Leo nimetimiza miaka 30, sijawahi miliki hata Godoro

Leo nimetimiza miaka 30, sijawahi miliki hata Godoro

Kwanini usijibane hizo hela unazowapa hao wana mizinga ili ununue hilo Godoro,na vitu vingine?kaa ukijua kuwa maisha hayajawahi kuwa rahisi hivyo unavyowazia,hizo ten unazohonga ni hela ungeweza kufanyia mambo mengine ya maana na ukafanikiwa...,...
hujanisoma mkuu,wana wananiungia hizo ten sio nahonga.
 
Baada ya kutimiza huu umri nimejikuta natamka maneno magumu sana education is a lottery ticket not a safe investment.

Nimetafuta kazi nimekosa, nimefanya biashara nimefilisika.

So nilichobakiza ni kuwalamba wana mizinga ya ten tu ili niishi.
Inshort ulikuwa unamiliki group la WhatsApp tu
 
Bado una nafasi ya kupambana na kufanikisha baadhi ya malengo...Kwenye maisha kuna wakati unaweza usione mbele yako itakuaje hata kama utatumia microscope kutazama

Nyakati kama hizo zisizime ndoto zako bali ziwe za kukujenga na kukupa darasa jinsi gani maisha yalivyo...itakusaidia kama funzo huko mbeleni ..kuna wengine tuna vitanda pamoja na familia lakini hatuna uwezo wa kusurvive kila siku ila kwa sababu maisha hayana fomula tunakaza kimtindo maisha yanaendelea

Bado una nafasi kijana pambana mpaka Point ya mwisho
ngoja niishi nayo hii mkuu,kuna nyakati maisha yanakuwa na ukatili fulani ngoja nijifunze.
 
Yesu wangu mm hizo asset nimeanza kumiliki toka nikiwa na miaka 19

Sahivi nina miaka 22 ila nina kila kitu...
Baada ya kutimiza huu umri nimejikuta natamka maneno magumu sana education is a lottery ticket not a safe investment.

Nimetafuta kazi nimekosa, nimefanya biashara nimefilisika.

So nilichobakiza ni kuwalamba wana mizinga ya ten tu ili niishi.
 
Ungesema mahali unaishi watu wajue wanakusaidia vipi.

Ila kazi za mtaani unatakiwa usahau kidogo kuhusu makaratasi waliyokupa ulipomaliza skuli
nipo dar mkuu,game inakuwa ngumu nawish sometimes mpira urudi kwa kipa.
 
Baada ya kutimiza huu umri nimejikuta natamka maneno magumu sana education is a lottery ticket not a safe investment.

Nimetafuta kazi nimekosa, nimefanya biashara nimefilisika.

So nilichobakiza ni kuwalamba wana mizinga ya ten tu ili niishi.
vip ulikuwa kwenye kundi la mitano tena au mitano kwanza
 
Wala haujachelewa. Kinachoogopesha wengi ni uwoga wa maisha.
Mimi baada ya kumaliza elimu yangu, sina kazi, nashinda nalala tu nyumbani.
Nilipata mpaka msongo wa mawazo. Nilichoamua, nilitoka nikaenda mkoa wa mbali na nyumbani. Na lengo langu lilikuwa ni kuishi kwenye mkoa ambao sina ndugu wala rafiki ili nisipate msaada wowote ili nipambane zaidi kutafuta pesa.

Mwanzo huwa ni mgumu, utalala njaa, utadharaulika hata mate utatemewa ila ndiyo mwanzo wa kutoboa. Baada ya kulipa nauli 20,000. Nikalala guest ya 5,000, nikalipa chumba miezi 3 (45,000). Nikabakiwa na 2, 000 (elfu mbili). Imenijenga sana kutafuta pesa. Toka hapo ulipo, nenda mkoa mbali na kwenu, hakika kichwa chako kitakuwa chepesi kutafuta pesa.
nitajaribu hii risk, may be italipa.
 
Back
Top Bottom