Leo serikali na vyombo vya Dola nataka kusema nanyi hasa kuhusu suala la Utekaji

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

1. Binafsi Niko salama salimini.

2. Oooh! Robert unajua unazungumzia nini? Unaushahidi wa unachozungumza?

3. Sikiliza. Moja ya mambo yaliyotufikisha hapa tulipo nje ya madai mengine ya Haki(zingine) ni suala la Utekaji.

4. Nilisema, utekaji sio mbinu bora ya kushughulikia matatizo ndani ya taifa letu.

5. Utekaji ni kama kuita nzi ukiwa unapita na mnofu wa nyama. Nitaeleza.

6. Hii nchi sio Kila mtu ni mwanasiasa au anafuatilia siasa. Sio kila mtu.

7. Siasa wengi hufuatilia nyakati za Kampeni za Uchaguzi nje ya hapo asilimia kubwa ya Watanzania hawafuatilii siasa.

8. Lakini unapoanza kuteka WATU au panapoanza masuala ya Utekaji unafanya hata wasiohusika na siasa waanze kufuatilia wajue kulikoni nini kinaendelea huko siasani.

9. Kumteka Mtu ni kumfanya aeleweke kwa urahisi na madai Yake aliyoyalalamikia yaanze kuangaliwa kwa jicho la mwewe.

10. Nikupe Mfano Rahisi; Taikon labda ni CHADEMA au tufanye mwanaharakati. Anakimbizana Kila Siku na serikali au viongozi wa serikali katika kupigia kelele Jambo Fulani.

11. Ndugu zake Taikon labda sio wanasiasa au wanaharakati, wapo watumishi serikalini, wapo wajairiamali, wapo makundi yote. Wao sio wanasiasa na hawako interested na siasa.

12. Lakini ndugu yao ni mwanasiasa au mwanaharakati. Wanajua hilo. Wanaona ndio maisha aliyoyachagua kama wao walivyochagua kazi wanazofanya.

13. Ikitokea Taikon ametekwa au kapotea. Hapo ndugu, jamaa na marafiki na wale wapenda haki lakini hawapo kwenye siasa lazima wawe interested kujua nini kinaendelea, kwa nini huyu mtu atekwe, apotezwe au kuuawa.

14. Hivyo aliyetekwa ni mmoja lakini tukio hilo linaibua watu wengine wanaojiingiza kwenye alichokuwa anafanya Taikon kwaajili ya kutafuta Haki ya Taikon.

15. Mbinu ya kuteka watu haiwezi kufanya KAZI kamwe zaidi inapanua ufa na kuhatarisha usalama wa Jamii na nchi kwa ujumla.

16. Michezo ya siasa inajulikana, kama kuundiana scandal, kupeana makesi ya hovyohovyo, ku- blackmail n.k. hiyo ndio michezo ya siasa ambayo duniani kote IPO. Lakini sio kutekana na kupotezana hasa kwa kizazi hiki

17. Binafsi naamini kabisa kwenye huu ulimwengu hakuna ambaye Hana hatia. Kila mtu kwa Siku lazima avunje sheria Fulani. Hilo ni uhakika.

18. Binafsi naamini kabisa Kila mtu kuna Sheria Fulani mtu anaivunja na inamnufaisha. Hilo ninauhakika nalo.

19. Mbinu ya kutekana ni mbinu ya watu walioshindwa kufanya siasa. Wakaamua kucheza michezo ya kigensta.

20. Lakini ni kiashiria cha uvivu wa wanausalama kushughulikia mambo madogo.

21. Askari mvivu au ukiwa na vyombo vya usalama vyenye uvivu vinaona kazi kuanza kusumbuana na watu kwa hiyo wanatumia shortcut ambayo ni hatari Sana.

22. Vijana wanatukana hovyohovyo huko mtandaoni badala ya kutekwa. Wachukuliwe wakafanye usafi kwenye majengo ya serikali. Wakasafishe Miji. Kwanza hiyo Dar yenyewe ni chafu inanuka. Wakazibue mitaro iliyoziba.

23. Wakapande miti na kuimwagilia pembezoni mwa barabara. Serikali si haina pesa ya kuajiri watu wa kupanda miti na kuitunza. Itumie hao vijana wakiwakuta wanamakosa.

24. Kama ishu ni Sheria ziundwe sheria au ziongezewe.

25. Mimi Nina programu ya Greenroad yaani Barabara ya kijani. Ambayo inalenga kuhakikisha Barabara zote za Jiji la Dar zinakuwa miti au bustani nzuri. Hao vijana waleteni huku wanisaidie KAZI.

26. Huo ni mfano mmoja kati ya mingi. Sasa mtoto wa watu kusema hakutaki au akikutukana hata kama matusi ya nguoni hakuna haja ya kumpoteza. Mchukulie kama mwanao.

27. Ndugu zangu, watu Wana background tofauti, watu wamepitia mengi, usiseme mtoto Hana adabu, au mtoto anamtukana mtu kama Rais wa nchi Hana Adabu. Sijui anamkosea Rais. Basi taasisi ya Urais na usalama wa taifa wote mnamtolea macho mtoto WA watu.

28. KAZI ya ustawi WA jamii ni nini? Kazi ya Wanasaikolojia na sosholojia ni nini? Si wamejaa mitaani hawana KAZI. Wapeni KAZI.

29. Vijana Wana background tofauti. Wengine background ngumu jamani!
Wengine wamekulia bila malezi ya Wazazi.
Wengine Baba zao wamewakimbia.
Jamani! Jamani!
Wengine wamekuzwa na Bibi zao katika mazingira magumu.

30. Vijana wengine wamelelewa na single mother waliohangaika kwa namna halali na haramu kuwakuza katika mazingira magumu.

31. Wengine wamejikuza wenyewe! Wakati nipo Kidato cha Tano kule Matema Beach Kyela alikuwepo kijana aitwaye Gidos. Huyu jamaa alikuwa anajisomesha, anaroka saa tisa anaenda Ziwa NYASA kuchukua Dagaa anapeleka kyela mjini kuna mtu anampelekea. Anarudi shuleni anaendelea na masomo. Niliwahi kukaa naye anasema amejikuza mwenyewe kimazabe zabe. Huyu hawezi kuwa Sawa na mimi au wewe tuliokuwa tunategemea vitu kwa wazazi na walezi wetu.

32. Nyie wanausalama, washauri wa viongozi mnapofanya mambo yaangalieni kwa upande wake. Wachukulieni watu kama watoto au wazazi wenu. Waeleweni watu.

33. Haya vijana wengine background yao ya malezi imewafanya wawe na afya ya akili. Unawateka na kuwaua au kuwapoteza hiyo sio HAKI.

34. Tena hawa Gen Z ambao wanakulia kwenye familia zisizo na Baba na Mama mambo yatazidi kuwa mabaya.

35. Watu wameathirika kisaikolojia badala wapewe dawa ninyi mnawateka na kuwapoteza. Really? Hamjui tatizo. Hamlioni tatizo.

36. Lazima tujiulize mtu anapotukana au kuleta fujo mtaani au mtandaoni kiini cha tatizo ni kipi? Ili tatizo hilo liondolewe.
Na sio kuwateka. Huko ni kuongeza matatizo kwenye jamii.

37. Kwani KAZI ya maprofesa na wasomi ni ipi? Wafanye tafiti wajue tatizo nini?
Sisi watibeli hatunaga haja ya kufanya tafiti kwani mambo mengine yapo wazi.

38. Kiongozi wa serikali labda ni Rais, au mkuu wa majeshi au Polisi. Unatoa amri au oda. Wazazi wakanye watoto wenu.

39. Hao vijana Wana wazazi? Au Wana walezi? Kama wanao je Wana mahusiano gani na watoto wao?

40. Mtoto katelekezwa na Wazazi tangu akiwa Mdogo. Au wazazi wake walikuwa wanamfanyia ukatili tangu huko. Achaneni na hadithi za kizamani kuwa mzazi anapenda mtoto. Nope! Wapo watoto wakiambiwa waeleze mambo hapa utakimbia. Sisemi ni wore.

41. Kijana amekua kwa Mungu hapaelewi kwani pia hakufunzwa vizuri. Tegemeo lake ni SERIKALI. Huko serikalini nako anaona mauza uza. Wengine wanajiingiza kwenye madawa, wengine kwenye harakati kuikosoa serikali wakitegemea mabadiliko. Namna ha kukosoa itategemeana na background ya kijana. So kumhukumu Kwa kumteka sio kumtendea Haki. Ni ukatili.

42. Vijana wanataka kusikilizwa. Vijana hawajawahi kusikilizwa tangu wakiwa watoto. Wana sumu.

43. Serikali lazima ijali watu wake na kuelewa kiini cha matatizo yao.
Mimi kama mwanasosholojia na saikolojia kiini cha yote haya kimeanzia mbali. Ngazi ya familia, malezi na makuzi ya mtoto.

44. Sheria za familia lazima ziboreshwe. Kuzaa na kupachikana mimba, kupeana talaka ziangaliwe kwa umakini na watu wenye macho matatu.

45. Sasa vibinti vinapewa mimba, vinatelekezwa, vitoto vinaishi kiholela, vinapitia maisha magumu kuishi bila wazazi. Baadaye vinakuwa haviambiliki kwa sababi havikukuta huo mfumo Bora wa kuambiwa.
Sasa kama wazazi hawakuambilika wakazaa, wakatelekezana, walishindwa kukaambia kakiwa katoto Leo utakaambia nini kamekua kakubwa?
Si ndio hapa wanaitwa hawana adabu. Kama wazazi hawakuwa na adabu utegemee mtoto awe na adabu? Thubutu yake. Huo ni muujiza.

46. Sasa Mimi Nina maneno mengi. Hapa tutakesha.

47. Najaribu kusema, Serikali ipige marufuku Suala la utekaji. Hiyo mbinu haifanyi KAZI. Na kamwe haitoweza kufanya Kazi zaidi inaongeza uhasama katika taifa na kuhatarisha Amani ya nchi yeti.

48. Mbinu za kudili na kesi hizo kwa miaka 50 ijayo ni kudili na Saikolojia, sosholojia, uchumi, na wataalamu wa Sheria kuhakikisha Sheria za Haki na upendo kwa Kila mmoja wetu.

49. Mimi ni Yule mtibeli kutoka nyota ya Tibeli.

Acha nipumzike. Kesho panapo majaliwa tutajadili mada ya Disemba 9

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Serikali na Vyombo vya dola

20251118_180307.jpg

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Leo umejiondoa kwenye genista ya 'sioni watu barabarani wakuandamana' sawa sawa, hiyo ndiyo unatakiwa kuandika na siyo ile bwana mdogo.
 
1.Nashauri pia njia tunayotumia kupata viongozi wetu kwa kila ngazi ipitiwe upya,hapa kuna tatizo kubwa sana haswa hawa viongozi wa kisiasa,kuanzia wabunge mpaka raisi,haswa wabunge maana ndo kutoka kwenye hilo kundi wanajitokeza maraisi na wenyeviti wa vyama vya siasa.
2.Kila siku zinavyokwenda naona level ya weredi wa maraisi tuwapatao inashuka sana.Unabaki unajiuliza huyu alifikaje kwenye hiyo level,but unajijibu ninkutoka kwenye kundi la hawa wabunge tunaowachagua
3.Ukimsikiliza mzee Warioba,Mzee Chande kisha ukija kumsikiliza Samia unasema hapa kuna tatizo,kwa nini huyu Chande au anayelingana kidogo na uwezo wa Chande au Warioba hajawa Raisi bali Samia ndo kawa Raisi,unakosa jibu
4.Ukiangalia uwezo wa mawaziri wa sasa na baraza la mawaziri la mzee Mkapa unasema kama taifa tunazidi kuporomoka
5.Chukua Foreign Minister wa DRC yule mwana dada linganisha na Mombo au mchukue yule Foreign Minister wa Rwanda kisha mlinganishe na Makamba au Mombo utaona jinsi taifa lilivyo jeupe.
6.Swali ni tulifikaje hapa?
 
Maneno 6,0000.

Point ZERO.
 
Leo umejiondoa kwenye genista ya 'sioni watu barabarani wakuandamana' sawa sawa, hiyo ndiyo unatakiwa kuandika na siyo ile bwana mdogo.

Mkuu Mimi nazungumza mambo kwa uhalisia.. Kila kitu nikiandika nazingatia ukweli. Hiyo Siku ya 29 mpaka saa 3:30 barabara zilikuwa nyeupe na kimya
 
Vijana wanatukana hovyohovyo huko mtandaoni badala ya kutekwa. Wachukuliwe wakafanye usafi kwenye majengo ya serikali.

Vijana Wana background tofauti. Wengine background ngumu jamani!
Wengine wamekulia bila malezi ya Wazazi.

vitoto vinaishi kiholela, vinapitia maisha magumu kuishi bila wazazi. Baadaye vinakuwa haviambiliki kwa sababi havikukuta huo mfumo Bora wa kuambiwa.
Bado unalaumu vijana na mabinti bila kuAdress malalamiko yao kwasababu ya uchawa ni aibu.
 
1.Nashauri pia njia tunayotumia kupata viongozi wetu kwa kila ngazi ipitiwe upya,hapa kuna tatizo kubwa sana haswa hawa viongozi wa kisiasa,kuanzia wabunge mpaka raisi,haswa wabunge maana ndo kutoka kwenye hilo kundi wanajitokeza maraisi na wenyeviti wa vyama vya siasa.
2.Kila siku zinavyokwenda naona level ya weredi wa maraisi tuwapatao inashuka sana.Unabaki unajiuliza huyu alifikaje kwenye hiyo level,but unajijibu ninkutoka kwenye kundi la hawa wabunge tunaowachagua
3.Ukimsikiliza mzee Warioba,Mzee Chande kisha ukija kumsikiliza Samia unasema hapa kuna tatizo,kwa nini huyu Chande au anayelingana kidogo na uwezo wa Chande au Warioba hajawa Raisi bali Samia ndo kawa Raisi,unakosa jibu
4.Ukiangalia uwezo wa mawaziri wa sasa na baraza la mawaziri la mzee Mkapa unasema kama taifa tunazidi kuporomoka
5.Chukua Foreign Minister wa DRC yule mwana dada linganisha na Mombo au mchukue yule Foreign Minister wa Rwanda kisha mlinganishe na Makamba au Mombo utaona jinsi taifa lilivyo jeupe.
6.Swali ni tulifikaje hapa?
Kwani CCM si kulikua na chuo cha uongozi??
 
Back
Top Bottom