Wakuu,
Leo kuna binti kanifuata akasema ana jambo lake anataka kuzungumza na mimi.
Kwakua mimi huwa natoa ushauri wa kisheria basi nikajua nimepata mteja. Nikamwambia sawa ngoja nimalize shughuli tuzungumze. Sasa ananiambia kuwa ananipenda mno.
Na anataka nimpe jibu kama nimemkubali au la. Wakuu ndio kwanza nimepata katoto kadogo kana mapengo tu hata kuzungumza bado hakajui. Huyu naye ananiletea hadithi zake za mapenzi hapa naona ananichanganya tu.
Najua nikimkubalia nitaongeza mchepuko halafu niwe nalea mwanangu,mama yake,mimi, mchepuko namba moja ,mchepuko namba mbili na yeye pia.
Familia yangu itakua kubwa sana.