Leo rasmi nawasanua watanzania. Tupo wachache sana tunaofahamu hili jambo

Nakubaliana na wewe kwenye sehem ya 3, mfano halisi ni Edo, upinzani ulitumia miaka zaidi ya 7 kuelezea ufisadi na uchafu alionao na watanzania wakaelewa na upinzani huo huo ulipobadiri gia angani watanzania wale wale walianza kumsifia Edo.

Watanzania wale waliokuwa wanamsapoti Magufuli waulize leo wanasemaje.

Watanzania wale waliokuwa wanasema mama anaupiga mwingi waulize tena leo.
 
Na ww ni mmojawapo wa hao watanzania wasiojua nin kinaendelea,unakutana na mtu unamwambia kuna umuhimu watanzania kupata KATIBA MPYA anakujibu simple tuu katiba mpya ya kazi gani kisa tuu amejificha kwenye Chaka la ccm
 
[emoji706][emoji706][emoji706]halafu ukitulia ukakalie hichi [emoji867]
 
Daa Nyerere simlaumu ila alikosea mno mno kutunyima elimu ya Uraia aic pamoja na elimu ya kawaida.
Badala ya kumlaumu unapaswa kumpongeza maana hata hicho kiwango kidogo cha elimu ulichonacho ni mipango yake. Wakoloni hawakuwa na mpango wowote wa kutusomeshea watoto wetu, wao walisomesha wachache ili wapate watumishi tu, Nyerere akasema tujibanebane ili watoto wote waende shule, matokeo yake leo tuna maDr Mabuga wanaotumia alichowapa Nyerere kumponda!
 
"Yaani wakakuchamba na ukazimia hadi ukawa hujielewi, na wao wakawa hawakuelewi, wanakuona hujielewi maana hata wao hawajielewi?!"

Mimi naona mleta mada ndio hujielewi!
 
Tunaambiwa 80% ya watanzania ni wakulima. Carl Marx alisema akili ya mkulima ni sawa na gunia la nafaka, litaendelea kubaki hapohapo Hadi mtu alihamishe, lenyewe haliwezi kuhama. Wakulima hawawezi kufanya mabadiliko yoyote,

Maisha wanayoishi wanaona ni haki Yao, Wala sio jukumu la serikali kubalisha Maisha Yao, kiufupi hakuna uhusiano Kati ya serikali na Maisha Yao, kwanza wanajiona hawana tatizo lolote hata Kama yupo nyumba ya nyasi!!!

Mtu aneilaumu serikali kwa sababu ya uduni wa Maisha wanamwona ni kichaa, kujaribu kumtetea mkulima ni kutafuta matatizo yasio na sababu. Carl Marx alishauli njia moja tu....Revolution
 
Nakusikitikia kwa kuchelewa kulijua hilo. Wkt ww ndio unafaham leo kuna wengine walishajua kitambo na wakawa wanalipigia kelele.
 
Eh we ndiyo umegundua leo!

Mtaji wa wanasiasa ni umaskini+shida

Sasa nkikuwekea mazingira bora kesho ntarudi

Na gia gani??

Ova
 
Yani mtu anakuwa ameshaona ni mahala gani pakuiba ndipo anachukua form ya kugombea .Africa na Tanzania hasa ni shiiiiida
 
Ndio maana inaitwa saccos😅
 
Ha ha ha nimecheka kwa nguvu jirani yangu kaniuliza vipi, nikamuambia kuna mwamba yamemkuta huku, nadhani umeijua Tanzania hivi karibuni au ulikuwa unajua lakini ulikuwa huamini kile kinaendelea “ KILA MBUZI ALE KWA UREFU WA KAMBA YAKE”
Tuitafune hii nchi kwa kasi
 
Nakuonea huruma kuchelewa kujua haya mambo, mm nimeyajua haya toka nipo O level
 
Kwa kifupi iko hivi: wengi zaidi ya 70 % hawajui kinachoendelea katika nchi yao wala hawajali mradi wameshiba kidogo. Wenye uelewa ni wachache wanaweza wasizidi 15% kwa makadirio, lakini kati ya hao wenye uelewa majority of them wanatumia uelewa wao kujinufaisha binafsi huku wakiwahadaa wananchi kuwa wanapigania maslahi yao; wachache kabisa kati ya wale wachache wenye uelewa ndio wanapigania maslahi ya kweli ya wananchi lakini hawaeleweki wala kukubalika na wananchi. Wanaoaminika ni wale wachache wenye uelewa lakini wanatumia uelewa huo kujinufaisha binafsi. Na hao matapeli wako katika vyama vyote.
 
Kuna haja ya kuunda kikundi huru (sio cha kigaidi au kiuhaini) kitakachokuwa mstari wa mbele kupigania masilahi mapana ya nchi.

Kuamsha jaramba kali na la nguvu juu ya "HAKI NA UTU WA MTANZANIA" maana pasipo mebweko yenye nguvu na ya kutisha kuna watu wanahisi hii nchi ni mali yao binafsi.

Haiwezekani mtu from nowhere ajisemee tu, 'CCM ina wenyewe" ikiwa CCM ina wenye basi ujue nchi pia ina wenyewe.

Angalizo: Serikali nyingi duniani hasa katika mataifa ambayo madaraka yamekuwa chini ya chama kimoja kwa muda mrefu au kuna strong institutions kwa maana ya mihimili mikuu, basi nchi hizo huendeshwa na 'deep state' iliyojichimbia kwa muda mrefu. Hivyo, inahitajika nguvu ya ziada kung'oa mifumo mibovu na onevu kwa watu wa kawaida walioko nje ya mfumo.
 
Umeeleweka Mkuu sikuwa na nia mbaya kwa Baba wa taifa, Samahani kama umekwazika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…