CCM Music
JF-Expert Member
- Dec 5, 2018
- 1,036
- 1,784
Ndugu watanzania!
Leo naandika hili na leo ndio mwisho wangu kuandika hapa JF, sio kwa ubaya bali kwa ridhaa yangu mwenyewe.
Kuna mambo matatu makubwa:
1. Ukiona matatizo yoyote yaliyopo TANZANIA fahamu kuwa huo ni mradi wa watu wakubwa wachache. Mfano: Ukiona urasimu, ukiona maisha duni ya watanzania na mengine mengi nikiorodhesha hayaishi fahamu kuwa ni miradi ya watu. Kwa maneno mengine kuna watu wametaka kwa makusudi iwe hivyo. Na hata ajaribuye kutatua hilo yatamfika ya kumfika, hili ni moja!
2. Sitaki kuwakatisha tamaa, lkn nawaambia ukweli tupu. Tanzania kuna wapinzani wa kweli kwenye vyama vyao, lkn wengi wao wanatumia upinzania kama ngazi ya kuingilia CCM ulaji. Na hii ni kutokana na ukweli kuwa CCM ni msitu mnene wa watu wanaowinda maslahi yao iwe kiserikali, kifedha ama kichawi. Sasa wale wanaoshindwa kupambana na watabe kwenye game la ndani ya CCM huchagua upinzani km route yao ya kuingilia ndani ya CCM na hatimaye kuwaacha wafuasi wao midomo wazi. Wapinzani chukueni tahadhari mifano ya hili ni mingi mno! Hili ni la pili!
Tatu na mwisho kabisa, watanzania kwa ujumla wao ni binadamu wa aina yake. Wala hawana habari na Nchi yao kiviiiiiiiile, na ukijaribu kuwapigania wanaweza kukuchamba hadi ukazimia na usiwaelewe na wala wao wenyewe wasikuelewe yaani wakakuona hujielewi to the core. Kwa ujumla nasema 'Ufahamu' wa watanzania upo somewhere else may be no one knows! Hahahahaha....!
CCM Music!