Leo tarehe 15 August Wakristo Wanaadhimisha Sikukuu Ya Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria

View attachment 2718085

Ufunuo 12:1
"Kisha, ishara kubwa ikaonekana mbinguni: Mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!"

Luka 1:26
"Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, kwa msichana mmoja bikira aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu, ewe uliyejaliwa neema na Mungu! Bwana yuko nawe!” Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: Maneno hayo yanamaanisha nini? Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu. Yeye atakuwa mkubwa na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu"

Utangulizi: Tafakari ya Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria: Bikira Maria ni ishara na tumaini thabiti na ya faraja kwa taifa la Mungu linalosafiri. Tunaposherehekea Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Mama Bikira Maria, tunajifunza kuwa, Mama wa Yesu, akiwa amekwisha tukuzwa mbinguni mwili na roho, ni sura na mwanzo wa Kanisa ambalo litapata utimilifu wake katika ulimwengu ujao. Kadhalika anang’aa duniani kama alama ya hakika ya matumaini na ya faraja kwa Taifa la Mungu lililo safarini, mpaka siku ya Bwana itakapokuja (taz. 2Pet 3:10; Lumen Gentium, n. 68). Somo la kwanza: Ufunuo 11-.19; 12:1-6.10. Somo la pili: 1 Wakorinto 15:20-26. Injili: Luka 1:39-56. Karibu mpenzi msikilizaji wa Radio Vatican katika tafakari hii, leo ambapo Kanisa linaadhimisha Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Mama Bikira Maria Mtakatifu.

Tafakari: Moja ya mafundisho haya ya Kanisa ni kutoka katika somo la kwanza tulilosikia, kutoka kitabu cha Ufunuo wa Yohane 11:19; 12:1-6.10. Katika somo hili, Mababa wa Kanisa wanafundisha kuwa, kwanza somo linazungumzia mwanamke ambaye ni sura ya taifa la Mungu, ambalo ndilo Kanisa, ambapo pia Maria anawakilisha sura ya taifa la Mungu yaani Kanisa. Simulizi hili la joka linaturudisha kwenye kitabu cha Mwanza 3:15 ambapo Mungu aliweka uadui kati ya mwanamke na nyoka na kati ya uzao wa mwanamke na uzao wa nyoka ambaye ni shetani. Mwanamke aliyevikwa jua. Hii ni ishara ya kuwa mwanamke huyu amepambwa kwa neema za Mungu (salamu uliye jaa neema – salamu ya Malaika Gabrieli kwa Bikira Maria). Na mwezi chini ya miguu yake, maana yake kuwa mwanamke huyu hatapotea wala kuamgamia, bali ataishi milele. Na juu ya kichwa chake taji ya nyota 12, zinazowakilisha makabila 12 ya wana wa Israeli. Pia huwakilisha Mitume 12 ya Yesu, ikiwa na maana ya utawala wa Kanisa katika ulimwengu. Naye alikuwa na mimba akilia hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa. Hii li lugha ya picha inayoonesha mateso ya wokovu yaliyoletwa au kutimizwa na Kristo pale msalabani na hatimaye kufufuka kwa ushindi. Naye akazaa mtoto wa kiume – huyu ndiye Kristo Yesu Mkombozi wa ulimwengu, na mtoto huyu akanyakuliwa hata kwa Mungu, picha ya mateso, kifo, ufufuko na kupaa mbinguni kwa Kristo. Mwanamke akakimbilia nyikani, hii huwakilisha ukimbizi wa Wakristo wa kwanza kwa sababu ya mateso.

Tuhitimishe tafakari yetu kwa kusema kuwa tusihofu kumsifu Maria kwa sababu kila mara tunapomsifu Maria, yeye mara moja huzigeuza sifa hizo kuwa za Mungu. Ndio maana Elizabeti alipomsifu, mara moja Bikira Maria akasema “Moyo wangu wamtukuza Bwana...” Utenzi huu unaeleza hali ya kiroho ya Bikira Maria, na hakuna kitu kikubwa zaidi ya hali hii ya kiroho kwa ajili ya kutusaidia kupata uzoefu wa Fumbo la Ekaristi. Ekaristi imetolewa kwetu ili maisha yetu, kama yale ya Bikira Maria, yawe ya ukuu kabisa. Kwa maana “Mama anapoheshimiwa, Mwana hupata kujulishwa, kupendwa na kutukuzwa inavyostahili, na amri zake kushikwa, kwa kuwa katika Yeye vitu vyote viliumbwa (rej. Kol 1:15-16) na katika yeye ilimpendeza Baba wa milele utimilifu wote ukae (rej. Kol 1:19).” Tumtazame Bikira Maria, yeye anatufungulia matumaini ya wakati ujao uliojaa furaha na anatufundisha njia ya kuufikia: yaani kumpokea mwanaye kwa imani; daima tusipoteze urafiki wetu na mwanaye, bali tujiachilie ili, Mwanaye atuangazie mwanga wake na atuongoze kwa Neno lake; tumfuase mwanaye kila siku, hata nyakati ambazo tunahisi misalaba yetu kuwa mizito. Maria Sanduku la Agano Jipya aliye Mbinguni, anatuonesha kwa mwanga halisi kwamba tupo katika njia tukielekea katika nyumba yetu ya kweli, yaani ushirika wetu wa furaha na amani pamoja na Mungu. Hivyo, waamini wote wakristo wamsihi kwa nguvu Mama wa Mungu na Mama wa wanadamu, ili yeye aliyeusaidia mwanzo wa Kanisa kwa maombezi yake, pia sasa aliyetukuzwa mbinguni, juu ya Wenye heri na Malaika, awaombee kwa Mwanawe katika Ushirika wa Watakatifu wote, mpaka jamaa zote za Mataifa zilizopambwa jina la Kristo au zisizomjua bado Mwokozi wao, zikusanyike kwa furaha kuwa Taifa moja la Mungu katika amani na mapatano, kwa utukufu wa Utatu Mtakatifu sana usiogawanyika. Amina.

Tumsifu Yesu Kristu!
Mkuu badirisha heading, sio "wakristo"
Sema" waroman " yaani RC

Wakristo wa madhehebu mengine haya hatuyajui
 
It's true!
Asitujumuishe haya ni mambo ya Roman Catholic
Wanasema Wana mama Yao huko juu ,

ETI MUNGU kachukua , jiko Duniani, kampaisha juu,

Ni laana Sana hio ,thehebu,

Maria baada ya kuliwa Sana na josefu kitandani,

Mungu kaona amchukue mwenyewe juu,

Huu ni uchafu mkubwa, ndio maana wajiangalie Sana wanao ingia huko,
 
Ukatoliki ukiuendea kichwakichwa hutaelewa,,mambo mengi ni mafumbo elimu zao zilianzia misri kwa wakina isis na horus,
 
POKEO LOLOTE NJE YA USHAHIDI WA KIBIBLIA ,NI _ _ _Utapeli

MSINGI KAMILI WA UKRISTO NI YESU NA MITUME 12,

NA ULIANZISHWA NA YESU, BAADA NA KABLA YA HAPO HAKUKUWA NA MSINGI MWENGINE NA HAUTAKUWEPO,

KUMBE WENZETU WAMECHUKUA MAMBO MENGINE YA HUKO MISRI KUWA SEHEMU YA MISINGI YA UKRISTO
 
Mimi ni Mkristo ila sikubaliani na fundisho la bikira Maria kuitwa Mama wa Mungu, au kwamba alipalizwa. Kwahiyo usijumuishe Wakristo wote kwenye huo utopolo.
Wamenyewe wanadai.Papa akikaa kwenye kiti chake cha upapa.Chochote atakachosema hakina makosa.
Inategemeana na Papa amelala na kuamka vipi.Siyo maandiko yanasema vipi.
 
Wewe huna imani ya ukatoliki mengi tunaamini tu ili ya ishe hicho ndo kinacho itwa imani wewe usilete logic zako hapa, Dini ya RC haina logic kabisa, wewe ulisha wahi kuona wapi 1+1+1=1!!!! Ila kwa imani ya kikatoliki ni sawa, Mungu baba+ Mungu mtoto+ Mungu roho mutakatifu =1mungu moja [emoji1787][emoji1787][emoji7][emoji1787][emoji1787][emoji7]
Hebu taucheni uongo jamani.Ni wapi imani ya kidini inasema 1+1+1 =1.
Hata tunaonaimini Mungu mmoja nafsi tatu.Bado hatuamini 1+1+1=1.Hesabu zitabaki kuwa hesabu na asili ya Mungu mmija nafsi tatu itabaki kuwa hivyo.Hivyo ni vitu viwili tofauti.Heaavu kule Mungu huku.
 
Wakristo au wakatoliki? Hizo ni sikukuu walizojitungia wakatoliki tu. Tarehe ya kuzaliwa wala kufa kwa Yesu kristo haijulikani iweje siku ya kupaa kwa mama yake Yesu? Nani ana ushahidi wa kupaa kwa Mama yake Yesu?
 
Unamaanisha Nini unaposema Kwa mfano wetu?

Binadamu amefanana na Mungu?
Naam na hakika, ni kiumbe pekee aliyepewa utashi, anaeweza kuzungumza kujiamulia mambo yake na kuongeza ufahamu n.k na mfano wake ni anayeweza kusifu, kuabudu huu mfano tumepewa kutoka kwa Baba pekee
 
View attachment 2718085

Ufunuo 12:1
"Kisha, ishara kubwa ikaonekana mbinguni: Mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!"

Luka 1:26
"Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, kwa msichana mmoja bikira aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu, ewe uliyejaliwa neema na Mungu! Bwana yuko nawe!” Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: Maneno hayo yanamaanisha nini? Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu. Yeye atakuwa mkubwa na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu"

Utangulizi: Tafakari ya Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria: Bikira Maria ni ishara na tumaini thabiti na ya faraja kwa taifa la Mungu linalosafiri. Tunaposherehekea Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Mama Bikira Maria, tunajifunza kuwa, Mama wa Yesu, akiwa amekwisha tukuzwa mbinguni mwili na roho, ni sura na mwanzo wa Kanisa ambalo litapata utimilifu wake katika ulimwengu ujao. Kadhalika anang’aa duniani kama alama ya hakika ya matumaini na ya faraja kwa Taifa la Mungu lililo safarini, mpaka siku ya Bwana itakapokuja (taz. 2Pet 3:10; Lumen Gentium, n. 68). Somo la kwanza: Ufunuo 11-.19; 12:1-6.10. Somo la pili: 1 Wakorinto 15:20-26. Injili: Luka 1:39-56. Karibu mpenzi msikilizaji wa Radio Vatican katika tafakari hii, leo ambapo Kanisa linaadhimisha Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Mama Bikira Maria Mtakatifu.

Tafakari: Moja ya mafundisho haya ya Kanisa ni kutoka katika somo la kwanza tulilosikia, kutoka kitabu cha Ufunuo wa Yohane 11:19; 12:1-6.10. Katika somo hili, Mababa wa Kanisa wanafundisha kuwa, kwanza somo linazungumzia mwanamke ambaye ni sura ya taifa la Mungu, ambalo ndilo Kanisa, ambapo pia Maria anawakilisha sura ya taifa la Mungu yaani Kanisa. Simulizi hili la joka linaturudisha kwenye kitabu cha Mwanza 3:15 ambapo Mungu aliweka uadui kati ya mwanamke na nyoka na kati ya uzao wa mwanamke na uzao wa nyoka ambaye ni shetani. Mwanamke aliyevikwa jua. Hii ni ishara ya kuwa mwanamke huyu amepambwa kwa neema za Mungu (salamu uliye jaa neema – salamu ya Malaika Gabrieli kwa Bikira Maria). Na mwezi chini ya miguu yake, maana yake kuwa mwanamke huyu hatapotea wala kuamgamia, bali ataishi milele. Na juu ya kichwa chake taji ya nyota 12, zinazowakilisha makabila 12 ya wana wa Israeli. Pia huwakilisha Mitume 12 ya Yesu, ikiwa na maana ya utawala wa Kanisa katika ulimwengu. Naye alikuwa na mimba akilia hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa. Hii li lugha ya picha inayoonesha mateso ya wokovu yaliyoletwa au kutimizwa na Kristo pale msalabani na hatimaye kufufuka kwa ushindi. Naye akazaa mtoto wa kiume – huyu ndiye Kristo Yesu Mkombozi wa ulimwengu, na mtoto huyu akanyakuliwa hata kwa Mungu, picha ya mateso, kifo, ufufuko na kupaa mbinguni kwa Kristo. Mwanamke akakimbilia nyikani, hii huwakilisha ukimbizi wa Wakristo wa kwanza kwa sababu ya mateso.

Tuhitimishe tafakari yetu kwa kusema kuwa tusihofu kumsifu Maria kwa sababu kila mara tunapomsifu Maria, yeye mara moja huzigeuza sifa hizo kuwa za Mungu. Ndio maana Elizabeti alipomsifu, mara moja Bikira Maria akasema “Moyo wangu wamtukuza Bwana...” Utenzi huu unaeleza hali ya kiroho ya Bikira Maria, na hakuna kitu kikubwa zaidi ya hali hii ya kiroho kwa ajili ya kutusaidia kupata uzoefu wa Fumbo la Ekaristi. Ekaristi imetolewa kwetu ili maisha yetu, kama yale ya Bikira Maria, yawe ya ukuu kabisa. Kwa maana “Mama anapoheshimiwa, Mwana hupata kujulishwa, kupendwa na kutukuzwa inavyostahili, na amri zake kushikwa, kwa kuwa katika Yeye vitu vyote viliumbwa (rej. Kol 1:15-16) na katika yeye ilimpendeza Baba wa milele utimilifu wote ukae (rej. Kol 1:19).” Tumtazame Bikira Maria, yeye anatufungulia matumaini ya wakati ujao uliojaa furaha na anatufundisha njia ya kuufikia: yaani kumpokea mwanaye kwa imani; daima tusipoteze urafiki wetu na mwanaye, bali tujiachilie ili, Mwanaye atuangazie mwanga wake na atuongoze kwa Neno lake; tumfuase mwanaye kila siku, hata nyakati ambazo tunahisi misalaba yetu kuwa mizito. Maria Sanduku la Agano Jipya aliye Mbinguni, anatuonesha kwa mwanga halisi kwamba tupo katika njia tukielekea katika nyumba yetu ya kweli, yaani ushirika wetu wa furaha na amani pamoja na Mungu. Hivyo, waamini wote wakristo wamsihi kwa nguvu Mama wa Mungu na Mama wa wanadamu, ili yeye aliyeusaidia mwanzo wa Kanisa kwa maombezi yake, pia sasa aliyetukuzwa mbinguni, juu ya Wenye heri na Malaika, awaombee kwa Mwanawe katika Ushirika wa Watakatifu wote, mpaka jamaa zote za Mataifa zilizopambwa jina la Kristo au zisizomjua bado Mwokozi wao, zikusanyike kwa furaha kuwa Taifa moja la Mungu katika amani na mapatano, kwa utukufu wa Utatu Mtakatifu sana usiogawanyika. Amina.

Tumsifu Yesu Kristu!
Waliopaa bila kuonja Mauti.
1. Enock
2. Elia.

Aliyepa baada ya Mauti.
1.Yesu/Mungu katika utatu.

Mariamu si Bikra bada ya kumzaa Yesu aliolewa na kuendelea kuzaa watoto wengine wengi tu na mume wake Yusuph.

Kuna Dini flani imemfanya Mariam kuwa bikra wakati alipozaa aliendelea kufanya mapenzi na Yusufu/mume wake na kupata watoto.

Mariam alikufa na sasa anasubiri ufufuo, Mungu hana upendeleo eti kisa Yesu alipitia tumbo la Mariam ndio apalizwe, hizi story za Wazungu!
 
Mwamba martin luter aliyakataa hayo mafundisho feki

Kwanza Hayana ushahidi wa kutosha
 
Mwamba martin luter akiyakataa hayo mafundiko feki

Kwanza Hayana ushahidi wa kutosha
Ushahidi wa nini mkuu, Mungu mmoja nafsi tatu.
Huyo mama ni lisanamu dini flani imejichongea na ukiwakuta wanalisujudu, wanalibeba dar nzima kwa maandamano ukiwaambia wanaliabudu wanakataa wanasema wanaliheshimu.

elimu yao ni kama mavi[mtum Paulo alisema] !
 
Waliopaa bila kuonja Mauti.
1. Enock
2. Elia.

Aliyepa baada ya Mauti.
1.Yesu/Mungu katika utatu.

Mariamu si Bikra bada ya kumzaa Yesu aliolewa na kuendelea kuzaa watoto wengine wengi tu na mume wake Yusuph.

Kuna Dini flani imemfanya Mariam kuwa bikra wakati alipozaa aliendelea kufanya mapenzi na Yusufu/mume wake na kupata watoto.

Mariam alikufa na sasa anasubiri ufufuo, Mungu hana upendeleo eti kisa Yesu alipitia tumbo la Mariam ndio apalizwe, hizi story za Wazungu!
Kwa roma hilo ni fumbo, na mkilifatilia kwa biblia tu hamtakuja kulielewa maana ukatoliki hautumii biblia peke yake kwa mafundisho ya kanisa
 
Malizaneni kanisani huko sisi wengine hatuamini maswala ya bikira aliyezaa Watoto zaidi5
 
Sijataja Dini, inafahamika WA-kristo[Wafuasi wa Yesu] dunia nzima wanatumia BIBLIA. Kaa ni U-Kristo ulianzia Israeli ya Uyahudi na Waroma ndio walimpinga na kumsulubisha.

Yesu alisulubishwa na Warumi kwa amri ya Pilato, ambaye alikuwa gavana wa Kirumi wa Yudea wakati huo.

Sasa kama wanatumia vitabu vingine si ndio vile vya mafarisayo na masadukayo?
 
Pharao , Mariamu Mke wa Yusufu alizaa watoto 6 .
Unaweza kufanya mapenzi na mumeo na kuzaa ukabaki bikra?
Hiyo elimu ya dini wanayosemaga wanasoma kuliko dini zingine zinawasaidiaga nini?
Mungu haongozwi na maelimu ya darasani, ROHO MTAKATIFU NDIO MWALIMU MKUU.
 
Sijataja Dini, inafahamika WA-kristo[Wafuasi wa Yesu] dunia nzima wanatumia BIBLIA. Kaa ni U-Kristo ulianzia Israeli ya Uyahudi na Waroma ndio walimpinga na kumsulubisha.

Yesu alisulubishwa na Warumi kwa amri ya Pilato, ambaye alikuwa gavana wa Kirumi wa Yudea wakati huo.

Sasa kama wanatumia vitabu vingine si ndio vile vya mafarisayo na masadukayo?
Hio biblia bila wakatoliki msingeipata, ndo maana hawanaga shida na hivi vidhehebu vya ajabu maana ndo vinawashambulia kweli wakati ni watoto tu kwao
 
Kwamba ISRAEL NI WAKATOLIKI?
Kwamba Biblia imeanzia Roma?
Kwamba Paulo, Matayo, Luka walikuwa Warumi?
Unajua waandishi wa biblia wewe bwana katekista?
Unajivunia dini na dhehebu zinazofanya ushoga na kubaka watoto?

Yesu Kristo alizungumzia dini kwa njia mbalimbali katika mafundisho yake, akisisitiza umuhimu wa uhusiano wa kweli na Mungu juu ya utekelezaji wa taratibu na mila za kidini. Yafuatayo ni baadhi ya mafundisho muhimu ya Yesu kuhusu dini:

  1. Upendo na Haki: Yesu alisisitiza upendo kwa Mungu na jirani kama amri kuu. Alisema, "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote" na "Mpende jirani yako kama nafsi yako" (Mathayo 22:37-39). Aliweka wazi kuwa amri hizi mbili zinajumlisha sheria na manabii.​
  2. Unyenyekevu na Unafiki: Yesu alikemea vikali unafiki wa viongozi wa kidini wa wakati wake, Mafarisayo na Masadukayo. Alionya dhidi ya kufanya matendo ya dini ili kuonekana na watu, akisema, "Lakini wewe utoapo sadaka, usijue mkono wako wa kushoto kile ufanyacho mkono wako wa kuume" (Mathayo 6:3).​
  3. Uhusiano na Mungu: Yesu alifundisha kuwa uhusiano wa kibinafsi na Mungu ni muhimu zaidi kuliko taratibu za kidini. Aliwaambia wanafunzi wake kuwa Mungu ni Baba mwenye upendo ambaye anataka kujenga uhusiano wa karibu na watoto wake (Mathayo 6:9-13).​
  4. Kutimiza Sheria na Manabii: Yesu alisema kuwa hakuja kuitangua sheria bali kuitimiza. Alifafanua kwamba haki ya kweli inatokana na moyo safi na siyo utekelezaji wa nje wa sheria tu (Mathayo 5:17-20).​
  5. Mambo ya Ndani na ya Nje: Yesu alifundisha umuhimu wa usafi wa moyo kuliko usafi wa nje. Aliwakemea wale waliokuwa wakijali zaidi taratibu za nje huku mioyo yao ikiwa mbali na Mungu, akisema, "Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutojizuia" (Mathayo 23:25).​
 
Back
Top Bottom