Leo tarehe 9 September Apple wamezindua iPhone 17 series na accessories nyingine!

Leo tarehe 9 September Apple wamezindua iPhone 17 series na accessories nyingine!

Mkuu iphone ni simu nzuri tatio wabongo wengi wanaziponda kwa sababu hatuna huwezo wa kununua.
Iphone ni simu nzuri ila android inakupa machaguo mengi. Nimetumia zote kuna vitu kwenye iphone wameweka complications zisizokuwa na maana.
Kama unataka kuamisha vitu kwenye window kwenda iphone 😩
Kuweka nyimbo kwenye iphone 😩
App Ingine za bure kwenye android iphone inabidi upasuke.
Napenda Samsung ila nashindwa kuihama tena iphone
 
Mkuu iphone ni simu nzuri tatio wabongo wengi wanaziponda kwa sababu hatuna huwezo wa kununua.
Iphone ni nzuri ukishaizoea ila kama umetoka moja kwa moja kwenye android utaichukia, kila kitu kimekaa kinyume nyume. Miaka yote nimekua nikitumia Samsung.
Iphone ya kwanza kununua mwezi tu ilinishinda nikagawa, iphone ya pili nilipewa zawadi, ilinisumbua kutumia ila ilibidi nikomae nayo mana Samsung yangu ilikua inasumbua mbovu mbovu na sikua na bajeti ya kununua simu mpya, ya tatu nimenunua mwenyewe baada ya kunogewa.
 
IMG_7581.jpeg
Huku tumeshaanza kuijadili hata bado hawajatangaza lolote.
Google upate taarifa kamili kama 13 bado inapokea updates..
Kwa mimi sikushauri labda 14
 
Wakuu, leo September 9 Apple wamezindua simu zao mpya iPhone 17 series pamoja na bidhaa nyingine kama airpods na Apple watch matoleo mapya.

Kwa kuanza na iPhone, jumla ya simu nne zimezinduliwa na CEO wao Tim Cook. Simu tajwa ni iPhone 17, iPhone Air, iPhone 17 Pro na iPhone 17 Pro Max.

iPhone 17 (Base)
iPhone 17 ambayo ndio base model ina cha kioo cha 6.3 inch, Apple A19 chipset, 8GB RAM na storage ya 128/256/512GB.

Kwenye camera ipo na 48MP main camera na 48MP ultrawide lenses na selfie 18MP. Battery lililopo ni 3,600mAh. Pia iPhone wamesema base mode itaanza kwa $900 na utachagua rangi Black, White, Lime, au Red.

Kwahiyo ukifananisha na iPhone 16 ya mwaka jana, tuna camera mpya, kioo kimeongezeka kidogo, chip mpya, battery kidogo kubwa ila ila muonekano karibia sawa.

iPhone Air

Hii ni ingizo jipya katika iPhone series. Ipo na specs karibia zote kama za base iPhone 17 mfano A19 Pro chip, 8GB RAM, ila ina camera moja ya 48MP, na 18MP selfie, kioo kikubwa zaidi cha inch 6.5 Super Retina OLED ikiwa na refreshrate ya 120Hz.

Hii simu ni nyembamba sana just 5.6 mm na battery limepungua sana hadi 2,800mAh lengo kuu ikiwa ni kuifanya iwe nyembamba sana. Na pia itakua e-SIM model tu.

Pamoja na vyote, iPhone 17 Air inauzwa kuanzia $1,000 na rangi zitakua kama kwenye 17 base.

iPhone 17 Pro

Kipenzi cha wengi ni Pro na Pro Max. Hawa maarufu kama macho matatu watakua na camera za nyuma tatu, mbili kama za kwenye base 48MP main na 48MP Ultrawide, sasa ya tatu ni 48MP telephoto lens.

Tukianza na huyu iPhone 17 Pro, ina kioo cha 6.3 inch kama base, pia imepewa chip mpya A19 Pro kama wenzie, 12GB RAM na storage inaanzia 128GB hadi 1TB na huku ikiwa na battery la 3700mAh.

Kuhusu rangi, zilizopo ni White, Black, Blue, na Gold, na bei ni kuanzia $1,110.

iPhone 17 Pro Max

Bwana mkubwa Pro Max ana kioo cha 6.9 inch, A19 Pro chip, 12GB RAM na storage itaanzia 256GB hadi 1TB na battery la 5,000mAh.

Rangi zitakua kama kwenye Pro ila bei itaanzia $1,397 tu.

Airpods Pro 3

Kama wewe ni mdau wa EarPods, basi tutakubaliana hamna inayozido Airpods Pro likija kwenye swala la music, calls na noise cancellation.

Sasa Apple wamezindua pia leo Pro 3, ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu toka wazindue Pro 2 wanavyotoa iPhone 14.

Pro 3 inakuja na chip mpya ya H3, pia ina health sensors kwaajili ya kupima mapigo ya moyo na joto. Pia Pro 3 imepewa live translation ability kwaajili ya kuwasiliana na mtu ambae mnaongea lugha tofauti.

Apple Watches

Apple hawajaishia kuzindua simu na EarPods tu, wamezindua pia smartwatches zao.

Jumla ya saa tatu zimezinduliwa, Apple Watch Series 11, Ultra 3 na wameongeza kitu kipya Watch SE 3.

Series 11 haijabadirika sana kutoka series 10 ya mwaka jana, ila imeongezewa blood pressure detection.

Ultra 3 imekuja muda muafaka, ukichukulia mwaka jana hawakuleta Ultra mpya. Imeongezwa 5G connectivity na sasa ina support satellite messaging.

Model ya Watch SE 3 ni cheap version ya series 11.

SE itauzwa kuanzia $ 249, Series 11 $399 na Ultra 3 $799.

Itoshe kusema tu Kwamba iPhone ni simu za Wanawake, mwanaume ukitumia hii simu wewe ni Anko T au NOELI au upinde
 
Me nimerudi Android, nipo na Pixel 8 sahivi. Nitakomaa nayo miaka 2 nitacheki Pixel 10 au S25 hivi.

Mdogo ndogo, hapo iPhone watakua na iPhone 20 sijui, Bei ya Bajaji.
Mkuu hapo naona s25 ndiyo iko vizuri zaidi kuliko zote.japo pixl kwenye kamera yuko vizuri
 
Back
Top Bottom