Leo tarehe 16 Machi 2022 NATO waanza mazoezi makali ya kijeshi

Leo tarehe 16 Machi 2022 NATO waanza mazoezi makali ya kijeshi

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Nimeiona hii habari Al Jazeera.
Umoja wa NATO wamekutana katika mji wa Oslo Norway na kuanza mazoezi makubwa ya kivita ambayo hayajawahi kufanyika kabla.

Mazoezi hayo ambayo wao wamedai ni mazoezi ambayo hufanyika Kila baada ya miaka miwili yatahusisha kujikinga na mashambulizi ya nyukilia, na aina mbalimbali ya mashambulizi.

Wazo langu, hata Urusi ilianza mazoezi namna hii huko Beralusi na baadae ikaingia Ukraine.

NAKO TAIWAN, Leo hii.

Leo tarehe 16 machi 2022 Taiwan imeanza mazoezi makali sana ya kumzuia Adui asiingie katika visiwa hivyo, baada ya kuona Ukraine kavamiwa na Urusi

Naomba kuwasilisha.
 
Mimi namshauri Mh. Rais wa Tanzania mama samia suluhu. Awaambie watanzania wote waliopo Urusi na nchi za NATO warudi Tanzania haraka ikiwa pamoja na mabalozi wetu waliomo kwenye hizo nchi.

Pia jeshi letu lianze mazoezi kujiweka tayari tayari kwa lolote
 
Mimi namshauri Mh. raisi wa Tanzania mama samia suluhu. Awaambie watanzania wote waliopo urusi na nchi za NATO warudi Tanzania haraka ikiwa pamoja na mabalozi wetu waliomo kwenye hizo nchi.
Pia jeshi letu lianze mazoezi kujiweka tayari tayari kwa lolote
Tushafanya mazoezi ya kuvunja tofari mkuu bado nini tukumbushe basi..😊
 
Kama Ukraine wiki ya tatu hii hapo kyiv hamjakanyaga ndio mtawaweza NATO?
Kwani hapo Ukraine unadhani NATO hawashiriki? Hizo military supplies, mercenaries na vikwazo dhidi ya urusi ndo kushiriki kwenyewe. BTW hivi NATO walitumia muda gani kumwangusha Gadafi pale Libya? Vipi marekani na it's allies pale kwa Sadam Iraq ilikuwaje? Na vipi wamarekani wameshamuondoa Assad pale Syria? Naomba majibu tafadhali.
 
akikujibu naomba unitag tafadhali namie nijionee hayo majibu utojibiwa
 
Nimeiona hii habari Al Jazeera.
Umoja wa NATO wamekutana katika mji wa Oslo Norway na kuanza mazoezi makubwa ya kivita amabyao hayajawahi kufanyika kabla.

Mazoezi hayo ambayo wao wamedai ni mazoezi ambayo hufanyika Kila baada ya miaka miwili yatahusisha kujikinga na mashambulizi ya nyukilia, na ainabalimbali ya mashambulizi.

Wazo langu,hata Urusi ilanza mazoezi namna hii huko Beralusi,na baadae ikaingia Ukraine.

NAKO TAIWAN,Leo hii.

Leo tarehe 16 machi 2022 Taiwan imeanza mazoezi makali sana ya kumzuia Adui asiingie katika visiwa hivyo,baada ya kuona Ukraine kavamiwa na Urusi

Naomba kuwasilisha.
Habari tamu sana hizi
 
Back
Top Bottom