WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 1.
KESI IMEANZA
Majaji wapo tayari Mahakamani. Mawakili wa Serikali wapo tayari. Mshtakiwa Tundu Antipas Lissu yupo tayari na ameingia pamoja na Majaji, ili kuepuka kupata muda wa kuzungumza na audience.
Shahidi John Heche yupo tayari.
Saa 9:49 asubuhi
Karani wa Mahakama anajiandaa kusoma kesi ya Criminal Session, Kesi Na. 19605 ya Mwaka 2025, Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.
Wakili wa Serikali Mkuu, Ajuaye Zegeli, anawatambulisha mawakili wenzake:
1. Nassoro Katuga β Wakili wa Serikali Mkuu
2. Tawabu Issa β Wakili Mwandamizi
3. Job Mrema β Wakili wa Serikali Mkuu
4. Cuthbert Mbilinyi β Wakili wa Serikali
5. Ignas Mwinuka β Wakili wa Serikali Mkuu
6. Waniwa Kasara β Wakili wa Serikali
Ajuaye Zegeli: Kwa pamoja tunawakilisha Jamhuri.
Mshtakiwa Tundu Antipas Lissu yupo kizimbani na anajiwasilisha mwenyewe.
Shauri limekuja kwa ajili ya utetezi. Tupo tayari kuendelea na shahidi kwa maswali ya dodoso.
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, upo tayari?
Lissu: Nipo tayari, tuendelee.
Jaji Ndunguru: Shahidi, upo tayari?
Heche: Nipo tayari.
Jaji Ndunguru: Upande wa Jamhuri?
Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, ataanza Ignas Mwinuka.
MASWALI YA UPANDE WA JAMHURI KWA JOHN HECHE
Mwinuka: Shahidi, wewe kama mgombea umeshiriki chaguzi ngapi?
Heche: Waheshimiwa Majaji, nimeshiriki chaguzi tatu.
Mwinuka: Nitakuwa sahihi kwamba kati ya chaguzi tatu ulizoshiriki, katika mbili ulitangazwa mshindi?
Heche: Kwa mbinde, baada ya watu kuuawa.
Mwinuka: Jibu, kweli au si kweli?
Heche: Ni kweli.
Mwinuka: Nitakuwa sahihi nikisema ulizoshinda ni uchaguzi wa Udiwani mwaka 2008 na Ubunge mwaka 2015?
Mwinuka: Katika chaguzi mbili ulizoshinda, tuambie kama Polisi walishiriki kuweka kura kwenye masanduku ya kura.
Heche: Polisi hawajawahi kusaidia wapinzani, Waheshimiwa Majaji.
Mwinuka: Katika hizo chaguzi mbili ambazo Heche ulishinda, hebu tuambie kama mawakala walizuiliwa.
Heche: Mawakala wa upande upi?
Mwinuka: Mawakala wa vyama vingine walizuiliwa ili wewe ushinde?
Heche: Hapana.
Mwinuka: Umesema mwaka 2020 hukutangazwa na NEC?
Heche: Ndiyo.
Mwinuka: Unatambua kuwa matokeo yanapingwa Mahakama Kuu?
Heche: Natambua.
Mwinuka: Hebu tuambie, matokeo ya mwaka 2020 kutotangazwa kwako na NEC, kama matokeo yake ulienda kuyapinga Mahakamani?
Heche: Uchaguzi ulivurugwa nchi nzima, Waheshimiwa Majaji.
Mwinuka: Nazungumzia jimbo lako. Ulienda ku-challenge?
Heche: Siku-challenge.
Mwinuka: Hebu tuambie, ulijaza fomu? Wewe umegombea mara tatu.
Nitakuwa sahihi kwamba moja ya vigezo vya wewe kugombea ni kujaza fomu kwa usahihi?
Heche: Ni moja ya vigezo, kuna vigezo vingi.
Mwinuka: Nitakuwa sahihi nikisema ukijaza fomu kwa usahihi hadi ukaweza kuwa Mbunge...
Heche: Moja wapo ya vigezo.
Mwinuka: Ambacho wewe ulikitekeleza?
Heche: Ni sahihi.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI