukutia moyo ila kama ungeleta thd kua maisha umeyapatia na unamiliki magari ya kifahari na maisha ni mazuri basi wangekuponda na kukuona wewe ni muongo umepigika tu,

Hii ndio JF.
[emoji3][emoji3]
Hahaaaaaa na kweli asee.
Nakumbuka jamaa aliyeeleza alivyojenga nyumba kwa miaka 5 (Ni mingi) na bado akaonekana mwongo!!!.
 
Hahaaaaaa na kweli asee.
Nakumbuka jamaa aliyeeleza alivyojenga nyumba kwa miaka 5 (Ni mingi) na bado akaonekana mwongo!!!.
Mkuu,unajua mtu aliyefeli/ambaye hawezi kufanya jambo fulani basi huamini kabisa kua na wengine hawawezi kama yeye alivyoshindwa,au hata anaweza kusema ni uongo ili japo ajifariji tu.
 
Back
Top Bottom