Leo tarehe 15 August Wakristo Wanaadhimisha Sikukuu Ya Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria

View attachment 2718085

Ufunuo 12:1
"Kisha, ishara kubwa ikaonekana mbinguni: Mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!"

Luka 1:26
"Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, kwa msichana mmoja bikira aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu, ewe uliyejaliwa neema na Mungu! Bwana yuko nawe!” Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: Maneno hayo yanamaanisha nini? Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu. Yeye atakuwa mkubwa na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu"

Utangulizi: Tafakari ya Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria: Bikira Maria ni ishara na tumaini thabiti na ya faraja kwa taifa la Mungu linalosafiri. Tunaposherehekea Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Mama Bikira Maria, tunajifunza kuwa, Mama wa Yesu, akiwa amekwisha tukuzwa mbinguni mwili na roho, ni sura na mwanzo wa Kanisa ambalo litapata utimilifu wake katika ulimwengu ujao. Kadhalika anang’aa duniani kama alama ya hakika ya matumaini na ya faraja kwa Taifa la Mungu lililo safarini, mpaka siku ya Bwana itakapokuja (taz. 2Pet 3:10; Lumen Gentium, n. 68). Somo la kwanza: Ufunuo 11-.19; 12:1-6.10. Somo la pili: 1 Wakorinto 15:20-26. Injili: Luka 1:39-56. Karibu mpenzi msikilizaji wa Radio Vatican katika tafakari hii, leo ambapo Kanisa linaadhimisha Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Mama Bikira Maria Mtakatifu.

Tafakari: Moja ya mafundisho haya ya Kanisa ni kutoka katika somo la kwanza tulilosikia, kutoka kitabu cha Ufunuo wa Yohane 11:19; 12:1-6.10. Katika somo hili, Mababa wa Kanisa wanafundisha kuwa, kwanza somo linazungumzia mwanamke ambaye ni sura ya taifa la Mungu, ambalo ndilo Kanisa, ambapo pia Maria anawakilisha sura ya taifa la Mungu yaani Kanisa. Simulizi hili la joka linaturudisha kwenye kitabu cha Mwanza 3:15 ambapo Mungu aliweka uadui kati ya mwanamke na nyoka na kati ya uzao wa mwanamke na uzao wa nyoka ambaye ni shetani. Mwanamke aliyevikwa jua. Hii ni ishara ya kuwa mwanamke huyu amepambwa kwa neema za Mungu (salamu uliye jaa neema – salamu ya Malaika Gabrieli kwa Bikira Maria). Na mwezi chini ya miguu yake, maana yake kuwa mwanamke huyu hatapotea wala kuamgamia, bali ataishi milele. Na juu ya kichwa chake taji ya nyota 12, zinazowakilisha makabila 12 ya wana wa Israeli. Pia huwakilisha Mitume 12 ya Yesu, ikiwa na maana ya utawala wa Kanisa katika ulimwengu. Naye alikuwa na mimba akilia hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa. Hii li lugha ya picha inayoonesha mateso ya wokovu yaliyoletwa au kutimizwa na Kristo pale msalabani na hatimaye kufufuka kwa ushindi. Naye akazaa mtoto wa kiume – huyu ndiye Kristo Yesu Mkombozi wa ulimwengu, na mtoto huyu akanyakuliwa hata kwa Mungu, picha ya mateso, kifo, ufufuko na kupaa mbinguni kwa Kristo. Mwanamke akakimbilia nyikani, hii huwakilisha ukimbizi wa Wakristo wa kwanza kwa sababu ya mateso.

Tuhitimishe tafakari yetu kwa kusema kuwa tusihofu kumsifu Maria kwa sababu kila mara tunapomsifu Maria, yeye mara moja huzigeuza sifa hizo kuwa za Mungu. Ndio maana Elizabeti alipomsifu, mara moja Bikira Maria akasema “Moyo wangu wamtukuza Bwana...” Utenzi huu unaeleza hali ya kiroho ya Bikira Maria, na hakuna kitu kikubwa zaidi ya hali hii ya kiroho kwa ajili ya kutusaidia kupata uzoefu wa Fumbo la Ekaristi. Ekaristi imetolewa kwetu ili maisha yetu, kama yale ya Bikira Maria, yawe ya ukuu kabisa. Kwa maana “Mama anapoheshimiwa, Mwana hupata kujulishwa, kupendwa na kutukuzwa inavyostahili, na amri zake kushikwa, kwa kuwa katika Yeye vitu vyote viliumbwa (rej. Kol 1:15-16) na katika yeye ilimpendeza Baba wa milele utimilifu wote ukae (rej. Kol 1:19).” Tumtazame Bikira Maria, yeye anatufungulia matumaini ya wakati ujao uliojaa furaha na anatufundisha njia ya kuufikia: yaani kumpokea mwanaye kwa imani; daima tusipoteze urafiki wetu na mwanaye, bali tujiachilie ili, Mwanaye atuangazie mwanga wake na atuongoze kwa Neno lake; tumfuase mwanaye kila siku, hata nyakati ambazo tunahisi misalaba yetu kuwa mizito. Maria Sanduku la Agano Jipya aliye Mbinguni, anatuonesha kwa mwanga halisi kwamba tupo katika njia tukielekea katika nyumba yetu ya kweli, yaani ushirika wetu wa furaha na amani pamoja na Mungu. Hivyo, waamini wote wakristo wamsihi kwa nguvu Mama wa Mungu na Mama wa wanadamu, ili yeye aliyeusaidia mwanzo wa Kanisa kwa maombezi yake, pia sasa aliyetukuzwa mbinguni, juu ya Wenye heri na Malaika, awaombee kwa Mwanawe katika Ushirika wa Watakatifu wote, mpaka jamaa zote za Mataifa zilizopambwa jina la Kristo au zisizomjua bado Mwokozi wao, zikusanyike kwa furaha kuwa Taifa moja la Mungu katika amani na mapatano, kwa utukufu wa Utatu Mtakatifu sana usiogawanyika. Amina.

Tumsifu Yesu Kristu!
sema wale wa kanisa la roma ndo mungu wao wa kike
 
kwahiyo maria amekuwa pdf converter
 
Kwamba ISRAEL NI WAKATOLIKI?
Kwamba Biblia imeanzia Roma?
Kwamba Paulo, Matayo, Luka walikuwa Warumi?
Unajua waandishi wa biblia wewe bwana katekista?
Unajivunia dini na dhehebu zinazofanya ushoga na kubaka watoto?

Yesu Kristo alizungumzia dini kwa njia mbalimbali katika mafundisho yake, akisisitiza umuhimu wa uhusiano wa kweli na Mungu juu ya utekelezaji wa taratibu na mila za kidini. Yafuatayo ni baadhi ya mafundisho muhimu ya Yesu kuhusu dini:

  1. Upendo na Haki: Yesu alisisitiza upendo kwa Mungu na jirani kama amri kuu. Alisema, "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote" na "Mpende jirani yako kama nafsi yako" (Mathayo 22:37-39). Aliweka wazi kuwa amri hizi mbili zinajumlisha sheria na manabii.​
  2. Unyenyekevu na Unafiki: Yesu alikemea vikali unafiki wa viongozi wa kidini wa wakati wake, Mafarisayo na Masadukayo. Alionya dhidi ya kufanya matendo ya dini ili kuonekana na watu, akisema, "Lakini wewe utoapo sadaka, usijue mkono wako wa kushoto kile ufanyacho mkono wako wa kuume" (Mathayo 6:3).​
  3. Uhusiano na Mungu: Yesu alifundisha kuwa uhusiano wa kibinafsi na Mungu ni muhimu zaidi kuliko taratibu za kidini. Aliwaambia wanafunzi wake kuwa Mungu ni Baba mwenye upendo ambaye anataka kujenga uhusiano wa karibu na watoto wake (Mathayo 6:9-13).​
  4. Kutimiza Sheria na Manabii: Yesu alisema kuwa hakuja kuitangua sheria bali kuitimiza. Alifafanua kwamba haki ya kweli inatokana na moyo safi na siyo utekelezaji wa nje wa sheria tu (Mathayo 5:17-20).​
  5. Mambo ya Ndani na ya Nje: Yesu alifundisha umuhimu wa usafi wa moyo kuliko usafi wa nje. Aliwakemea wale waliokuwa wakijali zaidi taratibu za nje huku mioyo yao ikiwa mbali na Mungu, akisema, "Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutojizuia" (Mathayo 23:25).​
Bila wakatoliki msingepata biblia baaasi.....labda mngerudi kusoma torati,,,,ila hakuna biblia bila ukatoliki ,basi kama ndo muongozo wenu hata kama waliamua kuwapiga changa la macho wamefanikiwa
 
roma(wakatoliki) ndo waliojaribu kuipoteza bibilia,ila kwa uweza wa Mungu neno likatufikia
 
Kama wanaamini kweli ktk Kristo Yesu aliyezaliwa na Bikira Maria akawekwa kati yetu kwa umbo letu la ubinaadamu siyo vibaya nao wakaungana na Wakatoliki kuadhimisha siku hii maalumu kwa heshima kwake.

Siyo kwa ubaya lakini,otherwise kwa hekima ya mods wanaweza rekebisha heading iseme tofauti!
Usiwe mbishi. Weka wakatoliki tu usituingize wengine tusichokijua
 
Kama wanaamini kweli ktk Kristo Yesu aliyezaliwa na Bikira Maria akawekwa kati yetu kwa umbo letu la ubinaadamu siyo vibaya nao wakaungana na Wakatoliki kuadhimisha siku hii maalumu kwa heshima kwake.

Siyo kwa ubaya lakini,otherwise kwa hekima ya mods wanaweza rekebisha heading iseme tofauti!
Ingebaki tu kua Wakatoliki katika imani. Na sio Wakristo
 
Sikweli kwamba Bikira Maria Amepalizwa Mbinguni. Kupotoshwa huku ni Kutokana Na Kutokuya fahamu maandiko.

Kitabu cha Ufunuo ni kitabu cha unabii wa mambo yaliyopita Na yatakayokuja ina hitaji Ufunuo kuyafumbua mafumbo ya Mungu kwenye kitabu hiki.

Ufunuo 12:
Imeshapita ilikua inazungumzia Kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Ukisoma kitabu kile utagundua Kabla ya Yesu kuzaliwa kulikua Na Vita baina ya Uzao Na joka. Utaelewa vizuri ukisoma kitabu cha Matayo sura 2: kinatafsiri Unabii wa Ufunuo 12:

Kama unataka kuujua ukweli soma Ufunuo 12: sambamba Na Matayo 2: utaona Ufunuo 12: ilikua inanena unabii Ambao ulikuja kutimia kwenye Matayo 2:

Sasa hapa kanisa katoliki ndio lilipokosa tafsiri Na kupotosha. Ukweli ni kwamba Mama Maria Alikufa kama Watu wengine kabisa. Na sio kweli Amepalizwa mbinguni. Pia Hatuna mwombezi mwingine isipokua Yesu peke Yake kama kuhani Mkuu Anayetuombea mbele za Mungu. Soma 1 Yohana 2:1

Ushauri
Ni Vizuri sana kama wakristo tukawa wasomaji wa Neno la Mungu Na tusipende sana kusomewa maandiko Bali tunaposomewa neno la Mungu basi tuwe tayari Na Ufahamu maana Ufahamu uja kwa kulisoma Na kulielewa neno la Mungu.
 
Yesu anatoka kwa wayahudi na bibilia kwa waebrania, acha kutu lazimisha mambo kwa wakatoliki
Myahudi na muebrania alikua na torati yake,,,,biblia mmepewa na wakatoliki maana hakuna muasisi yeyote wa hivi vikanisa vyenu ambae alikua hayo maeneo ya wakina Yesu na maria enzi hizo zaidi ya wakatoliki...,,na mitume wote kazi zao zikaanzisha ukatoliki
 
Na hio biblia mnayofanya kutupigia kelele nayo humu mmepewa na wapagani,, bila wakatoliki msingemjua hata huyo yesu
Kaka Ucha Upotoshaji. Usilolijua Usilizungumze kaka. Ukristo haukuletwa Na wakatoliki Ukristo ulianzia kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume 11:26

Wakatoliki walikuja kuhodhi Ukristo kutokana Na Nguvu ya dola ya kirumi iliokua imetawala Dunia. Kwa kivuli cha kueneza dini.

Sasa kama huna fact ni bora usizungumze maana hujui historia.
 
Hicho kifungu ungeki quote wapi kama mkatoliki asingekuandikia hio biblia,,,hicho kitabu cha matendo ya mitume kimetoka mbiguni nacho, semeni mnavyotaka ila kwenye ukristo ukatoliki ni kama maji ndo baba yenu ndo mama yenu hamumkwepi
 
Nani kakwambia wakatoliki ndio wameleta biblia? Nenda katafute History ya Biblia Na MTU Aliye chapisha biblia uje Na Fact Kaka usilolijua usiliongee kwa kulewa Udhehebu kumbe hujui Kitu ni mfata upepotu.
 
We sema utakayo bila mkatoliki kukaa kukusanya hivyo vitabu na kutengeneza biblia leo hii msingekua na sehemu ya kukopi na kutupigia makelele
 
Nani kakwambia ukatoliki ndio ulikusanya nyaraka za biblia? Kaka acha ushabiki katafute history ya chanzo cha nyaraka za biblia alafu utagundua hujui Kitu zaidi umejaa ushabikitu.

Pia jua kwamba biblia sio Mali ya wakatoliki biblia ni Neno la Mungu kaka.

Biblia sio Mali ya mkatoliki au mpentekoste biblia ni neno la Mungu kwa watu wote.
 
Back
Top Bottom