Ulikuwa na dalili zipi zilizokufanya mpaka uende kupima pressure? Si nilisikia ukishaanza dawa ndio hauwezi kuacha? Wanasema kwamba ukiwa na pressure au kisukari mtalimbo unakuwa dolo?
Msingi wa kutokusitisha dawa kwenye presha si kwa sababu umezianza bali ni kwa sababu ni ugonjwa wa kudumu.
Kwa wachache ambao presha yao huwa haijawa kubwa sana huweza kurudi sawa kwa kurekebisha mtizamo na utaratibu mzima wa kimaisha, mambo hayo huusisha:
1: kupunguza uzito uliopindukia na kurudi sawa
2: kupunguza sana matumizi ya chumvi
3: kupunguza matumizi ya mafuta ya kuunga na yale yatokanayo na nyama.
4: kufanya mazoezi/aerobic
5: kusitisha uvutaji sigara
6: kupunguza matumizi ya pombe
7: kupunguza matumizi ya vyakula vya wanga
8: Matumizi mazuri ya vyakula vyenye asili ya protini, mboga za majani, matunda na samaki.
9: kontrol nzuri ya sukari pamoja na cholesterol.
10: matumizi mazuri ya kahawa
NB: Haya pia hutakiwa kuwa sehemu kuu ya maisha yako kwa utakapozembea presha au sukari hurejea tena. Na pia huu ndo unatakiwa kwa ujumla kuwa msingi wa maisha yetu.