Ahsante kwa ushauri mzuri. Niwe mwazi kabisa. Dawa nilizoanza kutumia nimesitisha. Jana na leo sijatumia, na sababu za kusitisha ni kwamba baada ya kuanza tu kutumia, ahsubuhi yake nikaanza kusikia mwili hauna nguvu. Nikajua ni kwa kuwa nilikojoa sana usiku huo.
Ahsubuhi nikaanza kunywa maji. Nilikunywa maji lita 5. Nilikojoa sana. Jioni ile hali ya mwili kukosa nguvu niliendelea kuisikia mpaka jioni ya saa 2 usiku.
Nikanyanyua simu kuongea na dr m1 ambaye ni rafiki yangu. Akanishauri nikacheck tena, labda kipimo cha mwanzo hakikuwa sahihi. Nikaenda kupima, this ilikuwa sehemu nyingine. Kupima ikasoma 180/110 imepungua 7/5.
Nikarudi home, nikanywa dawa. Kukojoa kama kawa. Ahsubuhi ile hali ya kuishiwa nguvu nikaona kama imezidi. Nikaendele kunywa maji lita 5 nyingine. Mpaka jioni nikajiona sipo sawa tofauti na kabla ya kuanza kutumia dawa.
Kwa hiyo usiku huo sikutumia tena dawa. Nikaamka kidogo nipo poa. Jana tena sijatumia, leo nimeamka mzima kabisa.
Nimeamua kuacha dawa kwa muda na sasa nabadili staili ya vyakula.
Ni mwendo wa mbogamboga, matunda, kupunguza chumvi na mazoezi.
Leo jioni nitaenda kucheck. Nitaleta mrejesho hapa.
Ahsante.